Hapa ndio ninapokuwa na walakini na uwepo wa Mungu

Hapa ndio ninapokuwa na walakini na uwepo wa Mungu

Mungu yupo
Huyo Mungu kama yupo, Yupo wapi?

Huyo Mungu kama yupo, Kwa nini anataka kuaminiwa yupo akiwa mafichoni, Badala ya kujitokeza hadharani akajulikana yupo kwa uhakika kabisa?

Hivi huyo Mungu anajielewa kweli?
Na hapendi kudhihakiwa.
Huyo Mungu kama hapendi kudhihakiwa, Kwa nini aliumba binadamu wenye uwezo wa kumdhihaki?

Huyo Mungu kama hapendi kudhihakiwa, Alishindwaje kuumba binadamu wema tu watakao mtii na kumwamini siku zote?
 
Wachungaji mje mnisaidie Jamani mimi nashindwa kujibu
 
tayari umeshafanya ibada.. umevumilia yote umekua na subira. muamini MUNGU usikate tamaa subira ni ibada na amini wakati unaona kila kitu kimefail ndio MUNGU hujidhihirisha. usiache kumwamini
miracles happen every day
 
Kasome kitabu cha Ayubu kina unabii mkubwa sana pale..lakini pia wakati una nafasi ya kuandika haya ukiwa na simu janja yenye network, bundle na chaji wakumbuke pia
Waliojibanza vibarazani wasio na makazi
Wagonjwa mahospitalini
Wafungwa magerezani
Nknk
Waliojibanza vibarazani wasio na makazi, wagonjwa mahospitali na wafungwa gerezani ni uthibitisho tosha kwamba Mungu hayupo.

Mungu huyo angekuwepo, Angesha wasaidia watu hawa waondokane na mateso yao.

Lakini Holaaaa!! Mungu huyo anayedaiwa yupo, Kashindwa kuwasaidia wagonjwa mahospitali, wafungwa gerezani na homeless wasio na makazi kwa miaka mingi sana.
 
Hakuna Mungu ni wazo lililotengenezwa na Wanadamu tu.

Kwenye ule mgogoro wa kule Palestina, walikufa wapalestina 46,000 ikiwemo watoto, wazee, wagane, wajane na watu wengine, msaada wake mliuona?

Vita ya Kongo hapo, zaidi ya miaka 40 watu wanauwawa, wamesaidiwa na nini?

Kinachoendelea hapo Sudan, kinafahamoka, kule Myanmar hasa kwenye Jimbo la Rohingya.

Tazama magonjwa na shida halafu matokeo yake ikawaje?
Kuna uhusiano gani wa kuwepo Mungu na hayo unayoyasema? Kwamba uwepo wa Mungu unategemea na yeye kutoa msaada?

Hebu nieleweshe.
 
Mungu anaadhibu watu wake ikiwa chanzo kikuu ni yeye.

Infact Mungu ni mjuzi wa Yote.

Hivyo alimuumba shetani huku akijua kwamba kuna watu watakwenda kuteseka.

Mateso haya yote duniani, Chanzo chake ni Mungu mjuzi wa yote ajuaye Mwisho kabla ya mwanzo maana haya yote alishayajua kabla.
Kwahiyo kama aliyajua ndio anayatenda yeye? Hebu nieleweshe.
 
Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hatakaa awepo.

The fact that an almighty God and all powerful God needs humans to speak for him and defend him, It's a prove that he doesn't exist.

Huyo Mungu kama yupo ajitokeze hadharani mwenyewe ajidhihirishe na kujitetea mwenyewe, Kama ana huo uwezo.
Kwanini afanye hivyo kwa uhitaji gani ambao utamlazimu afanye hivyo? Hebu nieleweshe.
 
Kuna Mungu.

Wapumbavu husema moyoni mwao Kuna Mungu.

Maana wamepumbazwa kuamini vitu bila uthibitisho.
Hata wewe umepumbazwa mkuu, kitendo cha wewe kukubali kuwa atheist unalazimika kufuata mambo kwa kuwa tu ni atheist hivyo lazima uyakubali tu ili kuendanda na definition ya atheism.
 
Waliojibanza vibarazani wasio na makazi, wagonjwa mahospitali na wafungwa gerezani ni uthibitisho tosha kwamba Mungu hayupo.

Mungu huyo angekuwepo, Angesha wasaidia watu hawa waondokane na mateso yao.

Lakini Holaaaa!! Mungu huyo anayedaiwa yupo, Kashindwa kuwasaidia wagonjwa mahospitali, wafungwa gerezani na homeless wasio na makazi kwa miaka mingi sana.
Nipe ushahidi wa Mungu kushindwa kuwasaidia?
 
