Tunapata taabu sana kukuelewa unapoishia kulalamika kua Magufuli ni muovu bila kuuweka wazi huo uovu wenyewe sasa.
1) Kutaka Mtu Kama Jecha apewe Tuzo Ni Unafiki na Uovu
2) Kutupa Vitu vya Mwanasiasa Mwenzako Nje kwa Kisingizio cha Deni halafu Baadaye Unajifanya wote watupiwe, Zimepita siku saba hakuna aliyetupiwa ni Uovu.
3) Kusema Seif akiumwa aachwe afe ni Uovu
4)Kuzuia Mikutano na shughuli za Kisiasa za Vyama Vingine wakati wewe Unafanya Siasa kwa nyimbo Bendera na Uniform pamoja na Hotuba za Uwongo na Majitaka Ni Uovu.
5)Kuzuia Mahafali za wanavyuo wa Chadema Wakati wa CCM wanafanya Maafali hayohayo kwa Uniform, Kwa Nyimbo za siasa Ni Uovu
6) Kuwatuma Polisi wamlinde na Wasimguse Lipumbavu huku akivunja Ofisi za CUF na Kupiga Mlinzi Ni Uovu
7)Kumtumia Mtungi Kuvuruga Demokrasia Ni Uovu
8)Kuzuia Mawazo Kuzikwa mpaka Mahakama ikaingilia Ni Uovu
9) Kupeleka FFU na Mbwa Bungeni Kupiga Wabunge ni Uovu
10) Kufukuzia watoto wa Masikini 7000 Mitaani kwa Makosa yasiyo yao Na Kisha Kuwatukana Vilaza (ingawa wao wanajua Kiingereza) Ni Uovu sana
11) Kukamata Wanasiasa Kwa Kesi za Kuwasingizia Uchochezi ati tu kwa Kukupinga ni Uovu
12) Kukamata Vijana Wadogo Mitandaoni kuwapiga Kuwaweka Rumande zaidi ya Miezi Bila kesi ati walikutukana Mtu Uliyeshangilia Lowassa akitukanwa Matusi ya Nguoni na Ukashangilia, Ni Uovu.
13) Kutuma Wakuu wa Wilaya na Mikoa Wavuruge Upinzania Majiji ambayo Wapinzani Ni Mameya Ni Uovu.
14) Kujifanya Huendi UN, kwa Kisingizio cha Tetemeko, huku Ukigoma kabisa kwenda kutembelea Wahanga uone hali halisi Ni Ujinga na Uovu
15) Kuweka Wakurugenzi wa Wilaya Makada wa CCM huku ukijua wao ndio wanaosimamia Chaguzi na Maendeleo Ni Uovu, Hila na Ujinga.
16) Kutokuchunguza Mauaji ya Polisi wanne waliouawa ili wasingiziwe CHADEMA na UKUTA Ni Uovu Mkubwa sana, Hata tu Kuchunguza? nani anaamini wale Polisi waliuawa na Majambazi?
Nimechoka Mwingine aendelee na List