Harmonize: Nilipewa Mkataba wa kuonewa na WCB na nilisingiziwa kumroga Diamond Platnumz

Harmonize aache ushamba, anajiskiaje anavyongea kila siku lakini hajibiwi kitu na Mondi.
 

Ngoja Misukule yake iliyopewa tecno na bando ije kupinga.
 
Maskini wa akili hua watu wa ajabu sana, yaani mtu mwenye roho mbaya awafungulie dunia ya mafanikio kiasi kile wasanii wake?

Mwenye roho mbaya ni yule anawasign vijana alafu hawapi support ya kutosha akihofia wakikua kisanaa watamgeuka na mifano tunayo hapa hapa bongo.
 
Ngoja waje wale wenye zile team zisizoshiriki ligi yeyote uone povu lao.
 
Je mtu kusema yake ya moyoni ndio kigezo cha mziki kumshinda?

Sidhani kama uwezo wako wa kufikiri ndio umefikia kikomo na kufikia hilo hitimisho eti muziki umemshinda.
Bora uliomshinda kuliko sisi tunaowafatilia ya mastaa, tusio na jina mjini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…