Hapa ndipo inapotoka nguvu ya Kanisa Katoliki

Wana nguvu wawaongeze watumishi mishahara nguvu ya kupiga Domo hakumsamdii Yeyote porojo zao

Wana nguvu watoe huduma Bure pyepyeke pyeke ukienda kupata huduma kwao unalipia wafanya biashara kama wafanya biashara Wengine hawana tofauti na bakhresa au Dangote akitetea malori yake
Wewe hata huna ulijualo na bahati mbaya sana huwa sipendi mipasho hiyo ya 'pye pye pye' umeshindwa kujenga hoja yako.Ngoja nifanye umeshinda Boss,nilikuignore kwa kukuitikia 'sawa boss' lakini hukunielewa.Sasa naitikia tena kwa herufi kubwa SAWA BOSS UMESHINDA.
 
Tulia acha kutetea wafanya Biashara hakuna shule ya kiislam ya bure wala ya kikatoliki ya bure wote ukienda huduma zao utauziwa tuuuu wote wafanya biashara

Si hospital sio vyuo sio Shule
SAWA BOSS UMESHINDA
 
KUtoka vyanzo ndani ya ubaloz wa vatican tanzania
1.waarabu wakipewa bandari,agenda kubwa sio kuendeleza bandari bali kueneza uislam na waislam ndio watawale tanzania kwa miongo kadhaa
2.waarabu wakipewa bandari zote za majini na nchi kavu, basi wataingiza silaha kiholela na kuunda vikundi vya uasi na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe (watanzania )
3.waarabu wakipewa bandari,kuna mgogoro wa kimkakati utatokea bainabya visiwan na bara na hivyo visiwani wataamua kujitenga hasa ikizingatiwa upande wao hakuna bandari amepewa mwarabu.
4.mwarabu akipewa babandari si atafanya kaz zihusuzo bandari bali wataingilia mifumo mingine ya kitaasisi na kujinufaisha wao na mabwana zao waliowapa bandari....
5.mwarabu akipewa bandari kundi kubwa la vijana wa kitanzania watakosa ajira.
6.kwa kutukia mfano wa loliondo eneo analomiki mwarabu tangu miaka ya 90 na kupelekea vifo vya watu waliojaribu kupaza sauti kama hayati stan katabalo..vivyo hivyo wakipewa badari maisha ya watanzania yatakuwa duni mara mbili ya ilivyo sasa..
7.mwarabua akipewa bandari..mamlaka nyingi za ndan ya nchi zitapigwa marufuku kutekelez majukuku yao ndan ya maeneo aliyokabidhiwa mwarabu.
8.mwarabu akipewa bandari ,utamaduni wa kitanzania utaathirika na kufutika ndani ya miaka 30 ijayo..
9.watawala waliopo kwa sasa tanzania wamejikita katika kujenga "nchi" badala ya kujenga "taifa"
10. Mtanzanja ajengewe uwezo wa kuendesha mambo yake na sio kuendeshwa...

Maaskofu wakatoliki hawajakurupuka kwa wanachokifanya sasa..wanajua huko mbele nini kitatokea iwapo mwarabu atapewa bandari...

NB: The vatican intelligence and its fields of resources are second to none!!

From room NO.26 Gaborone..

Pascal Mayalla
Mambo mengine inabidi tucheke tu 😂😂
 
Kama ilivyo ada, kila wakati katika kila nchi kuna ajenda ama sakata linalolindima, linaweza kuwa la kisiasa, kijamii ama kiuchumi. Ikiwa sehemu ya nchi zenye Siasa za mlengo wa Kidemokrasia, Tanzania imeingia katika mjadala mkali kati ya Serikali, wadau wa uwekezaji, vyama vya upinzani, asasi na taasisi mbali mbali.

Mjadala huu unahusisha uwekezaji bandarini, Uwekezaji unaotarajiwa kufanywa na kampuni ya kimataifa ya DP-World kutoka nchini Saudia. Kuzuka kwa mjadala mkali kati ya Serikali, taaisisi na Wadau kumetokana na baadhi ya vipengele ambavyo vinaonekana kutoleta tija au maslahi kwa Taifa.

