Harmonize: Nilipewa Mkataba wa kuonewa na WCB na nilisingiziwa kumroga Diamond Platnumz

Harmonize: Nilipewa Mkataba wa kuonewa na WCB na nilisingiziwa kumroga Diamond Platnumz

Naomba kuweka wazi kabisa kwamba mimi si mpenzi wa Muziki wa Tanzania na wala siwapendi wanamuziki wa Tanzania , hii ni kwa vile wamekuwa mara zote wakitumika na ccm kuwapotosha wananchi , na hasa hawa wanaoitwa Wanamuziki wa kizazi kipya , ambao pia wanatuhumiwa kusafirisha na kusambaza madawa ya kulevya hivyo kuharibu nguvu kazi ya Taifa .
Serikali ina mengi ya maana kuliko misutano ya wanaume wa dar wawili walioamua kuanikana hadharani
 
Diamond kashazoea sasa kuabudiwa na chawa wake sasa anataka kila mtu awe chawa kwake, wakati mtu kama yeye kwasasa alipaswa awe mtu wa maneno machache alafu vitendo ndo viongee, haya mambo ya kutaka taka fadhila kwa aliowasaidia ni too low for him haimpunguzii chochote katika mafanikio yake.
 
Huyu dogo anakaza sana tangu atoke huko kwa yale mameneja majizi.
Hajawahi kupotea maskioni mwa watu

NB:mnyakyusa kaenda kupiga goti saivi 😀
 
Diamond kashazoea sasa kuabudiwa na chawa wake sasa anataka kila mtu awe chawa kwake, wakati mtu kama yeye kwasasa alipaswa awe mtu wa maneno machache alafu vitendo ndo viongee, haya mambo ya kutaka taka fadhila kwa aliowasaidia ni too low for him haimpunguzii chochote katika mafanikio yake
Sema dogo anaroho ya kishetani sana
 
Kiukweli Diamond Platnumz amepigana vita nyingi sana mpaka sasa kiasi kwamba amekuwa nunda.

Ukitaka ushindane na Diamond usitie huruma maana unapoteza pambano kirahisi sana.
Kwa mmakonde vita hatoiweza,wengi wanamgwaya lkn mmakonde anaonesha dhahiri yupo tayar kwa lolote kivyovyote na ndo maana,Diamond na WCB yake hata wafanyaje dogo jeshi ataendelea kuwepo labda wamtoe uhai kabisa
 
mimi sio mfuatiliaji sana wa muziki wa kisasa lakini napenda Muziki mzuri, kwa ninavona konde anafanya vizuri tu hivo nashangaa humu anasemwa muziki umemshinda wakati mtaani na clubs unapigwa
 
Mziki bongo umekuwa kiki,unaweza kukuta Konde anatafuta kiki tu ingawa mziki wa sasa hivi kiki zimezidi mara wanaume wavae nguo za kike ,Hatukatai kwenye mziki kuna figisu ila mbona Alikiba ameweza mziki bila kiki? Kwa mwaka anaweza akatupa dongo mara moja ,hata Baba levo alisema Harmonize hasumbui ila Kiba ndo anawapaga wakati mgumu
 
mimi sio mfuatiliaji sana wa muziki wa kisasa lakini napenda Muziki mzuri, kwa ninavona konde anafanya vizuri tu hivo nashangaa humu anasemwa muziki umemshinda wakati mtaani na clubs unapigwa
Mziki wake unapigwa sana ,mfano amapiano zote ni hits tatizo yeye anafanya kwa mashindano
 
Back
Top Bottom