Harmonize ameonesha Akili Ya Waajiriwa Wengi Tanzania Ilivyo. [emoji28][emoji28][emoji28] Tungepata Hata Siku 7 kuwaona wenzetu walioendelea Namna Gani wanaheshimu Kazi, na Kuheshimu Maboss zao, Leo Harmonize asingeongea kama Anavyo ongea.
Kuna Kitu Kinaitwa Kampuni. Ikisha Kuwa Kampuni basi hata muajiriwa Fikra zako inabidi zianze kubadirika. Walio Ajiriwa kwenye Serious Companies Watakuwa naelewa nacho Sema.
Harmonize Alikuwa Msanii wa Kwanza kabisa Kuwa chini Ya WCB, huenda Wakati Diamond Anamchukua Harmonize Hakuwa na Mawazo ya kuja na Wasanii wengi na Kuwaendeleza wengi zaidi. So alimchukua kama Mtu anayetaka kumsaidia, lakini baada ya Kuingia WCB na Diamond anakuwa kiakili anakutaka na watu, Ndipo Mawazo ya kuwa na Kampuni itakayo kuwa Inamamia wasanii ikazidi kunoga, Hapo ni Lazima Diamond Akili ilianza kubadirika na kuanza kufikiria kama CEO na Sio Kama Diamond. Sasa Harmonize Alitakiwa Naye kuanza kubadirisha Fikra kuwa Sasa nipo chini ya Kampuni na Sio nipo Chini ya Mtu fulani. Angekubali hilo haya yote yasingetokea.
Kwanini Harmonize Anashindwa Kujiuliza hata Mh Rais alivyompigia simu Aliagiza Termination contract iwe signed na Sio Millioni 600 zirudi? Ina maana alielewa mikata ya Kampuni inavyo fanya kazi! Leo atalia na hizo millioni 600 lakini no one ambaye atakuja kusema kuwa hizi millioni 600 hukupaswa kulipa.
Harmonize ananikumbusha Aina ya Waajiriwa ambao wanafanyiwa Interview, anauliza Ungependa Tukulipe Sh ngapi kwa Mwezi anasema Mimi hela yoyote tuu mtakayo ona inafaa nitalipwa. Anaulizwa zaidi ya Mara 3 thamani yako ni Tsh ngapi katika kazi hii, Hataki kusema. Akisha Ajiriwa na Kupewa mkataba akaizoea Kampuni Anaanza kusema Huu mshahara ni mdogo sana na Haunitoshi, lakini kumbuka Umesha Sign mkataba. The same na Harmonize leo anakuja Kulia Na asilimia 60% kwa 40% huenda kweli ni ndogo, lakini kama ulikuwa unajiamini kuwa ipo siku utakuwa Juu, kwanini hukusema mwanzo? Kwanini hukuomba Vipengele vya mkataba Viseme kuwa kwasababu wewe ni msanii na unakua kila kitu, basi kuwe na kipengele cha ku review mkataba wako kila baada ya miezi 6 au Mwaka 1. Hakufikiria kwasababu akili yake ilimezwa kuwa BSS wamenikataa, huyu amenichukua. Hapa ndio Dhana ya Kuwa KUSOMA SHULE NI MUHIMU, Angekuwa Alisoma Suala la Mikataba angejua nini cha kufanya.
Sometime CEO anaweza kuwa Rafiki yako, na jana mmekunywa naye Bia ila kesho ukitaka kwenda Kumuona Ofisini anakwambia Nitumie Email au weka Appointment! Walio ajiriwa hili wanalijua sanaa, The same kwa Diamond Kuna Muda atasimama kama Diamond na kuna muda Atasimama kama CEO, Raisi Akiwa Kwenye Shughuli za kichama, basi wanachama ni rahisi kumuona na kumu access lakini akisimama kama Rais wa Nchi utaona kama Mambo yamebadirika.
Diamond Tunasema Alimsaidia Harmonize kwasababu alitake risk, Aliwekeza Pesa Bila Kujua kama Wananchi watampokea msanii au hawata mpokea, Sahizi Tunasema Harmonize alionewa kwasababu tunaona amesha Kuwa Star, Fikiria Hela Alizowekeza Diamond Kwa Hamornize Halafu, Mashabiki wasinge mpokea Diamond angekuwa Ametengeneza Hasara Kiasi gani? Tunarudi kule kule kwenye Kampuni, ukiwa Unaomba Msaada wa kuanzisha Kampuni na Unataka mtu aweke pesa zake, ni lazima Uandike proposal useme utafanya nini? , utapataje faida na Utarudisha Vipi Mtaji! Wakague ndio upate pesa. Lakini Diamond alimchukua jamaa, akawekeza pesa, bila kujari kama itakuwaje mbele. Sasa Tumuulize Harmonize kwa Jinsi vile alivyo imba BSS nani Angemchukua kama Msanii wake? Diamond alithubutu.
Ufike wakati wasanii wa Bongo waache kuvimba, watafute wanasheria wafundishwe sheria, mikataba na Vitu vingine, Shule ni Muhimu. Yule CEO wa Facebook, Whatsapp na Instagram. Kuna Programmer hawalali kuhakikisha Kila kitu kinaenda, kuna IT wanaipambania Kampuni, lakini CEO anaonekana Kawasaidia kuwapa Ajira na Yeye ndie anaye tajwa duaniani kuwa ni Tajiri sio wewe IT ambaye hulali [emoji28]