Harbinder Sigh Seth amewekeza nini Tanzania kinacholipa fedha alizoelekezwa? Akirudi kwao Kenya itakuwaje?

Harbinder Sigh Seth amewekeza nini Tanzania kinacholipa fedha alizoelekezwa? Akirudi kwao Kenya itakuwaje?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Huyu Mzee ameiba matrilioni ya nchi yetu. Watoto hawana madawati Wala madarasa, hospitali hazina madawa, mishahara haipandi nk then anahukumiwa alipe bilion zaidi ya ishirini anatangulia milioni mia mbili. Are we serious? Hizo bilioni 26 zitalipwa au ametupiga?

Ukiisoma taarifa za Kenya it's like huyu ni raia wa Kenya na amepiga dili huko pia kabla yakuja Tanzania. Je, hapa nchini amewekeza nini tunachoweza kuuza akitiroka?

Kwa umri wake na ujanja alionao na kwa kuzingatia hukumu ya jana isiyo na masharti magumu kwake tunaamini vipi kwamba atalipa? Kwa uzee ule akigoma akikimbia nchi tutafanya Nini?

Kuna watu wameshangilia kusikia bilioni kadhaa zitalipwa, ila nadhani tunapaswa kuitaka serikali iwe inatupa updates kila zinapolipwa isijekuwa game limechezwa kati ya DPP na mahakama Mzee atoke na tusilipwe fedha iliyoamuliwa.

Sitosau nilivyodhulumiwa noha yangu kipindi cha makinikia.
 
Maswali uliyo nayo, kila mtu anayo ila hatuna wa lutupatia majibu sahihi.

Tujipe muda, muda ni mwalimu mzuri sana and by then tutajua kila kitu kama tumepigwa au kama kuna jambo linafichwa, ila nahisi huyu singasinga atatoroka nchi very soon given kwamba hata hati ya kusafiria bado anayo.
 
Kwao huyu asili yake Mkinga wa Iringa Tanzania, ni mtanzania kindakindaki na mmoja wa wafanyabiashara wa kiTanzania waliofanikiwa kufanya biashara kubwa kubwa ndani na kimataifa tena kuaminiwa na serikali kadhaa nje ya Tanzania

Harbinder Seth (Singh) Iringa Tanzania from www.standardmedia.co.ke
2 Jul 2017 — ... the 1990s like business tycoon Harbinder Singh Sethi. Born and raised in Iringa, a small town in Tanzania's ...
Few people received top dollar construction contracts from the Kenyan government in the 1990s like business tycoon Harbinder Singh Sethi.

Born and raised in Iringa, a small town in Tanzania’s Southern Highlands, Sethi arrived in Nairobi in the 1980s.

At that time, the idea of tenderprenuership was still new in Kenya. But for a man who had founded his first company at 19, he knew at an early age that he could make a fortune from lucrative multi-billion shilling construction contracts from government entities.

Sethi quickly understood the Harambee spirit building up in Kenya and would from time to time show up at public functions to give ‘generous donations’. His donations would grab media headlines and endear him to government officials.

But it was not until after Ruaha Concrete Co Ltd, a firm he founded together with his siblings, was caught in scandals that his business activities in Kenya started receiving attention.

A 1997 report by the Auditor General found that Ruaha irregularly received a contract from Kenya Pipeline Company (KPC) to build a 9km access road. Despite this, the construction was still rocked by serious delays, large cost overruns and poor workmanship.

The project cost shot up two and a half times from Sh197 million in February 1995 to over Sh510 million by June 1998, when the road was finally completed. The auditor recommended that Ruaha Concrete be blacklisted and investigated.

READ MORE : How tycoon with dubious Kenyan past got entangled in Tanzania’s mega scam
 
Angefia jela pia ungeanzisha hii thread kuwa serikali imfufue Kwanza alipe hela, Bora alipe izo billions maisha yaendelee
 
Kwa umri wake na ujanja alionao na kwa kuzingatia hukumu ya jana isiyo na masharti magumu kwake tunaamini vipi kwamba atalipa? Kwa uzee ule akigoma akikimbia nchi tutafanya Nini?
Nanukuu "ana puto tumboni anahitaji kwenda nje kwa matibabu, akiendelea kukaa jela atakufa muda si mrefu" walisikika watetezi wake wakisema miaka kadhaa iliyopita.

Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu, ngozi nyeupe inatujua tulivyo na inatumia udhaifu wetu kutupiga, kuna mtu anaitwa Chavda, aliyoyafanya hapa miaka ya 90 si madogo, na hayupo tena, alitumia ujanjaujanja huohuo akatokomea na pesa nyingi ambazo hakuzitolea jasho hapa nchini.
 
kwamujibu wa makubaliano na serikali kuhakikisha debi linalipwa, bond yake ni mitambo ya IPTL
 
Sethi ni Mtanzania, mzaliwa wa Ruaha Iringa na ndio mwenye kampuni ya Ruaha Construction ya Kenya. Sethi ni tajiri mkubwa sana wa akili, hali na mali, hiyo IPTL, kile kiwanja tuu ni zaidi ya bilioni 30, bado majengo, bado mitambo. Hivyo akiwa huru, hiyo bilioni 26 japo amepewa mwaka mzima wa kulipa, lakini will make it within 6 months.

Hivyo usiwe na wasiwasi kabisa.

Kufuatia jina lako la pili, nilidhani badala ya kuandika kumhusu Sethi, nilidhani utaandika kumhusu ndugu yako JR, atendewe haki kwa kuachiwa bila masherti yoyote maana kiukweli hana kosa lolote na usikute ni karma ya mateso ya huyu mzee imechangia kumharakisha naniliu!

P
 
IPTL sio Mali yake ndugu Huyu jamaa nasikia alitoa shilingi 6m , akaruhusiwa kumilikai mahela ya Kwenye account ya escoro kimsingi hakuja na hela yote ya maana
Anazo hisa kwenye IPTL ?
 
Hakuna Pesa nyingine itakayotoka zaidi ya kuuza kile kiwanda kwa wanunuzi wa vyuma chakavu.
 
Dhamana si mitambo yake ya kufua umeme? Nilisikia kitu kama hicho
 
Ameiba nini mkuu? Huyu ni siasa tu. Kachukua hela ambayo mliyomuambia ni zake. Baada ya miaka miwili mnasema kaiba. Au unasahau ule ubishi wapinzani walisema ni hela ya serikali nyie mkasema ni za IPTL?

Sasa kanunua kampuni, kadraw hela zake , baada ya muda mnamgeuka mnasema kaiba!
 
Back
Top Bottom