Mwaka 2009 tulienda na rafiki yangu Bunju kununua Viwanja,tukaanza kujenga mdogomdogo lakini rafiki yangu (RIP)alijenga fasta ikabaki kupaua tu(kumbuka wote tulikuwa mabachela). Siku moja anatoka site akapata ajali Tegeta(aligongana na Lori),alifariki palepale. Huyu rafiki yangu tulikuwa tumepanga nyumba moja Sinza(yeye Chumba chake,mimi changu lakini sebule,jiko nk tunashea. Tangu tunanunua Viwanja mpaka anafariki hakuna aliyewahi kumpeleka site ndugu,rafiki wala jamaa. Hivyo nyumba niliiokota kwa style hiyo,niliipaua,nikaifanyia finishing na sasa nakula Kodi. Lakini kwa kuwa tulikuwa tumeshibana sana hivyo huwa najitajidi kuwatumia Pesa Wazazi wake Moshi kila mwezi,na wamekuwa kama Wazazi wangu na wananiita mwanao.
SWALI KWA NINI SIKUIPA TAARIFA FAMILIA HIYO?huyu Marehemu rafiki yangu ndie aliyekuwa amesoma kwao,Kaka na Dada zake wote ni wale waleviwalevi waliojichokea tu,hivyo kama ningetoa taarifa naamini wangeshauri nyumba iuzwe tu wapate Pesa ya kunywea pombe. Tangu niikamilishe mwaka 2011 mpaka leo nakula Kodi tu,Hati nilishaipata kwa jina langu na maisha yanasonga.