Wewe ni mwiziMshamba huyo hajui mimi pia nilishachukua kiwanja kwa staili hiyo walikuja vijana wenye eneo baada ya dingi yao kuvuta nilishajenga..eti walinunua laki tatu mwaka 2001. Hawana hata hati wamekuja na kimkataba kilishanyewa na mende mm nikatoa hati wakafunga mdomo wakaondoka be capitalist in life hakuna huruma.
Mkuu hii ni mkoa gani?Kwa nyumba sijui ipoje ila kwa kiwanja afadhali
Mi nilijipatia kiwanja kwa namna hiyo
Kilikuwa ubavuni kwangu na mwenyewe hakuwahi kuonekana
Nikaenda ardhi nikawaeleza wakaniambia kasafishe kwanza ukiona kimya weka msingi tulia
Nilifanya hivyo na hakutokea mtu lakini palikuwa ma tofali 12 pale chini
Baada ya mwaka nikaenda ardhi nikawaeleza wakanipa offer/hati na hadi leo napamiliki
Unaweza kuichukua,lkn ukajikuta kwenye matatizo makubwa.Ukute nyumba hiyo ina Mazingaombwe mengi yaani full vibwengo na mauzauza.Kuna nadharia mbili hapa.
1. Yawezekana mmiliki alikuwa anamjengea mchepuko. Ili siku moja aje amfanyie surprise. Lkn kabla ya surprise jamaa akapata ugonjwa ama ajali na kufariki. Kwahiyo si mchepuko wala familia waijuao nyumba hii.
2. Mmiliki alipoikamilisha alipigwa kifungo cha miaka 30 au zaidi jela.
Je, nijitwale hii nyumba? Vipi kama nadharia ya 2 ndiyo sahihi? Akitoka jela na kurudi uraiani itakuwaje? Ingawa kuna usemi wa kiswahili unanipa moyo "cha kuokota siyo cha kuiba, mwenye mali mpumbavu".
Hana hata baadhi yaliyo ya kweli?
How mkuu? Mbona hufunguki?[emoji1787][emoji1787]
Nyumba za namna hiyo ni hatari sana mkuu
Alishasema hana jinsia, utakavyokuja ndivyo utakavyopokelewa.
Shem ni wewe!Wewe hamia yatakuwa ndio mahari yako hayo, mwenyewe atakaporudi anakuoa kiroho safi.
Akisubiri miaka 12 ndiyo achukue, maana yake ni kwamba sheria inaanza kuhesabu kuanzia siku alipoitwaa hiyo nyumba na siyo kuanzia siku ilipotelekezwa na aliyeijengaSubiri itimie miaka 12 uichukue.
Sheria inatambua abondoned baada ya miaka 12
Mimi ubavuni kwangu kuna viwanja 2 double sijui vya mtu mmoja au la.Mwaka 2009 tulienda na rafiki yangu Bunju kununua Viwanja,tukaanza kujenga mdogomdogo lakini rafiki yangu (RIP)alijenga fasta ikabaki kupaua tu(kumbuka wote tulikuwa mabachela). Siku moja anatoka site akapata ajali Tegeta(aligongana na Lori),alifariki palepale. Huyu rafiki yangu tulikuwa tumepanga nyumba moja Sinza(yeye Chumba chake,mimi changu lakini sebule,jiko nk tunashea. Tangu tunanunua Viwanja mpaka anafariki hakuna aliyewahi kumpeleka site ndugu,rafiki wala jamaa. Hivyo nyumba niliiokota kwa style hiyo,niliipaua,nikaifanyia finishing na sasa nakula Kodi. Lakini kwa kuwa tulikuwa tumeshibana sana hivyo huwa najitajidi kuwatumia Pesa Wazazi wake Moshi kila mwezi,na wamekuwa kama Wazazi wangu na wananiita mwanao.
SWALI KWA NINI SIKUIPA TAARIFA FAMILIA HIYO?huyu Marehemu rafiki yangu ndie aliyekuwa amesoma kwao,Kaka na Dada zake wote ni wale waleviwalevi waliojichokea tu,hivyo kama ningetoa taarifa naamini wangeshauri nyumba iuzwe tu wapate Pesa ya kunywea pombe. Tangu niikamilishe mwaka 2011 mpaka leo nakula Kodi tu,Hati nilishaipata kwa jina langu na maisha yanasonga.
Ahaaa hapo nimekusoma mwanasheria wangu.Akisubiri miaka 12 ndiyo achukue, maana yake ni kwamba sheria inaanza kuhesabu kuanzia siku alipoitwaa hiyo nyumba na siyo kuanzia siku ilipotelekezwa na aliyeijenga
Safi. Kuitwaa nyumba siyo lazima ufanye vitu vikubwa sana.Nyumba za namna hiyo zipo nyingi mno hasa jijini Dar es salaam.