Lakini, hivi karibuni, kumeibuka na hisia mbali mbali baada ya Sakata hili kujadiliwa na Taasisi za kidini, hasa, baada ya Waraka wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini (TEC), Waraka ulioonyesha msimamo wa Baraza hilo ambao unakinzana na ule wa Serikali, wa kuruhusu uwekezaji wa kampuni ya DP-World kama ulivyoainishwa katika vipengele vya Mkataba huo (IGA)

Kati ya maswali yaliyogonga vichwa vya watu, ni wapi basi, Kanisa hili kongwe linapata Mamlaka ya kutangaza misimamo yake hadharani juu ya masuala ya Kisiasa licha ya kuwa Taasisi ya kidini.

HIZI NI SABABU KUU TATU ZINAZOIPA TAASISI HII USHAWISHI KWA SERIKALI YA TANZANIA.

  1. Mtaji watu: Historia inaonyesha, tangu kabla ya uhuru, Kanisa Katoliki nchini Tanzania, limekuwa na idadi kubwa ya waumini, ambao kimsingi ndio mtaji mkubwa wa ushawishi na nguvu ya kanisa hili kufikia 32% ya waumini mpaka 2022. Kama ujuavyo, Siasa inagusa maisha ya watu, lakini, mamlaka juu ya maisha ya watu hayaishii kwa Wanasiasa pekee. Zipo taasisi nyingine zenye nguvu juu ya maisha ya watu, nazo ni Taasisi za kidini, asasi za kiraia pamoja na mashirika. Yote haya yanagawana nguvu na Wanasiasa, lakini kwa upande wa Kanisa Katoliki, ushawishi wake ni mkubwa. Hivyo basi, si Kanisa linalohitaji Serikali ili liwe na nguvu, bali, ni Serikali kupitia Wanasiasa wake linahitaji Kanisa ili kuongeza na Kudumisha ushawishi na nguvu kwa watu linao waongoza.
  2. Mchango wa Kanisa Kanisa Katoliki katika maendeleo tangu uhuru: Kazi mojawapo kuu ya Serikali ni kutoa huduma za Kijamii, kama Elimu kupitia ujenzi wa Shule, Miundombinu na Afya kupitia ujezi wa Hospitali. Kihistoria, elimu tuliyoanza kuipata hata punde baada ya Uhuru ilikuwa ni elimu yenye chembe za Kikoloni. Lakini, mpaka inafika wakati wa Utekelezaji wa Sera za Kijamaa miaka 1967-80 Shule zilizokuwa zikimilikiwa na Kanisa Katoliki zilikuwa ni Mara tatu ya zile zilizojengwa na Serikali. Kwa kutoa fursa sawa, bila kuzingatia misingi au tamaduni za Kidini, Serikali iliamua kuzitaifisha zote, hivyo, Kanisa likapoteza Shule nyingi na Hospitali ili kutengeneza usawa. Wingi wa shule hizi, ulitokana na Uambatanishaji wa huduma za Kijamii kama Afya na Elimu uliokuwa unafanywa na Wamisionari, wa Katoliki. Jambo ambalo lilivutia watu wengi hususan wa eneo la bara kuishi karibu na maeneo hayo. Mbali na hilo, hata leo 2023 Kanisa hilo Limeendelea kuwa na umiliki wa Taasisi kama Shule, Vyuo na Hospitali nyingi zaidi nchini.
  3. Kanisa Katoliki, limelea na kukuza viongozi wengi wa Kisiasa, Kijeshi na Kijamii: Kuanzia awamu ya Kwanza mpaka awamu ya tano, Maraisi wote katika mfululizo wa maisha yao hawakuwahi kuepuka kabisa malezi ya Kanisa hili. Si tu Marais, bali hata viongozi wa ngazi za juu za Jeshi, wamelelewa na wengineo kama aliyekuwa Mkuu wa Majeshi aliyemaliza muda wake, Gen. Venance Salavatory Mabeyo. Kuna Wanasiasa wengi leo hii ambao wamelelewa na kanisa hili na kukuzwa katika malezi ya kirho, nidhamu na hata kufunzwa uongozi kupitia kanisa hili.
Hivyo basi, suala hapa si kuwa Kanisa hili linataka Ushawishi kutoka kwa Viongozi hawa, la hasha, ila kupitia Sababu hizi viongozi wa nchi hii wanaliheshimu Kanisa hili. Suala la Kanisa Katoliki kutoa Waraka na Kusomwa kwa Waumini wake, ambao kimsingi ndio Wananchi na Wateja wa Wanasiasa, ni jadi na utamaduni wake wa muda mrefu, ikiwa ni kama Itifaki ya Kanisa.

