Harmonize: Nilipewa Mkataba wa kuonewa na WCB na nilisingiziwa kumroga Diamond Platnumz

Harmonize: Nilipewa Mkataba wa kuonewa na WCB na nilisingiziwa kumroga Diamond Platnumz

Aiseee!!! Inaumiza sana yaani ishu ya contract termination mpaka Rais aingilie kati, Diamond siyo mtu mzuri, kwanza angalia alivyo mkataa baba yake mzazi, angalia hizi za harmonize, na bado hatujui yaliyo chini ya kapeti huko.

Nchi ngumu sana hii.
 
Magufuri ameondoka tutajua ccm ina nguvu kiasi gani hapo 2025. Tuliokuwa upande wa Magufuri na si ccm tutajulikana hadharani tutaonyesha nguvu yetu
 
Diamond na ushirikina ni Kama chanda na Pete

Hata huyo Harmonize

Kimsingi wasanii wote unaowajua bongo fleva na bongo movies washirikina kishenzi

Wananuka matunguli

Wengine wamepikwa kwenye vyungu

Huwezi amini hata hao wanaojifanya smart and classy ni wazee wa vilinge Kama kawa.

Labda wale wa hip hop Ila nao kuna wazee wa matunguli Kama kawa
 
Hivi harmo alivyotoka wasafi si diamond aliendelea kumsuport tena akawa anapiga ngoma zake kwenye media? Harmo alivyoanza kumtumia hbaba sijui mwijaku kumtukana diamond ndo mambo yalipoharibika sasa diamond kujibu mapiga anaonekana mbaya?
Chawa kila comment unadakia ,duuh haya tumekuelewa mama tiffah
 
HARMONIZE NDIO ALIKUWA ANAINYONYA WCB SABABU,KITENDO CHA KUPEWA 40% WAKATI PALE LEBO INATAKIWA IJIENDESHE NI UNYONYAJI, ILIPE KODI MBALIMBALI,ILIPE WAFANYAKAZI,IBOLESHE VIFAA VYA STUDIO,MALADHI KWA WASANII WAKE WAKATI WA KUSHOOT,KUENDESHA TAMASHA LAO, NA NK ,
MJADALA UISHE,
 
Nimemkubali na nitaendelea kumkubali Harmonize kwa hili la kuvunja mkataba kwa amani tu yaani kalipa milion 600. Kuna msanii gani hapa Tz mwenye ubavu kama wa kufanya jambo hili bila kuteteleka kiuchumi?

Big up Harmonize kwa kujiajiri, sasa hivi unapata 100% ya jasho lako kuliko kuendelea kukatwa tozo ya 60% ya mapato kwakweli inaumiza sana
 
Diamond anatakiwa ayatolee ufafanuz haya malalamiko , Harmonize anamtuhumu Diamond kwamba kuna watu anawatuma wamchafue notable Baba levo na Juma lokole , ili kumharibu kimziki yes yawezekana ni kweli , Ila harmonize haangalii Kwa upande wake kuwa na yeye ana chawa akina mwijaku , carlmastory, hbaba , jaymaudaku na wengine weng na wao kazi Yao ni kumwandama diamond , lakini pia Wasafi wakiandaa event yeye harmonize na yeye anaandaa ili kudivert attention ... Means na yeye anaishi na kuamini humo humo kwenye Fitina na figisu , anamponda mond kwa madhaifu yake hata hvyo bado anamtegemea mond indirect ili awin, ...... Tatizo linakuja hafikii peak Ile anayotaka sababu mwenzake kaenda mile nyingi mbele na ana nguvu nyingi zaidi ndo chanzo cha malalamiko hayo yote.

Turudi Kwa Maghufuli , mtoa mada kuna kitu umekiruka au umekificha Kwa maksudi ili
ujumbe wako wenye utata na kisiasa ufike , mpak kusema Jiwe alimbembeleza Diamond kitu ambacho Kwa Maelezo ya harmonize sio kweli ...

Harmonize anadai alifanya kila njia kuwaomba watu wenye nguvu ya kimaamuz ili wamsaidie azma yake ya kuvunja mkataba , kwani by that time kwake ilikuwa ni ngumu hata kumfikia Diamond Kwa jinsi mambo yalivyokuwa yana-turn around...

Aliwafikia watu kama kusaga ( sababu ya status yake na ushkaji na mond ), alimfikia mama dangote (nguvu ya mama) alimfikia mwenyekiti sjui ndo katibu wa Basata, na alimfikia mwakiyembe ( by that time Wazir wa Sanaa ) , Kwa Maelezo yake anadai wote hawakuonyesha kumsaidia na inaonekana hawakuwa tayar , huku akiandamwa na pressure toka Kwa wadhamini wake CRDB na Sayona , Kondeboy aliona kete Yake ya mwisho ni Raisi John Pombe Joseph Maghufuli....

Jiwe alifanya sehemu yake Kwa kumpigia simu Wazir wa Sanaa na michezo kuhusu hlo sakata,na nafk Mwakiyembe alikuwa aware na hyo changamoto thus why alifanya maamuz ya haraka , kumzuia diamond kukwea pipa mpak amalize hlo suala ...

Kwa hyo Siyo kwamba Maghufuli alimbembeleza Diamond ...na kama ingekuwa hvyo ingechukua sku mbili au tatu ...

Zaidi ya yote Kongole Kwa Harmonize Kwa upambanaji na roho ya kiume , kuhusu Fitina hata yeye hzo Fitina anazifanya , ushindi wake sio wa haraka kama anavyofkria sababu mwenzake still bado ni ngome imara ...!!
Daah leo umeongea kiume Sana ,hizi ndio nondo za kiume Sasa hujaegemea upande ,kongole Sana mwamba
 
1.pesa ya kuvunja mkataba ilitolewa na sayona crdb bank na jembe ni jembe sio kama tulivyoaminishwa kuwa sarah alihusika
2.diamondi ni mtu mwenye roho mbaya sana rejea kauli za ommy dimpoz,belle 9 ,shettah rich
Naunga mkono huu uzi 100%
 
Back
Top Bottom