Hapa ndio ninapokuwa na walakini na uwepo wa Mungu

Kama ni hivyo mbona hatuoni duniani dini kuzuiliwa kwa sababu zinaeneza mafundisho yao ya imani waziwazi kwa watu ambao unasema ni kusambaza uongo? Hebu elezea nielewe.
Dini ni uhuru wako wa kikatiba.

Lakini kupewa uhuru wa kikatiba kuamini kwenye dini, sio kigezo cha kufanya imani za kidini ziwe za ukweli.
Huko kumfosi mtu kukubali imani ndio kunafanyikaje hebu toa mifano wewe ushawahi kufosiwa kukubali imani bila kinyume na ridhaa yake au umeona humu JF watu wakifosiwa kukubali imani fulani?
Nyuzi za kumkiri na kumwamini Yesu ni nyingi sana hapa JF. Wakristo wanapiga kampeni za huyo Yesu akubalike na kila mtu.

Nyuzi za kusilimu na kumwamini Allah ni nyingi sana hapa JF . Waislamu wamekuwa wakipiga kampeni Allah wao na mtume Muhammad akubalike na kila mtu.
Imani ya aina yeyote ile ni kutokuwa na uhakika wala uthibitisho.

Ukishakuwa na uhakika na uthibitisho juu ya jambo fulani, Hiyo sio imani tena.
 
Lete

Lete ushahidi usio na shaka kuhusu uwepo wake.

Kwa hiyo akiamini nyonzo ndio shonvi naye autambue kuwa ukweli?

Ukweli hakuna Mungu hapa duniani.
Ukweli hauwi ukweli kwa sababu wewe umesema tu ni ukweli, nimekutolea mifano kuonyesha huko kusema hakuna Mungu huo ni mtazamo wako tu na wengine nao wana mitazamo yao tofauti, sasa wewe umekazana kusema kutokuwepo kwa Mungu ndio ukweli halafu hauna cha kushawishi watu wakubali kuwa huo ndio ukweli na si mtazamo tu wa baadhi ya watu ambapo umezaliwa umeukuta.

Kama kutokuwepo ushahidi usio na shaka wa uwepo wa Mungu ndio inatoa tafsiri ya moja kwa moja kuwa hakuna Mungu basi hata Agnostics nao wangesema wazi hakuna Mungu kama usemavyo wewe, ila kwa kuwa kukosekana ushahidi hakutoi tafsiri ya moja kwa moja kuwa hakuna Mungu basi ndio maana Agnostics hawadai hakuna Mungu kama unavyodai wewe.

Ambacho wewe huelewi ni kwamba unaposema kwa uhakika kabisa kuwa Mungu hakuna inakuwa umetoa madai, sasa hauwezi tena kusema mimi nithibitishe ili kupinga unachokidai wewe. Unachokidai wewe kithibitishe mwenyewe.
 
Kama ni hivyo basi usingekuwa unajiingiza kwenye mabishano ya kuhusu Mungu,
Huwezi kuniambia kwamba nisijiingize kwenye mabishano kuhusu Mungu, Wakati habari za uwepo wa Mungu zinaletwa hapa JF kwenye public forum ambako pia kuna sisi tusio amini Mungu.

Ukileta imani yako hapa kwenye public forum JF kuhusu uwepo wa Mungu na wakati huohuo unajua kwamba kuna wasio mwamini Mungu, Basi unakuwa umeiweka hiyo imani yako kikaangoni.

Inaweza kufanywa vyovyote na yeyote.

Ukitaka imani yako ya Mungu isiguswe na yeyote, Baki nayo hukohuko moyoni mwako au kwenye nyumba zenu za ibada.

Lakini mkileta hizo imani na dini zenu hapa JF kuhusu Mungu, Tutazikosoa na kuzichambua.
 
Sasa mbona hatuoni dini kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kusambaza uongo kwenye jamii?

Sasa watu kuweka nyuzi za mambo ya imani ndio kumfosi mtu mwengine kuamini jambo bila ridhaa ambapo ni kinyume na sheria?

Ndio maana nasema wewe unapinga imani.
 
