Hapa jirani yangu pana nyumba haijawahi kukaliwa na watu tokea ikamilike kujengwa. Ni mwaka wa 10 huu, mpaka geti linaanza kuoza. Nijitwalie?


😄😄, pole sana SELEMAN, nakushauri kazana kutafuta hela.
 
Acha ufala pangisha hiyo nyumba
 
Kwa nyumba sijui ipoje ila kwa kiwanja afadhali
Mi nilijipatia kiwanja kwa namna hiyo
Kilikuwa ubavuni kwangu na mwenyewe hakuwahi kuonekana
Nikaenda ardhi nikawaeleza wakaniambia kasafishe kwanza ukiona kimya weka msingi tulia

Nilifanya hivyo na hakutokea mtu lakini palikuwa ma tofali 12 pale chini
Baada ya mwaka nikaenda ardhi nikawaeleza wakanipa offer/hati na hadi leo napamiliki
 
We ni mwizi
 
kuna ndugu yangu alikiwa mfanyabiashara mkubwa wa mazao, kuna mkoa alienda katika shughuli zake sehemu ya faida alinunua kiwanja ambacho kilikuwa na msingi teyari.

Kwa bahati mbaya makabidhiano ya nyaraka muhimu hayakukamilika ila kwakuwa alikuwa na uhakika akawa amefuata mzigo mwingine.

Aliporudi mkoai ilipo familia yake akawapa hiyo taarifa kuwa kuna kiwanja kanunua mkoa fulani wilaya flani na jinsi kilivyo,

Wakati anajipanga ili kupeleka mzigo tena kwenye ule mkoa akapatwa na maradhi na hayakumchukua siku nyingi akawa amefariki na story ya hicho kiwanja ikaisha kwa namna hiyo.
 
Mkuu unajaribu kumshauri nini mdau😅😅
 
Acha wizi mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…