Kwa kumalizia, ndugu zangu mnaodhani Kanisa hili linatawala nchi eleweni halitawali kwa Mamlaka yake kikanisa, bali kwa ushawishi wake kama Taasisi kongwe, anayetawala nchi hii ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya Raia.

Ahsanteni.

Mwl. Diwani.

Rejea makala hii kutoka Vatican News - Mchango wa Kanisa Katoliki Nchini Tanzania! Elimu, Afya na Ustawi wa Jamii
DP wanatoka Dubai na sio Saudia mkuu
 
Umesahau mchango wao mwingine mkubwa- kueneza ukoloni
 
Kanisa katoliki ni project ya wazungu kuvuna mali za waafrika italia kwenyewe njaa kali homeless kila kona. Italia ni moja ya nchi maskini ulaya na pia hii theory yako ina fit zaidi miaka ya 1950-2000s sasa hivi morality ya katoliki hakuna na makanisa ulaya yanafungwa au kugeuzwa kumbi za starehe kila mtu anajua vicarious fill dei ni 666 na pontif ndiyo kijana wa shetani. Mali za dunia zinahama ulaya magharibi na kuhamia asia arabia Afrika na ulaya mashariki endelea kuota
 
Tusikae kimya sasa kusubiri miaka 10 ijayo Rais wetu aandike Kitabu cha kujutia kuingia mkataba huu mbovu wa Bandari, tumkosoe mapema ili akija kuandika kitabu hicho aseme nilishauriwa ila nilikataa Ushauri"-Baba Paroko wetu leo 27/08/2023
Miaka kumi ijayo uchumi wetu ukiwa umekua na nchi yetu kwa wakati huo ikiwa ni hub inayoheshimika katika ukanda kama utakuwa hai ni vizuri uje umpongeze rais Samia kwa maono yake na kujiamini kwake akiwa mkuu wa nchi iitwayo Tanzania.

Utakuwa umetenda uungwana wa hali ya juu kwa kuwa na maoni yenye kutenda haki na sio kuwa sehemu ya wanaoweza sana kulaumu mpaka wanausahau wajibu wao wa kufuatilia kauli zao, kumbuka hii ni kauli kubwa sana yenye kumhitaji anayeiweka hadharani kuwa wa kwanza kufuatilia ndani ya hiyo miaka kumi huo mrejesho wake utakuwa vipi.
 
Kama ilivyo ada, kila wakati katika kila nchi kuna ajenda ama sakata linalolindima, linaweza kuwa la kisiasa, kijamii ama kiuchumi. Ikiwa sehemu ya nchi zenye Siasa za mlengo wa Kidemokrasia, Tanzania imeingia katika mjadala mkali kati ya Serikali, wadau wa uwekezaji, vyama vya upinzani, asasi na taasisi mbali mbali.

Mjadala huu unahusisha uwekezaji bandarini, Uwekezaji unaotarajiwa kufanywa na kampuni ya kimataifa ya DP-World kutoka nchini Saudia. Kuzuka kwa mjadala mkali kati ya Serikali, taaisisi na Wadau kumetokana na baadhi ya vipengele ambavyo vinaonekana kutoleta tija au maslahi kwa Taifa.

