LEMA AWAPIGA MASWALI MAZITO WAJUMBE WA MKUTANO MKUU CHADEMA SAKATA LA RUSHWAMbowe kasema uchaguzi utakuwa live TV zote za duniani zinazotaka kuja zitaingia ukumbi wa uchaguzi
1. Wajumbe kuhakikiwa live
2. Kura kupigwa live
3. Matokeo kuhesabiwa live
4. Mshindi kutangazwa live
5. Mshindi kuhutubia live
6. Mshindwa kuhutubia live
Haya yote watashudia wanachama wa chadema wakiwa majumbani mwao.
TLS kupitia mwambukusi ataalikwa.
Mdude ataona live
Madeleka ataoana
Lissu alitegemea hayo mambo yatafanywa ukumbini bila nje ya ukumbi yaani dunia kushuhudia ili maria space, Dr slaa, na baadhi ya wanaoishi nje wawahadae wanachadema kwamba lissu kaibiwa kura ili apate support.
Lissu hataibiiwa kura 1, lkn asubiri kimbunga cha kumkataa kutoka wajumbe.
Kwanini wamkatae.
Akipewa chama atavuruga legacy ya kila kiongozi tofauti na Mbowe. Lini na wapi Mbowe kavuja legacy ya Mtei, Bob makani na wengine anapotoa hutuba zake?
Lssu kabla hajapata, anaitetea legacy pekee ya msigwa lkn zote anaonesha atazivuruga. Mbowe anamwita fisadi na hata Bob makani na mtei inaonekana atawasakama jambo litaivuruga kabisa chadema na kufurahisha cloud house
Kilichobaki lissu atakuja na hoja ya kwamba wapiga kura wamehongwa huko huko kabla ya ukumbini pesa za Abdullah jambo litakuwa halina nguvu mtu mwenye akili kuamini hilo. Na akiamua kuondoka ataondoka na team manager wake, akibaki chadema awe mwenyekiti wa Tawi lake anapoishi
Lissu hakubaliki kuwa mwenyekiti Chadema
Godbless Lema, Mwenyekiti Mstaafu wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini atoa ujumbe mzito kwenda kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CHADEMA kuhusu sakata la rushwa katika uchaguzi wa chama hicho taifa utakaofanyika Januari 21, 2025.
"Swali moja la msingi kwa WAJUMBE wa CHADEMA ni hili , ikiwa utapewa pesa, usafiri, pombe na chakula wkt huu lakini ukuletewa pesa wakati wa uchaguzi wa serikali za Mitaa, Kijiji na Vitongoji, je hizo pesa sasa zinatoka wapi? Na wanaotoa pesa wananunua kura kwa sababu gani kwa kazi isiyo hata na mshahara ? CHADEMA sio duka wala Bar . Wajumbe sikilizeni , hiki CHAMA kina damu za rafiki zenu , maumivu makubwa na mateso kwa watu wengi, msilaani maisha yenu kwa starehe na rushwa. Sasa basi wakileta pesa kula , kunywa halafu waadhibu ktk boksi la kura. Nyie sio Blue Band wakubebwa kama Maboksi. Upinzani ni tabia njema na sio rangi za nguo. Msiue matumaini ya Taifa kwa kushindwa kutofautisha tabia zetu na @ccm_tanzania" - Godbless Lema, Aliyekuwa Mwenyekiti wa @ChademaTz wa Kanda ya Kaskazini.