Hapa ndipo inapotoka nguvu ya Kanisa Katoliki

Wewe hata huna ulijualo na bahati mbaya sana huwa sipendi mipasho hiyo ya 'pye pye pye' umeshindwa kujenga hoja yako.Ngoja nifanye umeshinda Boss,nilikuignore kwa kukuitikia 'sawa boss' lakini hukunielewa.Sasa naitikia tena kwa herufi kubwa SAWA BOSS UMESHINDA.
 
Tulia acha kutetea wafanya Biashara hakuna shule ya kiislam ya bure wala ya kikatoliki ya bure wote ukienda huduma zao utauziwa tuuuu wote wafanya biashara

Si hospital sio vyuo sio Shule
SAWA BOSS UMESHINDA
 
Mambo mengine inabidi tucheke tu 😂😂
 
DP wanatoka Dubai na sio Saudia mkuu
 
Umesahau mchango wao mwingine mkubwa- kueneza ukoloni
 
Kanisa katoliki ni project ya wazungu kuvuna mali za waafrika italia kwenyewe njaa kali homeless kila kona. Italia ni moja ya nchi maskini ulaya na pia hii theory yako ina fit zaidi miaka ya 1950-2000s sasa hivi morality ya katoliki hakuna na makanisa ulaya yanafungwa au kugeuzwa kumbi za starehe kila mtu anajua vicarious fill dei ni 666 na pontif ndiyo kijana wa shetani. Mali za dunia zinahama ulaya magharibi na kuhamia asia arabia Afrika na ulaya mashariki endelea kuota
 
Tusikae kimya sasa kusubiri miaka 10 ijayo Rais wetu aandike Kitabu cha kujutia kuingia mkataba huu mbovu wa Bandari, tumkosoe mapema ili akija kuandika kitabu hicho aseme nilishauriwa ila nilikataa Ushauri"-Baba Paroko wetu leo 27/08/2023
Miaka kumi ijayo uchumi wetu ukiwa umekua na nchi yetu kwa wakati huo ikiwa ni hub inayoheshimika katika ukanda kama utakuwa hai ni vizuri uje umpongeze rais Samia kwa maono yake na kujiamini kwake akiwa mkuu wa nchi iitwayo Tanzania.

Utakuwa umetenda uungwana wa hali ya juu kwa kuwa na maoni yenye kutenda haki na sio kuwa sehemu ya wanaoweza sana kulaumu mpaka wanausahau wajibu wao wa kufuatilia kauli zao, kumbuka hii ni kauli kubwa sana yenye kumhitaji anayeiweka hadharani kuwa wa kwanza kufuatilia ndani ya hiyo miaka kumi huo mrejesho wake utakuwa vipi.
 
Nikili leo nimependa kufuatilia makala zako. Nilichojifunza, uandishi wako hauna lengo la kuegemea upande wowote hisipokuwa facts tu. Ni kweli ulivyoeleza ndiyo nguvu ya Kanisa Katoliki.

Lengo la dini yoyote pamoja na kufundisha mambo ya kiroho ni kuhakikisha kuwepo na ustawi wa jamii. Sasa nini kinachangia ktk ustawi wa jamii, ni swala linalotuchanganya watu wengi na tunapokosa majibu sahihi ndiyo tunakuja na lugha za "kuchanganya dini na siasa". Kabla sijaendelea, Somalia leo hakuna utulivu na watu wengi ni Waislam. Je, wachanganya dini hipi na siasa? DRC pale je, ni dini hipi inachanganywa na siasa?

TEC wako sahihi kabisa walipotoa ule waraka wao kwasababu moja ya majukumu yake ni ustawi wa jamii. Na waraka wenyewe haukulenga kuishambulia dini nyingine yoyote wala serikali bali walionyesha vipengere vilivyo na kasoro ndani ya mkaba ule. Ni jambo jema ambalo makundi mengine katika jamii yangetamani kulifanya. Wametoa hoja na nilitegemea wapingaji nao wawapinge kwa hoja Ila kinachotokea wote tunakijua. Ni muda mrefu sana viongozi wa dini wamekuwa wakishiriki shughuli za kiasa. Nitolee mfano, kipindi cha hawamu ya tano, makundi ya kidini karibu yote yalikuwa hayaachwi nyuma kwenye shughuli za Serikali na pengine ktk mikutano ya kisiasa. Tulisikia makundi haya dini yakitoa sifa kedekede kwa viongozi. Ukipewa sifa ukubali kukosolewa pale unapokosea. Sasa iweje kwenye kupewa sifa siyo kuchanganya dini na siasa, hisipokuwa kwenye kukosoa?