Lakini, hivi karibuni, kumeibuka na hisia mbali mbali baada ya Sakata hili kujadiliwa na Taasisi za kidini, hasa, baada ya Waraka wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini (TEC), Waraka ulioonyesha msimamo wa Baraza hilo ambao unakinzana na ule wa Serikali, wa kuruhusu uwekezaji wa kampuni ya DP-World kama ulivyoainishwa katika vipengele vya Mkataba huo (IGA)

Kati ya maswali yaliyogonga vichwa vya watu, ni wapi basi, Kanisa hili kongwe linapata Mamlaka ya kutangaza misimamo yake hadharani juu ya masuala ya Kisiasa licha ya kuwa Taasisi ya kidini.

HIZI NI SABABU KUU TATU ZINAZOIPA TAASISI HII USHAWISHI KWA SERIKALI YA TANZANIA.

  1. Mtaji watu: Historia inaonyesha, tangu kabla ya uhuru, Kanisa Katoliki nchini Tanzania, limekuwa na idadi kubwa ya waumini, ambao kimsingi ndio mtaji mkubwa wa ushawishi na nguvu ya kanisa hili kufikia 32% ya waumini mpaka 2022. Kama ujuavyo, Siasa inagusa maisha ya watu, lakini, mamlaka juu ya maisha ya watu hayaishii kwa Wanasiasa pekee. Zipo taasisi nyingine zenye nguvu juu ya maisha ya watu, nazo ni Taasisi za kidini, asasi za kiraia pamoja na mashirika. Yote haya yanagawana nguvu na Wanasiasa, lakini kwa upande wa Kanisa Katoliki, ushawishi wake ni mkubwa. Hivyo basi, si Kanisa linalohitaji Serikali ili liwe na nguvu, bali, ni Serikali kupitia Wanasiasa wake linahitaji Kanisa ili kuongeza na Kudumisha ushawishi na nguvu kwa watu linao waongoza.
  2. Mchango wa Kanisa Kanisa Katoliki katika maendeleo tangu uhuru: Kazi mojawapo kuu ya Serikali ni kutoa huduma za Kijamii, kama Elimu kupitia ujenzi wa Shule, Miundombinu na Afya kupitia ujezi wa Hospitali. Kihistoria, elimu tuliyoanza kuipata hata punde baada ya Uhuru ilikuwa ni elimu yenye chembe za Kikoloni. Lakini, mpaka inafika wakati wa Utekelezaji wa Sera za Kijamaa miaka 1967-80 Shule zilizokuwa zikimilikiwa na Kanisa Katoliki zilikuwa ni Mara tatu ya zile zilizojengwa na Serikali. Kwa kutoa fursa sawa, bila kuzingatia misingi au tamaduni za Kidini, Serikali iliamua kuzitaifisha zote, hivyo, Kanisa likapoteza Shule nyingi na Hospitali ili kutengeneza usawa. Wingi wa shule hizi, ulitokana na Uambatanishaji wa huduma za Kijamii kama Afya na Elimu uliokuwa unafanywa na Wamisionari, wa Katoliki. Jambo ambalo lilivutia watu wengi hususan wa eneo la bara kuishi karibu na maeneo hayo. Mbali na hilo, hata leo 2023 Kanisa hilo Limeendelea kuwa na umiliki wa Taasisi kama Shule, Vyuo na Hospitali nyingi zaidi nchini.
  3. Kanisa Katoliki, limelea na kukuza viongozi wengi wa Kisiasa, Kijeshi na Kijamii: Kuanzia awamu ya Kwanza mpaka awamu ya tano, Maraisi wote katika mfululizo wa maisha yao hawakuwahi kuepuka kabisa malezi ya Kanisa hili. Si tu Marais, bali hata viongozi wa ngazi za juu za Jeshi, wamelelewa na wengineo kama aliyekuwa Mkuu wa Majeshi aliyemaliza muda wake, Gen. Venance Salavatory Mabeyo. Kuna Wanasiasa wengi leo hii ambao wamelelewa na kanisa hili na kukuzwa katika malezi ya kirho, nidhamu na hata kufunzwa uongozi kupitia kanisa hili.
Hivyo basi, suala hapa si kuwa Kanisa hili linataka Ushawishi kutoka kwa Viongozi hawa, la hasha, ila kupitia Sababu hizi viongozi wa nchi hii wanaliheshimu Kanisa hili. Suala la Kanisa Katoliki kutoa Waraka na Kusomwa kwa Waumini wake, ambao kimsingi ndio Wananchi na Wateja wa Wanasiasa, ni jadi na utamaduni wake wa muda mrefu, ikiwa ni kama Itifaki ya Kanisa.