Kwahiyo kama aliyajua ndio anayatenda yeye? Hebu nieleweshe.
Mungu wa kwenye biblia ndiyo kaelezwa hivyo, Sasa wewe unataka nikueleweshe nini?

Au Mungu ni mjuzi wa yote lakini hawezi kujua na kuizuia mipango ya Shetani ambaye inasemekana ndiyo chanzo cha kuteseka?
 
Yuko Mbinguni, Chanzo chake hakijulikani
Umewahi kufika huko mbinguni ukamuona au unauthibitisho upi kwamba yupo mbinguni?

Kama unakubaliana na wazo kwamba chanzo chake hakijulikani ila yeye yupo yaani ni kama Ali appear from nowhere.

Je, Unashindwaje kuamini pia huenda ulimwengu mzima na kila kitu duniani navyo havina chanzo na vili-appear from nowhere?
 
Nipe ushahidi wa Mungu kushindwa kuwasaidia?
Ushahidi gani unataka na mateso yao unayaona?

Kuteseka kwao ni uthibitisho tosha kwamba Mungu Kashindwa kuwasaidia.

Huyo Mungu angekuwa anasaidia, Kusingekuwa na watu wanao teseka. Duniani.
 
Hata wewe umepumbazwa mkuu, kitendo cha wewe kukubali kuwa atheist unalazimika kufuata mambo kwa kuwa tu ni atheist hivyo lazima uyakubali tu ili kuendanda na definition ya atheism.
Atheist ni mtu asiyekuwa na imani ya aina yeyote ile.

Hata wewe ulizaliwa "Atheist" Hukuwa na imani ya aina yeyote ile wakati umezaliwa.

Mpaka pale wazazi wako au walezi wako walipo kuaminisha kwenye imani na dini.

Hivyo wazazi wako ndio wamekupumbaza kwa kukuaminisha kwenye imani na dini za kuletwa tangu ukiwa mdogo.

Once you are born you are given a name, a nationality, a religion and faith. You spend the rest of your life defining and defending fictional identities.

Mara tu ulipozaliwa ulipewa jina, uraia, dini na imani. Unatumia muda wako wote wa maisha kutetea na kuelezea dhana za kufikirika tu.

Una elewa hilo?
 
Kwanini afanye hivyo kwa uhitaji gani ambao utamlazimu afanye hivyo? Hebu nieleweshe.
Sasa kama huyo Mungu yupo na anataka kuaminiwa yupo, Kwa nini anajificha?

Kwa nini asijitokeze hadharani akajulikana yupo kwa uhakika kabisa pasipo utata na utofauti wa kiimani?
 
Habari za siku ya leo Wanajamiiforums?

Kama kichwa cha habari kilivyojitosheleza. Sababu zinazonifanya niwe na mashaka na uwepo wa Mungu ni hizi hapa.

Sina dhambi mi ni mtakatifu haswa,
Lakini nimepitia mambo mazito mno ambayo mtu yeyote lazima angekuwa na mashaka na uwepo wa Mungu.

Sio kwamba simuamini Mungu kwa asilimia mia, Bali nina mashaka na uwepo wake (Nipo DILEMMA).

Ni hayo tu
Tukisema hatuna dhambi twajidanganya wenyewe..

Kimsingi Muumba yupo,just take time to think deep.

Ila sio muumba wa kwenye vitabu hasa kile cha pedophile
 
Mungu wa kwenye biblia ndiyo kaelezwa hivyo, Sasa wewe unataka nikueleweshe nini?

Au Mungu ni mjuzi wa yote lakini hawezi kujua na kuizuia mipango ya Shetani ambaye inasemekana ndiyo chanzo cha kuteseka.
Hata kama ni mipango ya shetani ila watendaji ni binaadamu wenyewe, shetani hamforce mtu kufanya kitu.
 
Sasa kama huyo Mungu yupo na anataka kuaminiwa yupo, Kwa nini anajificha?

Kwa nini asijitokeze hadharani akajulikana yupo kwa uhakika kabisa pasipo utata na utofauti wa kiimani?
Sasa akijitokeza hadharani na kila mtu akajua uwepo wake bila utata je hapo itakuwa suala la kuamini tena? Hebu nieleweshe.
 
Habari za siku ya leo Wanajamiiforums?

Kama kichwa cha habari kilivyojitosheleza. Sababu zinazonifanya niwe na mashaka na uwepo wa Mungu ni hizi hapa.

Sina dhambi mi ni mtakatifu haswa,
Lakini nimepitia mambo mazito mno ambayo mtu yeyote lazima angekuwa na mashaka na uwepo wa Mungu.

Sio kwamba simuamini Mungu kwa asilimia mia, Bali nina mashaka na uwepo wake (Nipo DILEMMA).

Ni hayo

Aseee
 
Back
Top Bottom