Naomba kuweka wazi kabisa kwamba mimi si mpenzi wa Muziki wa Tanzania na wala siwapendi wanamuziki wa Tanzania , hii ni kwa vile wamekuwa mara zote wakitumika na CCM kuwapotosha wananchi , na hasa hawa wanaoitwa Wanamuziki wa kizazi kipya , ambao pia wanatuhumiwa kusafirisha na kusambaza madawa ya kulevya hivyo kuharibu nguvu kazi ya Taifa.
Bali nimesononeshwa sana na yaliyojitokeza kwenye mgogoro wa Harmonize na Diamond , pale huyo Harmonize alipokuwa anaomba kujitoa kwenye lebo ya WASAFI , mengi sana ameongea mwenyewe kila mtu kayasikia wala sina haja ya kuyarudia , bali nitagusia kidogo maeneo mawili tu.
Kwamba Diamond alimwambia Harmonize kwamba anaweza asimkamilishie kile anachotaka na wala hatomfanya chochote na kokote atakakoenda hatofanikiwa , kwa vile HAMUWEZI KISERIKALI , KIFEDHA NA KIUCHAWI , hii ni kauli ya kijinga sana kutolewa na anayeitwa msanii mkubwa , ni kauli ya kishamba sana iliyojaa Utanzania mtupu!
Jambo lingine linalotia aibu ni kitendo cha Harmonize Kuomba msaada kwa Magufuli moja kwa moja baada ya ngazi za chini ikiwemo wizara kumgwaya Diamond , Yaani Rais wa nchi ampigie simu Msela Diamond na kumbembeleza ili akubali kuterminate mkataba wa Harmonize na Wasafi ! hili ni jambo la kutia aibu sana , Yaani inawezekanaje Wizara na BASATA kutiwa mfukoni na msanii mmoja?
Haya mambo yakiachwa iko siku yatakuja kufedhesha mamlaka ya Rais , na sisi kama wananchi hatutakubali.