Kwa kumalizia, ndugu zangu mnaodhani Kanisa hili linatawala nchi eleweni halitawali kwa Mamlaka yake kikanisa, bali kwa ushawishi wake kama Taasisi kongwe, anayetawala nchi hii ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa niaba ya Raia.

Ahsanteni.

Mwl. Diwani.

Rejea makala hii kutoka Vatican News - Mchango wa Kanisa Katoliki Nchini Tanzania! Elimu, Afya na Ustawi wa Jamii
Nikili leo nimependa kufuatilia makala zako. Nilichojifunza, uandishi wako hauna lengo la kuegemea upande wowote hisipokuwa facts tu. Ni kweli ulivyoeleza ndiyo nguvu ya Kanisa Katoliki.

Lengo la dini yoyote pamoja na kufundisha mambo ya kiroho ni kuhakikisha kuwepo na ustawi wa jamii. Sasa nini kinachangia ktk ustawi wa jamii, ni swala linalotuchanganya watu wengi na tunapokosa majibu sahihi ndiyo tunakuja na lugha za "kuchanganya dini na siasa". Kabla sijaendelea, Somalia leo hakuna utulivu na watu wengi ni Waislam. Je, wachanganya dini hipi na siasa? DRC pale je, ni dini hipi inachanganywa na siasa?

TEC wako sahihi kabisa walipotoa ule waraka wao kwasababu moja ya majukumu yake ni ustawi wa jamii. Na waraka wenyewe haukulenga kuishambulia dini nyingine yoyote wala serikali bali walionyesha vipengere vilivyo na kasoro ndani ya mkaba ule. Ni jambo jema ambalo makundi mengine katika jamii yangetamani kulifanya. Wametoa hoja na nilitegemea wapingaji nao wawapinge kwa hoja Ila kinachotokea wote tunakijua. Ni muda mrefu sana viongozi wa dini wamekuwa wakishiriki shughuli za kiasa. Nitolee mfano, kipindi cha hawamu ya tano, makundi ya kidini karibu yote yalikuwa hayaachwi nyuma kwenye shughuli za Serikali na pengine ktk mikutano ya kisiasa. Tulisikia makundi haya dini yakitoa sifa kedekede kwa viongozi. Ukipewa sifa ukubali kukosolewa pale unapokosea. Sasa iweje kwenye kupewa sifa siyo kuchanganya dini na siasa, hisipokuwa kwenye kukosoa?

Jambo la ukidini ktk sakata hili limekuzwa na wanasiasa wenyewe hasa pale walipokosa hoja za msingi kutetea mkataba wenyewe. Viongozi niliowahi kuwasikia akiwemo prof. Kitila wote wana majibu ya jumlajumla tofauti na kinachohojiwa ndani ya mkataba. Wanachofanya ni drama ya kumfurahisha mwenye nyumba. Sasa ktk jamii si wote tuna uelewa wa aina moja. Nadhani kuna kundi lina machungu dhidi ya katoliki na hichi ndicho tunachokishuhudia. Nasema kundi kwasababu si wote kama tunavyoweza kudhani.

Mwarobaini wa kulimaliza hili, ni Rais mwenyewe kukemea na kuruhu mjadala, wanaopinga mkataba wapinge kwa hoja na wanaokubaliana nao waukubali kwa hoja zilizomo ndani ya mkaba wenyewe na siyo kushambuliana.
 
Miaka kumi ijayo uchumi wetu ukiwa umekua na nchi yetu kwa wakati huo ikiwa ni hub inayoheshimika katika ukanda kama utakuwa hai ni vizuri uje umpongeze rais Samia kwa maono yake na kujiamini kwake akiwa mkuu wa nchi iitwayo Tanzania.

