Hapa ndio ninapokuwa na walakini na uwepo wa Mungu

Hapa ndio ninapokuwa na walakini na uwepo wa Mungu

Mimi sitaki watu wasijadili kuhusu Mungu.

Kujadili ni uhuru wako wa kikatiba.

Mimi napingana na hizo imani kumhusu huyo Mungu anayejadiliwa.
Si ndio unasema ajitokeze na kujitetea mwenyewe hutaki watu wamtetee na kumuelezea badala yake.
 
Hayo matatizo umepitia ilikua kwaajili ya wewe kumjua Mungu na uwepo wa Mungu ,vinginevyo bila hayo matatizo usingeweza kuwa na imani kuhusu Mungu
 
Mungu/miungu haijawahi kuzungumza na binadamu yoyote, kwa kuwa ni dhana tu.
Binadamu kadhaa wakaja kuwaambia wenzao kwamba mungu kaongea nao.
Wakatunga sifa, masharti na ahadi hewa toka kwa Mungu na wakasambaza uzushi wao.
Wakiulizwa wanathibitishaje kuwa na mawasiliano na Mungu, hawana majibu. Wanadai nyie aminini tu. Imani haihitaji uthibitisho. Leo hii watu wanaamini tu. Je, huu si ukichaa?
 
Si ndio unasema ajitokeze na kujitetea mwenyewe hutaki watu wamtetee na kumuelezea badala yake.
Ndio aje yeye mwenyewe kama ana huo uwezo.

Hizi mnazopiga hapa ni blah blah tu. Kujitahidi kumuelezea.
 
Sasa kama ni hivyo basi usiseme hautaki watu wamtetee Mungu na kutaka Mungu ajitete mwenyewe, unaingia kwenye majadiliano ya watu kuhusu Mungu halafu unataka hao watu wasijadili wao kuhusu Mungu unataka ajitokeze Mungu mwenyewe hiyo ni akili ya wapi?

Yani wewe unakuta watu wanajadili tuhuma ya Rais Samia iliyoandikwa kwenye kutabu kuwa alikoswa kubakwa halafu unawaambia hao watu waache kujadili na kutaka ajitokeze Samia mwenyewe.
Huwezi kunipangia namna ya kujadili.

Wewe unataka mimi nijadili jinsi wewe unavyo fikiri, Badala ya jinsi mimi mwenyewe ninavyo fikiri.

Na hii ni akili ya wapi?
 
Habari za siku ya leo WanaJamiiForums?

Kama kichwa cha habari kilivyojitosheleza. Sababu zinazonifanya niwe na mashaka na uwepo wa Mungu ni hizi hapa.

Sina dhambi mi ni mtakatifu haswa,
Lakini nimepitia mambo mazito mno ambayo mtu yeyote lazima angekuwa na mashaka na uwepo wa Mungu.

Sio kwamba simuamini Mungu kwa asilimia mia, Bali nina mashaka na uwepo wake (Nipo DILEMMA).

Ni hayo tu
Mitume na Watakatifu ndio walipata majaribu makubwa
Mungu humpa mtu jaribu kulingana na ukubwa wa Imani yake...Kasome Biblia/Quran yako tena....
 
Kuna Mungu.

Wapumbavu husema moyoni mwao Kuna Mungu.

Maana wamepumbazwa kuamini vitu bila uthibitisho.

Stop twisting em words...

Zaburi 53
1 Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wametenda uovu wa ufisadi na kuchukiza, Hakuna atendaye mema.
 
Mitume na Watakatifu ndio walipata majaribu makubwa
Mungu humpa mtu jaribu kulingana na ukubwa wa Imani yake...Kasome Biblia/Quran yako tena....
Mungu mwenye kujua yote tangu mwanzo na hata milele, Anakupa majaribu ili apime nini au ili agundue nini?

Kwani yeye hajui matokeo mpaka akupe majaribu?
 
Stop twisting em words...

Zaburi 53
1 Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wametenda uovu wa ufisadi na kuchukiza, Hakuna atendaye mema.
Huyo Mungu, Kwa nini aliumba binadamu wapumbavu wenye uwezo wa kusema yeye hayupo?

Huyo Mungu, Alishindwaje kuumba binadamu wema tu watakao mtii na kusema yeye yupo siku zote na wakati wote?

