Harmonize: Nilipewa Mkataba wa kuonewa na WCB na nilisingiziwa kumroga Diamond Platnumz

Harmonize: Nilipewa Mkataba wa kuonewa na WCB na nilisingiziwa kumroga Diamond Platnumz

Naomba kuweka wazi kabisa kwamba mimi si mpenzi wa Muziki wa Tanzania na wala siwapendi wanamuziki wa Tanzania , hii ni kwa vile wamekuwa mara zote wakitumika na CCM kuwapotosha wananchi , na hasa hawa wanaoitwa Wanamuziki wa kizazi kipya , ambao pia wanatuhumiwa kusafirisha na kusambaza madawa ya kulevya hivyo kuharibu nguvu kazi ya Taifa.

Bali nimesononeshwa sana na yaliyojitokeza kwenye mgogoro wa Harmonize na Diamond , pale huyo Harmonize alipokuwa anaomba kujitoa kwenye lebo ya WASAFI , mengi sana ameongea mwenyewe kila mtu kayasikia wala sina haja ya kuyarudia , bali nitagusia kidogo maeneo mawili tu.

Kwamba Diamond alimwambia Harmonize kwamba anaweza asimkamilishie kile anachotaka na wala hatomfanya chochote na kokote atakakoenda hatofanikiwa , kwa vile HAMUWEZI KISERIKALI , KIFEDHA NA KIUCHAWI , hii ni kauli ya kijinga sana kutolewa na anayeitwa msanii mkubwa , ni kauli ya kishamba sana iliyojaa Utanzania mtupu!

Jambo lingine linalotia aibu ni kitendo cha Harmonize Kuomba msaada kwa Magufuli moja kwa moja baada ya ngazi za chini ikiwemo wizara kumgwaya Diamond , Yaani Rais wa nchi ampigie simu Msela Diamond na kumbembeleza ili akubali kuterminate mkataba wa Harmonize na Wasafi ! hili ni jambo la kutia aibu sana , Yaani inawezekanaje Wizara na BASATA kutiwa mfukoni na msanii mmoja?

Haya mambo yakiachwa iko siku yatakuja kufedhesha mamlaka ya Rais , na sisi kama wananchi hatutakubali.
 
Halafu hyo no 7 ndo ukweli mtupu,jamaa alilazimisha sana kukaa kwenye nyimbo ya "KWANGWARU" ilitakiwa akae davido lkn kijana wa tandale akatumia uboss wake kukaa kwenye ngoma kinguvu[emoji12]
 
Naomba kuweka wazi kabisa kwamba mimi si mpenzi wa Muziki wa Tanzania na wala siwapendi wanamuziki wa Tanzania , hii ni kwa vile wamekuwa mara zote wakitumika na ccm kuwapotosha wananchi , na hasa hawa wanaoitwa Wanamuziki wa kizazi kipya , ambao pia wanatuhumiwa kusafirisha na kusambaza madawa ya kulevya hivyo kuharibu nguvu kazi ya Taifa .
Yatakuja au tayari yamelifedhehesha taifa! Yaani Rais wa nchi awabembelezee wasanii! Sishangai kwani Rais alimvika kofia msanii! Nikamkumbuka yule mama aliyemfunga kamba za viatu mwanae ikulu mbele ya Rais.
 
Watu unaowasaidia wengi hugeuka Maadui [emoji855]

Huyu Harmonize Ndio alilia Kwa Suprise ya Mond pale Dar Live

Halafu hii siku Diamond alipiga Ndege Wawili Kwa Jiwe Moja Alienda Kwa Davido

Baadae Akaenda kumsupport harmonize na Dogo Mpaka Machozi yalimtoka

Leo WCB wamekuwa Wabaya [emoji2297]
HARMONIZE ALIKUWA NA KIPAJI DIAMOND ALIKUWA PESA.

THAT'S HOW CAPITALIST WORLD WORK
 
Hivi harmo alivyotoka wasafi si diamond aliendelea kumsuport tena akawa anapiga ngoma zake kwenye media? Harmo alivyoanza kumtumia hbaba sijui mwijaku kumtukana diamond ndo mambo yalipoharibika sasa diamond kujibu mapiga anaonekana mbaya?
Tafuta kazi ya maana ikuingizie pesa Diamond na Harmonize hawakusaidii chochote na hawakujui
 
Back
Top Bottom