Jambo la ukidini ktk sakata hili limekuzwa na wanasiasa wenyewe hasa pale walipokosa hoja za msingi kutetea mkataba wenyewe. Viongozi niliowahi kuwasikia akiwemo prof. Kitila wote wana majibu ya jumlajumla tofauti na kinachohojiwa ndani ya mkataba. Wanachofanya ni drama ya kumfurahisha mwenye nyumba. Sasa ktk jamii si wote tuna uelewa wa aina moja. Nadhani kuna kundi lina machungu dhidi ya katoliki na hichi ndicho tunachokishuhudia. Nasema kundi kwasababu si wote kama tunavyoweza kudhani.

Mwarobaini wa kulimaliza hili, ni Rais mwenyewe kukemea na kuruhu mjadala, wanaopinga mkataba wapinge kwa hoja na wanaokubaliana nao waukubali kwa hoja zilizomo ndani ya mkaba wenyewe na siyo kushambuliana.
 
Mkataba una mapungufu uzuri hata yeye samia anajua hilo japo kashupaza shingo,kwa hili limkataba hakuna pongezi yoyote huko mbele ya safari imeshaonyesha toka mwanzo haufai
 
Mkataba una mapungufu uzuri hata yeye samia anajua hilo japo kashupaza shingo,kwa hili limkataba hakuna pongezi yoyote huko mbele ya safari imeshaonyesha toka mwanzo haufai
Huo sio mkataba wa kwanza kushughulikia mradi mkubwa hapa Tanzania, umeshaitazama mingine iliyotangulia na kuulinganisha na huu wa sasa?.
 
It's supernatural powerful, hakuna anaweza kulibomoa, awe papa, serikali wala Taifa lolote. Dola ya kirumi ilisalimu amri, ukomonisti ukajifia! Kila anatishia uhai wake anabomoka yeye. Miaka zaidi ya 2000 linasonga.
 
Huo sio mkataba wa kwanza kushughulikia mradi mkubwa hapa Tanzania, umeshaitazama mingine iliyotangulia na kuulinganisha na huu wa sasa?.
Huu ni wa kimangungo haufai pamoja na watu kuwa na uelewa sasa pamoja na kupata uzoefu kwa iliyopita mama abdul katuangusha kuingia mkataba mbovu kama huu
 

Maaskofu wako kwa manufaa ya Kanisa Cathoric, hakuna askofu anayefanya kazi kwa manufaa ya Taifa hili.

Ukishafika level fulani ndani ya Catholic tayari wewe ni mtumishi wa Vatican na Catholic na upo kwa maslahi yao, mengine ni story tu.

Lamsingi, tutumikie Taifa letu kwa manufaa ya Taifa letu na sio kuwa vibaraka wa mambo tusiyoyajua.
 
It's supernatural powerful, hakuna anaweza kulibomoa, awe papa, serikali wala Taifa lolote. Dola ya kirumi ilisalimu amri, ukomonisti ukajifia! Kila anatishia uhai wake anabomoka yeye. Miaka zaidi ya 2000 linasonga.
Umesema yote kwa mara moja.

Miaka zaidi ya elfu mbili kuna tawala mbalimbali zenye nguvu zilikuja na kuondoka. Kuna uzushi na mavuguvu mbalimbali yalikuja na kuondoka.

Kwa mtu makini anaeangalia historia, hawezi kusema Kanisa Katoliki lina nguvu kwa sababu ya idadi yake ya watu duniani, au kwa sababu ya shughuli zake za kijamii na uchumi au elimu na tafiti maana kama ni hivyo kuna tawala nyingi zilizopata kuwa na nguvu zote za kiuchumi, elimu, tafiti na teknolojia na kwa vipindi mbalimbali zimejaribu kuliangusha Kanisa, lakini badala yake tawala hizo zimeanguka zenyewe, Kanisa linaendelea.

Wakuu wa nchi na Serikali wanajua Kanisa Katoliki ni nini. Lakini kuna baadhi hawajui na hawa mara nyingi katika historia huwa wanajaribu kukabiliana na Kanisa.
 
Aisee!
 
Taifa lako ni lipi? Kwa msingi gani unasema maaskofu wanatumikia Vatican?
 
Huu ni wa kimangungo haufai pamoja na watu kuwa na uelewa sasa pamoja na kupata uzoefu kwa iliyopita mama abdul katuangusha kuingia mkataba mbovu kama huu
Mikataba isiyo ya kimangungo umeshawahi kuiona?, faida zake zikianza kuonekana hautakumbuka lolote kuhusu mkataba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…