Ni zamu ya konde boi kila kona... Si ki mashairi vina na midundo tena bali ziara za kuonesha ukwasi, kukubalika na ukaribu na mamlaka zenye nguvu...
Tunda limewiva sasa kila mtu analitaka... Mkulima keshasahaulika.... Nina machache kwakwe Konde boi
1. Kipaji adimu/adhimu.... Hili halina ubishi.. Kipaji kipo hasa cha utunzi wa nyimbo zinazogusa hisia... Na midundo inayohamasisha kucheza... Lakini daima mkumbuke aliyekushika mkono, aliyekulea, aliyekukuza... Aliyekutoa kusikojulikana mpaka leo upo hapo ulipo... Mheshimu sana huyu.... Ana mustakabali juu yako... Usikubali kamwe kutumika ukamkejeli kumtusi ama kumsema vibaya
2. Ni haki yako kuondoka WASAFI... kwa lugha nyingine tunasema mwana kakua... Na kama ni shule tunasema umehitimu.... Nenda kwa amani, aga kwa furaha... Shukuru kwa kila jambo... Kaanze maisha mapya kwa miguu yako mwenyewe na kwa kujiamini... Lakini kamwe usinyee kambi... Usiteme bazoka kwa njugu za kuonjeshwa...
Hao wanaokusifu na kukupamba leo ndio hao hao walikudhihaki na kukutema mate huku wakikumbia miaka mitatu tu iliyopita...
3. Punguza kuiga... Kuwa na ubunifu mpya.. Japo wanasema learn from the best lakini angalia unaiga nini.... Ili isionekane kama ni copy n paste.... Utajimaliza.... Hapa wanakusema na haya na mengine mengi
. Aliponunua V8 jipya ukajibu mapigo
. Ameanzisha FM radio nawe unataka kufanya hivyo...
. Alipoenda Tandale na kugawa misaada ukaenda kariakoo...
4. Ziepuke hila za wanasiasa... Wanakuona sasa kwakuwa kuna watu wamekupika na kuna hadhira ikakupokea.... Wanasiasa hawana marafiki wa kudumu bali wana maslahi ya kudumu.... Hadhira iliyokufikisha hapo haiko kwenye kundi la wanasiasa . ni fans wako toka imani tofauti, vyama tofauti, itikadi tofauti nknk... Usiikosee na kuipa kisogo ... Ikishajigawa kwa matendo yako... Mbele yako iko mashakani.... Wanasiasa wakutumie kwa faida huku ukibalance.. Epuka ahadi za uongo
5. Waangalie watu wanaokuzunguka sasa na kukusujudia... Wanafanya hivyo kwakuwa unacho cha kuwapa na wanafaidika na wewe... Punguza ziara zisizo na tija... Chagua ya kuongea... Angalia unaongea nini na nani na wapi... Usikubali kamwe kuchonganishwa na walezi wako....
6. Wewe ni msanii sio mwanasisa... Achana na hizi ziara... Rudi kajichimbie utoe vitu vipya vikali zaidi... Muda unaopoteza utakugharimu labda tu kama hutaki kurudi kwenye gemu kwa matumaini ya ahadi ya ubunge....
7. Kuna kitu kinaitwa asili... Asili pia ni shina ama ni chanzo... Una asili na WASAFI na Mondi... Kamwe usikubali kugombanishwa naye.. Nasema usikubali... Shina ni shina tuu... Wakati unasubiri kumalizana na WASAFI... Usirukeruke... Hawa wapambe kila kona wanakupoteza na kukupotosha pakubwa.....
Nitaendelea panapo majaliwa
Ndimi Jr fan wa kazi zako......