Hapa jirani yangu pana nyumba haijawahi kukaliwa na watu tokea ikamilike kujengwa. Ni mwaka wa 10 huu, mpaka geti linaanza kuoza. Nijitwalie?

Mshamba huyo hajui mimi pia nilishachukua kiwanja kwa staili hiyo walikuja vijana wenye eneo baada ya dingi yao kuvuta nilishajenga..eti walinunua laki tatu mwaka 2001. Hawana hata hati wamekuja na kimkataba kilishanyewa na mende mm nikatoa hati wakafunga mdomo wakaondoka be capitalist in life hakuna huruma.
Wewe ni mwizi
 
Kwa nyumba sijui ipoje ila kwa kiwanja afadhali
Mi nilijipatia kiwanja kwa namna hiyo
Kilikuwa ubavuni kwangu na mwenyewe hakuwahi kuonekana
Nikaenda ardhi nikawaeleza wakaniambia kasafishe kwanza ukiona kimya weka msingi tulia

Nilifanya hivyo na hakutokea mtu lakini palikuwa ma tofali 12 pale chini
Baada ya mwaka nikaenda ardhi nikawaeleza wakanipa offer/hati na hadi leo napamiliki
Mkuu hii ni mkoa gani?
 
Kuna nadharia mbili hapa.

1. Yawezekana mmiliki alikuwa anamjengea mchepuko. Ili siku moja aje amfanyie surprise. Lkn kabla ya surprise jamaa akapata ugonjwa ama ajali na kufariki. Kwahiyo si mchepuko wala familia waijuao nyumba hii.

2. Mmiliki alipoikamilisha alipigwa kifungo cha miaka 30 au zaidi jela.

Je, nijitwale hii nyumba? Vipi kama nadharia ya 2 ndiyo sahihi? Akitoka jela na kurudi uraiani itakuwaje? Ingawa kuna usemi wa kiswahili unanipa moyo "cha kuokota siyo cha kuiba, mwenye mali mpumbavu".
Unaweza kuichukua,lkn ukajikuta kwenye matatizo makubwa.Ukute nyumba hiyo ina Mazingaombwe mengi yaani full vibwengo na mauzauza.

Sent from my V1901A using JamiiForums mobile app
 
Nyumba za namna hiyo zipo nyingi mno hasa jijini Dar es salaam.

Mahali ninapoishi,kuna nyumba zimejengwa kwa mfuatano zikiwa 3,inasemekana Mzee anao watoto 3 aliamua kuwajengea hizo nyumba,mzee alifariki ila madogo wapo wanaishi nje ya nchi!

Walikuja kipindi fulani( Zaidi ya mika 10 iliyopita) wakaangalia zile nyumba na mahali zilipo wakasema hawazihitaji!.

Kuna Sheikh mmoja ameamua kujimegea moja anaishi na familia yake,zile nyingine 2 zinazidi kuota nyasi tu na nyoka kujazana huko ndani!.

Nyumba ni nzuri na naza kisasa mno!,lakini madogo walisema hawawezi kuja kuishi Tanzania.

Sasa wenyeji kila mmoja anaogopa na kusema wanaweza kushitakiwa,lakini ukweli ni kwamba hakuna mtu wa kukushitaki wala nini!.

Ngoja nivute muda,mwakani nasafisha moja naingia,mdogo mdogo hadi inakuwa yangu!

Maana kwa dalili zilizopo hakuna wa kuhoji zaidi ya kuendelea kuchakaa!,Siku watu wa Ardhi wakishituka zitakwenda na maji!.

Mwakani najimilikisha moja!
 
Mwaka 2009 tulienda na rafiki yangu Bunju kununua Viwanja,tukaanza kujenga mdogomdogo lakini rafiki yangu (RIP)alijenga fasta ikabaki kupaua tu(kumbuka wote tulikuwa mabachela). Siku moja anatoka site akapata ajali Tegeta(aligongana na Lori),alifariki palepale. Huyu rafiki yangu tulikuwa tumepanga nyumba moja Sinza(yeye Chumba chake,mimi changu lakini sebule,jiko nk tunashea. Tangu tunanunua Viwanja mpaka anafariki hakuna aliyewahi kumpeleka site ndugu,rafiki wala jamaa. Hivyo nyumba niliiokota kwa style hiyo,niliipaua,nikaifanyia finishing na sasa nakula Kodi. Lakini kwa kuwa tulikuwa tumeshibana sana hivyo huwa najitajidi kuwatumia Pesa Wazazi wake Moshi kila mwezi,na wamekuwa kama Wazazi wangu na wananiita mwanao.
SWALI KWA NINI SIKUIPA TAARIFA FAMILIA HIYO?huyu Marehemu rafiki yangu ndie aliyekuwa amesoma kwao,Kaka na Dada zake wote ni wale waleviwalevi waliojichokea tu,hivyo kama ningetoa taarifa naamini wangeshauri nyumba iuzwe tu wapate Pesa ya kunywea pombe. Tangu niikamilishe mwaka 2011 mpaka leo nakula Kodi tu,Hati nilishaipata kwa jina langu na maisha yanasonga.
Mimi ubavuni kwangu kuna viwanja 2 double sijui vya mtu mmoja au la.
Tangu 2020 nianze kuja huku mara kwa mara na 2021 nilipohamia sijamwona mwenyewe.
Nalima mbogamboga na mihogo.
Nawaza sijui nipige ukuta kote au nitulie kwanza.
Wanadamu tuache ubinafsi, mali zako mtu hutaki hata kumeonyesha mke ukifa je!
 