Mahali ninapoishi,kuna nyumba zimejengwa kwa mfuatano zikiwa 3,inasemekana Mzee anao watoto 3 aliamua kuwajengea hizo nyumba,mzee alifariki ila madogo wapo wanaishi nje ya nchi!
Walikuja kipindi fulani( Zaidi ya mika 10 iliyopita) wakaangalia zile nyumba na mahali zilipo wakasema hawazihitaji!.
Kuna Sheikh mmoja ameamua kujimegea moja anaishi na familia yake,zile nyingine 2 zinazidi kuota nyasi tu na nyoka kujazana huko ndani!.
Nyumba ni nzuri na naza kisasa mno!,lakini madogo walisema hawawezi kuja kuishi Tanzania.
Sasa wenyeji kila mmoja anaogopa na kusema wanaweza kushitakiwa,lakini ukweli ni kwamba hakuna mtu wa kukushitaki wala nini!.
Ngoja nivute muda,mwakani nasafisha moja naingia,mdogo mdogo hadi inakuwa yangu!
Maana kwa dalili zilizopo hakuna wa kuhoji zaidi ya kuendelea kuchakaa!,Siku watu wa Ardhi wakishituka zitakwenda na maji!.
Mwakani najimilikisha moja!
Safi. Kuitwaa nyumba siyo lazima ufanye vitu vikubwa sana.
Unaweza ukuwa unaenda kuwasha taa na kuzima, kama umeme upo
Mwagilia maua
Panda miti
Kaa kibarazani😀
Fungua na kufunga milango
Washa moto upike
Fanya vikao vya familia
Lima majani huko nje
Panda ukoka
Safisha dari ondoa bui bui
Nenda msalani
Fukuza watoto wanaocheza kibarazani
Fanya jambo lolote ambalo litakupa hadhi ya umiliki.
Dadeki🙆Mimi ubavuni kwangu kuna viwanja 2 double sijui vya mtu mmoja au la.
Tangu 2020 nianze kuja huku mara kwa mara na 2021 nilipohamia sijamwona mwenyewe.
Nalima mbogamboga na mihogo.
Nawaza sijui nipige ukuta kote au nitulie kwanza.
Wanadamu tuache ubinafsi, mali zako mtu hutaki hata kumeonyesha mke ukifa je!
Kumiliki ardhi ni tofauti na kutawala ardhi.Mkuu haya yote nitayafanya,Ahsante kwa mbinu 🤣
Kisheria hii inatwa 'bad means for good motive'.Mwaka 2009 tulienda na rafiki yangu Bunju kununua Viwanja,tukaanza kujenga mdogomdogo lakini rafiki yangu (RIP)alijenga fasta ikabaki kupaua tu(kumbuka wote tulikuwa mabachela). Siku moja anatoka site akapata ajali Tegeta(aligongana na Lori),alifariki palepale. Huyu rafiki yangu tulikuwa tumepanga nyumba moja Sinza(yeye Chumba chake,mimi changu lakini sebule,jiko nk tunashea. Tangu tunanunua Viwanja mpaka anafariki hakuna aliyewahi kumpeleka site ndugu,rafiki wala jamaa. Hivyo nyumba niliiokota kwa style hiyo,niliipaua,nikaifanyia finishing na sasa nakula Kodi. Lakini kwa kuwa tulikuwa tumeshibana sana hivyo huwa najitajidi kuwatumia Pesa Wazazi wake Moshi kila mwezi,na wamekuwa kama Wazazi wangu na wananiita mwanao.
SWALI KWA NINI SIKUIPA TAARIFA FAMILIA HIYO?huyu Marehemu rafiki yangu ndie aliyekuwa amesoma kwao,Kaka na Dada zake wote ni wale waleviwalevi waliojichokea tu,hivyo kama ningetoa taarifa naamini wangeshauri nyumba iuzwe tu wapate Pesa ya kunywea pombe. Tangu niikamilishe mwaka 2011 mpaka leo nakula Kodi tu,Hati nilishaipata kwa jina langu na maisha yanasonga.
Inategemea na Nyumba iko wapi..Kuna nadharia mbili hapa.
1. Yawezekana mmiliki alikuwa anamjengea mchepuko. Ili siku moja aje amfanyie surprise. Lkn kabla ya surprise jamaa akapata ugonjwa ama ajali na kufariki. Kwahiyo si mchepuko wala familia waijuao nyumba hii.
2. Mmiliki alipoikamilisha alipigwa kifungo cha miaka 30 au zaidi jela.
Je, nijitwale hii nyumba? Vipi kama nadharia ya 2 ndiyo sahihi? Akitoka jela na kurudi uraiani itakuwaje? Ingawa kuna usemi wa kiswahili unanipa moyo "cha kuokota siyo cha kuiba, mwenye mali mpumbavu".