QURAN 3: 65-74
65. Enyi Watu wa Kitabu!(Wakristo na Wayahudi) Mbona mnabishana juu ya Ibrahim, na hali Taurati na Injili hazikuteremshwa ila baada yake? Basi hamzingatii?
66. Angalieni! Nyinyi mlibishana katika yale mliyo yajua. Mbona sasa mnabishana katika yale msiyo yajua? Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye, na nyinyi hamjui.
67. Ibrahim hakuwa Yahudi wala Mkristo, lakini alikuwa mwongofu Muislamu, wala hakuwa katika washirikina.
68. Watu wanao mkaribia zaidi Ibrahim ni wale walio mfuata yeye na Nabii huyu na walio amini. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wa Waumini.
69. Kipo kikundi katika Watu wa Kitabu (Wakristo na Wayahudi) wanao penda kukupotezeni; lakini hawapotezi ila nafsi zao, nao wenyewe hawatambui.
70. Enyi Watu wa Kitabu! (Wakristo na Wayahudi) Mbona mnazikataa Aya za Mwenyezi Mungu ilhali nyinyi mnashuhudia?
71. Enyi Watu wa Kitabu! Mbona kweli mnaivisha uwongo, na kweli mnaificha na hali mnajua?
71
72. Na kikundi katika Watu wa Kitabu walisema: Yaaminini yale waliyo teremshiwa Waislamu mwanzo wa mchana, na yakataeni mwisho wake; huenda wakarejea.
72
73. Wala msimuamini ila anaye fuata dini yenu. Sema: Hakika uwongofu ni uwongofu wa Mwenyezi Mungu, kuwa apewe mtu mfano wa mlio pewa nyinyi au wakuhojini mbele ya Mola wenu Mlezi. Sema: Hakika fadhila zimo mikononi mwa Mwenyezi Mungu. Humpa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa na Mjuzi.
73
74. Yeye humchagua kumpa rehema zake amtakaye; na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye fadhila kubwa.