Utakuwa umetenda uungwana wa hali ya juu kwa kuwa na maoni yenye kutenda haki na sio kuwa sehemu ya wanaoweza sana kulaumu mpaka wanausahau wajibu wao wa kufuatilia kauli zao, kumbuka hii ni kauli kubwa sana yenye kumhitaji anayeiweka hadharani kuwa wa kwanza kufuatilia ndani ya hiyo miaka kumi huo mrejesho wake utakuwa vipi.
Mkataba una mapungufu uzuri hata yeye samia anajua hilo japo kashupaza shingo,kwa hili limkataba hakuna pongezi yoyote huko mbele ya safari imeshaonyesha toka mwanzo haufai
 
Huo sio mkataba wa kwanza kushughulikia mradi mkubwa hapa Tanzania, umeshaitazama mingine iliyotangulia na kuulinganisha na huu wa sasa?.
 
Kanisa Katoliki sio dhehebu. Kanisa Katoliki sio taasisi. Kanisa Katoliki ni Mamlaka.

Kanisa Katoliki ni mamlaka ya dini. Ndilo lililo na mamlaka yote duniani juu ya watu na Serikali.

Nguvu ya Kanisa Katoliki si kwa sababu ndilo lina waamini wengi duniani au kwa sababu lina nguvu za uchumi na elimu; au kwa sababu ya shughuli zake za kijami. Haya kwa yenyewe ni mambo madogo ambayo hayawezi kufanya liwe na nguvu wakati wote katika historia miaka zaidi ya elfu mbili sasa.
It's supernatural powerful, hakuna anaweza kulibomoa, awe papa, serikali wala Taifa lolote. Dola ya kirumi ilisalimu amri, ukomonisti ukajifia! Kila anatishia uhai wake anabomoka yeye. Miaka zaidi ya 2000 linasonga.
 
Huo sio mkataba wa kwanza kushughulikia mradi mkubwa hapa Tanzania, umeshaitazama mingine iliyotangulia na kuulinganisha na huu wa sasa?.
Huu ni wa kimangungo haufai pamoja na watu kuwa na uelewa sasa pamoja na kupata uzoefu kwa iliyopita mama abdul katuangusha kuingia mkataba mbovu kama huu
 
KUtoka vyanzo ndani ya ubaloz wa vatican tanzania
1.waarabu wakipewa bandari,agenda kubwa sio kuendeleza bandari bali kueneza uislam na waislam ndio watawale tanzania kwa miongo kadhaa
2.waarabu wakipewa bandari zote za majini na nchi kavu, basi wataingiza silaha kiholela na kuunda vikundi vya uasi na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe (watanzania )
3.waarabu wakipewa bandari,kuna mgogoro wa kimkakati utatokea bainabya visiwan na bara na hivyo visiwani wataamua kujitenga hasa ikizingatiwa upande wao hakuna bandari amepewa mwarabu.
4.mwarabu akipewa babandari si atafanya kaz zihusuzo bandari bali wataingilia mifumo mingine ya kitaasisi na kujinufaisha wao na mabwana zao waliowapa bandari....
5.mwarabu akipewa bandari kundi kubwa la vijana wa kitanzania watakosa ajira.
6.kwa kutukia mfano wa loliondo eneo analomiki mwarabu tangu miaka ya 90 na kupelekea vifo vya watu waliojaribu kupaza sauti kama hayati stan katabalo..vivyo hivyo wakipewa badari maisha ya watanzania yatakuwa duni mara mbili ya ilivyo sasa..
7.mwarabua akipewa bandari..mamlaka nyingi za ndan ya nchi zitapigwa marufuku kutekelez majukuku yao ndan ya maeneo aliyokabidhiwa mwarabu.
8.mwarabu akipewa bandari ,utamaduni wa kitanzania utaathirika na kufutika ndani ya miaka 30 ijayo..
9.watawala waliopo kwa sasa tanzania wamejikita katika kujenga "nchi" badala ya kujenga "taifa"
10. Mtanzanja ajengewe uwezo wa kuendesha mambo yake na sio kuendeshwa...