Ni Mungu gani anaemtoa mwanae kafara? Hiyo kitu ilitungwa na wayahudi na ikaenea karibu dunia nzima. Walitumia uchawi gani? Eti Mungu kagawanyika sehemu tatu, huo sio uhuni?
 
Sasa kama ni hivyo basi usiseme hautaki watu wamtetee Mungu na kutaka Mungu ajitete mwenyewe, unaingia kwenye majadiliano ya watu kuhusu Mungu halafu unataka hao watu wasijadili wao kuhusu Mungu unataka ajitokeze Mungu mwenyewe hiyo ni akili ya wapi?

Yani wewe unakuta watu wanajadili tuhuma ya Rais Samia iliyoandikwa kwenye kutabu kuwa alikoswa kubakwa halafu unawaambia hao watu waache kujadili na kutaka ajitokeze Samia mwenyewe.
 
Sasa mbona hatuoni dini kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kusambaza uongo kwenye jamii?
Nimekwambia dini ni uhuru wa mtu kikatiba.

Una uhuru wa kuamini chochote utakacho, Haijalishi ni ukweli au Uongo.

Hata ukiamua kuamini mawe, miti, mapango, milima n.k
Sasa watu kuweka nyuzi za mambo ya imani ndio kumfosi mtu mwengine kuamini jambo bila ridhaa ambapo ni kinyume na sheria?
Ukianza kuhubiria watu kwamba imani yako ni bora sana kuliko ya kwake.

Hapo unaanza kufosi imani yako ionekane bora kuliko ya kwake.
Ndio maana nasema wewe unapinga imani.
Ndio napinga Imani.

Ila naheshimu wenye hizo imani.
 
Na wewe kwa nini unataka nisijadili hivi ninavyo jadili?

Kila mtu ana uhuru wa kujadili atakavyo.

Sasa wewe unataka mimi nijadili jinsi wewe unavyo fikiri, Badala ya jinsi mimi mwenyewe ninavyo fikiri?

Na wewe hii ni akili ya wapi?
Yani wewe unakuta watu wanajadili tuhuma ya Rais Samia iliyoandikwa kwenye kutabu kuwa alikoswa kubakwa halafu unawaambia hao watu waache kujadili na kutaka ajitokeze Samia mwenyewe.
Vipi kama hicho kitabu ni uongo?

Tutahakikisha vipi hicho kilicho andikwa kwenye kitabu kumhusu Rais samia ni ukweli?
 
Sasa kama dini ni uhuru na ni ruksa kusambaza imani bila kujali ni ukweli au uongo sasa shida yako wewe hapo ni ipi? Watu wanatumia uhuru wao hata wewe unao uhuru wa kudai Mungu hakuna huvunji sheria.

Kama unaheshimu wenye hizo imani mbona unapinga wasitangaze imani zao?
 
Sio mimi nakukataza kujadili bali wewe ndio hautaki watu kujadili kuhusu Mungu, unataka Mungu mwenyewe ajitokeze hautaki watu kumtetea.
 
Wapi nimepinga wasitangaze imani zao?

Mimi napingana na imani zao wanazo zitangaza.

Sipingani na wao kutangaza imani zao.

Ndio maana hakuna anaye kuzuia kuanzisha uzi hapa JF kuhusu imani yako.

Lakini ukianzisha uzi hapa JF kutangaza imani yako, Tutapinga hiyo imani yako kwa hoja.

Hatupingi watu kutangaza imani zao, Tunapinga hizo imani zinazo tangazwa.

Una elewa?
 
Sio mimi nakukataza kujadili bali wewe ndio hautaki watu kujadili kuhusu Mungu, unataka Mungu mwenyewe ajitokeze hautaki watu kumtetea.
Mimi sitaki watu wasijadili kuhusu Mungu.

Kujadili ni uhuru wako wa kikatiba.

Mimi napingana na hizo imani kumhusu huyo Mungu anayejadiliwa.
 
Hayo nduo yanatia mashaka ya huyu mwenye upendo na uwezo wote
 
🤣🤣 problem of Evil..
Mungu Yupo Sema Tunatakiwa Kuchunguza zaidi Kumjua
 
Mtu kutangaza imani yake unaita ni kuforce na kwamba ni kosa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…