Huyo Mungu anayetukana watu wake mwenyewe, Pia na yeye ni Mpumbavu sana.

Huyo Mungu hajielewi kabisa.
 
Huyo Mungu anayetukana watu wake mwenyewe pia na yeye ni Mpumbavu sana.

Inawezekana hujui tafsiri ya neno "pumbavu" ndio maana waliita ni tusi, kwa mujibu wa kamusi ya Kiswahili sanifu.

pumbavu:
-sioweza kutumia akili vizuri, sioelewa jambo
, hiki ni kivumishi cha sifa.

Mwanadamu umeumbwa na akili lakini hutaki kuitumia vizuri, wala kutaka kuelewa mambo.
 
Habari za siku ya leo WanaJamiiForums?

Kama kichwa cha habari kilivyojitosheleza. Sababu zinazonifanya niwe na mashaka na uwepo wa Mungu ni hizi hapa.

Sina dhambi mi ni mtakatifu haswa,
Lakini nimepitia mambo mazito mno ambayo mtu yeyote lazima angekuwa na mashaka na uwepo wa Mungu.

Sio kwamba simuamini Mungu kwa asilimia mia, Bali nina mashaka na uwepo wake (Nipo DILEMMA).

Ni hayo tu
Mambo gani hayo uliyopitia
 
Huyo Mungu kwa nini aumbe watu wasioweza kutumia akili zao vizuri?

Huyo Mungu kwa nini aumbe watu wasiotaka kuelewa mambo?

Huyo Mungu, Alishindwaje kuumba binadamu waelewa watakao elewa mambo siku zote na wakati wote?

Huyo Mungu, Alishindwaje kuumba binadamu watakao tumia akili zao vizuri siku zote na wakati wote?

Hivi huyo Mungu anajielewa kweli?
 
Habari za siku ya leo WanaJamiiForums?

Kama kichwa cha habari kilivyojitosheleza. Sababu zinazonifanya niwe na mashaka na uwepo wa Mungu ni hizi hapa.

Sina dhambi mi ni mtakatifu haswa,
Lakini nimepitia mambo mazito mno ambayo mtu yeyote lazima angekuwa na mashaka na uwepo wa Mungu.

Sio kwamba simuamini Mungu kwa asilimia mia, Bali nina mashaka na uwepo wake (Nipo DILEMMA).

Ni hayo tu
Huna dhambi? hicho kipimo cha kuonyesha kuwa huna dhambi ni kipi? mtakatifu mashaka ameyatoa wapi?
 
Dhambi kubwa uliyonayo ni hiyo ya kuamini huna dhambi
Sin is an imaginary disease invented by religion to sell you an imaginary cure.

It's like creating virus to sell Anti-Virus.

Dhambi ni dhana uchwara iliyotungwa na dini kukupa wewe hofu na kukuuzia baraka za kufikirika tu.

Hakuna dhambi.

Dhambi haipo.
 
Sijawahi kupata baraka ya aina yoyote kutoka kwa Mungu.
Ndugu yangu ni dhambi kubwa kumsema Mwenyezi Mungu kwa mambo ya uongo. Tafadhali omba msamaha kwa Mwenyezi Mungu na ufute hili bandiko lako linalomkashifu Mwenyezi Mungu.
Ukiwa na jambo unataka kufahamu kuhusu Mwenyezi Mungu basi soma vitabu vya dini acha kumuandika humu kwenye mitandao kwa mambo usiyoyafamu kuhusu Mwenyezi Mungu usije ukajikuta unalaanika.
Tumuheshimu Mwenyezi Mungu inavyo pasta kuheshimiwa.
 
Sijawahi kupata baraka ya aina yoyote kutoka kwa Mungu.
Pumzi tunayovuta kila siku iitwapo leo ni baraka na utajiri wa Afya kwenye maisha yetu.

Somanvzuri kitabu cha Ayubu mtumishi wa kweli wa Mungu aliyevutiwa naye hapa Duniani. Usipokielewa, rudi tena. Utaona wazi wazi uwepo wa Mungu ktk maisha yetu.
God is Good all the Time.
 
Kristo alikuja kwa ajili ya wenye dhambi na hivyo wakristo ni wadhambi.Niliyekwishatubu sina dhambi na hivyo sihitaji kusali maana mimi ni mtakatifu.
 
Back
Top Bottom