Maaskofu wakatoliki hawajakurupuka kwa wanachokifanya sasa..wanajua huko mbele nini kitatokea iwapo mwarabu atapewa bandari...

NB: The vatican intelligence and its fields of resources are second to none!!

From room NO.26 Gaborone..

Pascal Mayalla

Maaskofu wako kwa manufaa ya Kanisa Cathoric, hakuna askofu anayefanya kazi kwa manufaa ya Taifa hili.

Ukishafika level fulani ndani ya Catholic tayari wewe ni mtumishi wa Vatican na Catholic na upo kwa maslahi yao, mengine ni story tu.

Lamsingi, tutumikie Taifa letu kwa manufaa ya Taifa letu na sio kuwa vibaraka wa mambo tusiyoyajua.
 
It's supernatural powerful, hakuna anaweza kulibomoa, awe papa, serikali wala Taifa lolote. Dola ya kirumi ilisalimu amri, ukomonisti ukajifia! Kila anatishia uhai wake anabomoka yeye. Miaka zaidi ya 2000 linasonga.
Umesema yote kwa mara moja.

Miaka zaidi ya elfu mbili kuna tawala mbalimbali zenye nguvu zilikuja na kuondoka. Kuna uzushi na mavuguvu mbalimbali yalikuja na kuondoka.

Kwa mtu makini anaeangalia historia, hawezi kusema Kanisa Katoliki lina nguvu kwa sababu ya idadi yake ya watu duniani, au kwa sababu ya shughuli zake za kijamii na uchumi au elimu na tafiti maana kama ni hivyo kuna tawala nyingi zilizopata kuwa na nguvu zote za kiuchumi, elimu, tafiti na teknolojia na kwa vipindi mbalimbali zimejaribu kuliangusha Kanisa, lakini badala yake tawala hizo zimeanguka zenyewe, Kanisa linaendelea.

Wakuu wa nchi na Serikali wanajua Kanisa Katoliki ni nini. Lakini kuna baadhi hawajui na hawa mara nyingi katika historia huwa wanajaribu kukabiliana na Kanisa.
 
Nyie watu hivi mmechanganyikiwa nini? Wana nguvu gani?

Hizo hoja ulizosema hapo zote hazina msingi. Hizo ni fikra mgando ambazo mmekuwa mkilishana katika vijiwe vyenu vya kahawa huko alafu unakuja kutudanganya humu wenze akili zetu?

Sicilia nikwambie mtoa mada. Hakuna nguvu ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania. Hawana nguvu yeyote ile. Hata kwa Wakristo tu kwa sasa nchini Tanzania wakristo wengi wapo kwenye madhehebu ya kiprotestant na haya ndo madhehebu yenye ukwasi nchini kwa sasa.

Hata ukija kwenye oradea ya matajiri wa Tanzania. Ambao hawa ndo watu ambao unaweza sema wanaweza tetemesha nchi wengi ni waislamu na wachache waliobaki ambao ni wakristo wengi ni wadhehebu ya kiprotestant hasa walutheri.

Hiyo nguvu ya kabisa katoliki mmeitoa wapi?
Aisee!
 
Maaskofu wako kwa manufaa ya Kanisa Cathoric, hakuna askofu anayefanya kazi kwa manufaa ya Taifa hili.

Ukishafika level fulani ndani ya Catholic tayari wewe ni mtumishi wa Vatican na Catholic na upo kwa maslahi yao, mengine ni story tu.

Lamsingi, tutumikie Taifa letu kwa manufaa ya Taifa letu na sio kuwa vibaraka wa mambo tusiyoyajua.
Taifa lako ni lipi? Kwa msingi gani unasema maaskofu wanatumikia Vatican?
 
Huu ni wa kimangungo haufai pamoja na watu kuwa na uelewa sasa pamoja na kupata uzoefu kwa iliyopita mama abdul katuangusha kuingia mkataba mbovu kama huu
Mikataba isiyo ya kimangungo umeshawahi kuiona?, faida zake zikianza kuonekana hautakumbuka lolote kuhusu mkataba.
 
Back
Top Bottom