Safi. Kuitwaa nyumba siyo lazima ufanye vitu vikubwa sana.

Unaweza ukuwa unaenda kuwasha taa na kuzima, kama umeme upo

Mwagilia maua

Panda miti

Kaa kibarazani😀

Fungua na kufunga milango

Washa moto upike

Fanya vikao vya familia

Lima majani huko nje

Panda ukoka

Safisha dari ondoa bui bui

Nenda msalani

Fukuza watoto wanaocheza kibarazani

Fanya jambo lolote ambalo litakupa hadhi ya umiliki.
 
Mkuu haya yote nitayafanya,Ahsante kwa mbinu 🤣
 
Mimi ubavuni kwangu kuna viwanja 2 double sijui vya mtu mmoja au la.
Tangu 2020 nianze kuja huku mara kwa mara na 2021 nilipohamia sijamwona mwenyewe.
Nalima mbogamboga na mihogo.
Nawaza sijui nipige ukuta kote au nitulie kwanza.
Wanadamu tuache ubinafsi, mali zako mtu hutaki hata kumeonyesha mke ukifa je!
Dadeki🙆

Ndiyo maana nikinunua kiwanja au shamba, kama sina hela ya kujenga nitachimba mashimo, au ninakilima nusu, kama kuna miti ninapruni.

Nikishindwa yote hayo ninaenda hapo ninakaa nakula muwa naacha maganda.

Yote hayo ni kuonyesha uhai kwamba hili eneo lina mwenyewe na huenda alitoka hapa siku 1 au 2 zilizopita.
 
Mwaka 2009 tulienda na rafiki yangu Bunju kununua Viwanja,tukaanza kujenga mdogomdogo lakini rafiki yangu (RIP)alijenga fasta ikabaki kupaua tu(kumbuka wote tulikuwa mabachela). Siku moja anatoka site akapata ajali Tegeta(aligongana na Lori),alifariki palepale. Huyu rafiki yangu tulikuwa tumepanga nyumba moja Sinza(yeye Chumba chake,mimi changu lakini sebule,jiko nk tunashea. Tangu tunanunua Viwanja mpaka anafariki hakuna aliyewahi kumpeleka site ndugu,rafiki wala jamaa. Hivyo nyumba niliiokota kwa style hiyo,niliipaua,nikaifanyia finishing na sasa nakula Kodi. Lakini kwa kuwa tulikuwa tumeshibana sana hivyo huwa najitajidi kuwatumia Pesa Wazazi wake Moshi kila mwezi,na wamekuwa kama Wazazi wangu na wananiita mwanao.
SWALI KWA NINI SIKUIPA TAARIFA FAMILIA HIYO?huyu Marehemu rafiki yangu ndie aliyekuwa amesoma kwao,Kaka na Dada zake wote ni wale waleviwalevi waliojichokea tu,hivyo kama ningetoa taarifa naamini wangeshauri nyumba iuzwe tu wapate Pesa ya kunywea pombe. Tangu niikamilishe mwaka 2011 mpaka leo nakula Kodi tu,Hati nilishaipata kwa jina langu na maisha yanasonga.
Kisheria hii inatwa 'bad means for good motive'.

Umezulumu kwa malengo mema.

Sasa je, umezulumu kweli? Na je lengo lako ni jema?

Majibu hapo yanategemeana na mawazo yako na ya mtu anayepata huu mkasa.

Vipi, rafiki yako alikuwa anaendesha boda au gari? Kwa sababu hujasema aligongana na lori akiwa na usafiri gani
 
Kuna nadharia mbili hapa.

1. Yawezekana mmiliki alikuwa anamjengea mchepuko. Ili siku moja aje amfanyie surprise. Lkn kabla ya surprise jamaa akapata ugonjwa ama ajali na kufariki. Kwahiyo si mchepuko wala familia waijuao nyumba hii.

2. Mmiliki alipoikamilisha alipigwa kifungo cha miaka 30 au zaidi jela.

Je, nijitwale hii nyumba? Vipi kama nadharia ya 2 ndiyo sahihi? Akitoka jela na kurudi uraiani itakuwaje? Ingawa kuna usemi wa kiswahili unanipa moyo "cha kuokota siyo cha kuiba, mwenye mali mpumbavu".
Inategemea na Nyumba iko wapi..
Kama Nyumba iko Sumbawanga,Tanga,Zanzibar,Pemba,Shinyanga....
Mkuu Iogope kama Ukoma!

Ila kama iko Dodoma ,Singida, Morogoro ,Arusha mzee we ingia safisha Kabisa iyo mali yako...

Ila hiyo mikoa nilokukataza unaweza geuka Chakula cha Majini au Misukule..

Usiseme hukuambiwa
 
Back
Top Bottom