Happy birthday Mtume na nabii wa mwisho wa Soka Saint Gaucho

Happy birthday Mtume na nabii wa mwisho wa Soka Saint Gaucho

Yupo Mexico anakula bataaaaa... Ameisha hana chake.. Hata mwanangu hamjui, lakini muulize kuhusu Messi atakutajia hadi mtaa anaotoka kule Argentina sijui kajulia wapi.


Usirogwe kumuonesha clip za dinho!!

Hatomtaka huyo messi
 
Usirogwe kumuonesha clip za dinho!!

Hatomtaka huyo messi

Hahahahah! Sina uhakika, nampa uhuru maana hata huyu MESSI kamjua mwenyewe tu.

Ila kwa jinsi anavoongea akimjua dinho maskani hapatakalika
 
Hahah mkuu uwasilishaji wako umefanikiwa kuiteka hadhila hahah, gaucho oyee
  • Huu uandishi wake , hakika hata mimi nimekamatika
Huyu ndie Ronaldo de Assis Moreirra almaarufu kama Ronaldinho Gaucho the saint ambae akiwa uwanjani basi Malaika huacha shughuli zao na kuanza kumtazama.
 
Kwanza alikua ni mtoto mdogo aliyebebwa na mastaa wakomavu sana.. Na ndio maana baada ya hapo hawakua na jipya, huyu jamaa hajadumu ktk ubora, mbwembwe zilimzidi huyu.


Robo Fainali dhidi ya England anatengeneza goli la kwanza na kisha anakuja kupiga freekick ambayo hata makipa wangekuwa wanne pale wasingeudaka ule mpira...mpaka mwisho Brazil 2-1 England

Hah hah hah Haters mwaka huu mtatofautisha kati ya Busha na Shipa.
 
Hili halipingiki mkuu.. Messi ni kiumbe wa ajabu huyu.


Nesi mwenyewe anakiri kuwa ile pasi aliopewa na Saint Gaucho ambayo ndio ilifungua ukurasa wake wa kufunga magoli pale Barca ndio iliokuwa na mwangaza wa mafanikio anayoyapata kwa sasa, pia anasisitiza kuwa tangu hapo hatokuja kujifananisha na Gaucho coz Gaucho ni God Father wake.

Kwi kwi kwi kwiiiiii
 
Ukiachana na WC mimi sioni kingine Gaucho anachomzid Messi. Gaucho ana mbwembwe sana, ila Messi the way anavyodribble ni burudani tosha kabisa sababu hata Gaucho hadrible kama Messi kwa mimi nionavyo.
Halafu Messi anazile chenga zake za kukutisha kama anaenda kushoto au kulia, ukienda upande huu yeye anaenda upande huu.


Hizo chenga za Nesi hata Mwaikimba anapiga, ila je ni nani ambae ameweza kufanya miujiza aliofanya Ronaldo de Assis Moreirra akiwa kwenye mechi?

Ndo maana unaona hata hapo Simba Sports Kilabu kuna Nesi, ila huwezi kusikia New Gaucho.
 
Nesi mwenyewe anakiri kuwa ile pasi aliopewa na Saint Gaucho ambayo ndio ilifungua ukurasa wake wa kufunga magoli pale Barca ndio iliokuwa na mwangaza wa mafanikio anayoyapata kwa sasa...pia anasisitiza kuwa tangu hapo hatokuja kujifananisha na Gaucho coz Gaucho ni God Father wake...

kwi kwi kwi kwiiiiii

We mkuu usipotoshe jamii,, leta ushahidi wote
 
Yupo Mexico anakula bataaaaa... Ameisha hana chake.. Hata mwanangu hamjui, lakini muulize kuhusu Messi atakutajia hadi mtaa anaotoka kule Argentina sijui kajulia wapi.


Hah ah hah kama wewe Baba mtu unamjuwa Nabii wa mwisho wa soka basi huyo mwanao atamjuwa siku si nyingi its a matter of time.
 
Gaucho ndio mchezaji Wang wa uhai wangu. Jamaa anajua


Sio wewe tu mkuu, ile ni kwa yeyote anaeujua Mpira. Ila kwa hawa wanaoangalia mpira mara wabadilishe channel na kuangalia FUTUHI hawawezi kuelewa nini Nabii Gaucho kafanya na ndio maana wanachuma dhambi tu hapa.
 
Sio wewe tu mkuu, ile ni kwa yeyote anaeujua Mpira, ila kwa hawa wanaoangalia mpira mara wabadilishe channel na kuangalia FUTUHI hawawezi kuelewa nini Nabii Gaucho kafanya na ndio maana wanachuma dhambi tu hapa

Usijiseme mkuu. Futa na povu afu panga hoja.
 
Clip za mwaka gani labda? Mimi Gaucho nimemuona akiwa ktk zama zake.
Hajakuwa mwiba kama Messi.


Hah hah hah hah kama Nesi ni Mwiba basi Dinho ni Msumali. Hata ukivaa Timbaland cha moto utakiona.
 
Usijiseme mkuu.. Futa na povu afu panga hoja... Hahahahahah

Hoja ipo hapo juu.

Hoja ni kumtakia maadhimisho mema ya siku ya kuzaliwa Mtume na Nabii wa mwisho wa Soka yaani Saint Ronaldo de Assis Moreirra almaarufu kama Ronaldinho Dinho Gaucho. Haya tuma salam zako sasa za kumtakia maisha mema kisha futa povu then twende kwenye jukwaa la Gaucho vs Nesi
 
Back
Top Bottom