Harmonize: Nilipewa Mkataba wa kuonewa na WCB na nilisingiziwa kumroga Diamond Platnumz

Harmonize: Nilipewa Mkataba wa kuonewa na WCB na nilisingiziwa kumroga Diamond Platnumz

Uzi kwa ajili ya Diamond Platnumz.

Jina lenyewe ukilitamka linatisha.

Jina limewapa rizki vijana wa kutosha.

Bila ili jina hutoboi hapa mjini.
Hivi ni kweli alitoka na bodaboda kutoka airport hadi basata?
 
Naomba kuweka wazi kabisa kwamba mimi si mpenzi wa Muziki wa Tanzania na wala siwapendi wanamuziki wa Tanzania , hii ni kwa vile wamekuwa mara zote wakitumika na ccm kuwapotosha wananchi , na hasa hawa wanaoitwa Wanamuziki wa kizazi kipya , ambao pia wanatuhumiwa
Rais mpiga push up,mwenye kauli za kufedhehesha naye mazi ga Nyanza.
 
Ila hamo Na diamond wakiimba nyimbo pamoja zinakuwaga balaa
Sipendi watu ambao wanapenda kunyenyekewa
Mtu ashawalipa m600 bado mnamtakia nini??
Yaan mtu akae chini yako tu wamuache harmonize bana
Lini ulimsikia diamond anasema anataka kunyenyekewa zaidi ya kumsikia harmonize
 
Hapana wcb walianza bana kumsakama
Hamo mstasrabu sanaa
Harmonize anaustaharabu upi huyu si alitengeneza video ndani ya hiyo video akaweka mtu anayefanana na diamond akaandika mstari boss akipata demu anatangaza lakini huyo alivyotoka Wasafi akaanza kutunga nyimbo za vijembe kwa diamond kuna wimbo unaitwa haunistui n.k dada inaonesha sio mfuatiliaji wa mziki.
 
Kama umefuatilia vyema interview yote, utabaini hakuwa na nia ya kuzungumza alicho zungumza, ndio sababu ameweka wazi ni mara ya kwanza kuzungumza kwa kina alichozungumza kuhusu kuondoka kwake wcb na maswala mengine tusiyokuwa tunafahamu.
Usichokijua ni kwamba tukio lile liliandaliwa na waandishi walimsubiri wakijua nini kitatokea
 
anacholaumiwa domo ni makasiriko yake juu ya mtu ambaye anataka kujinasua kwa gharama yoyote kutoka kwenye mikono ya unyonyaji,kwanini uchukie mtu anayepambania uhuru wake?

milioni 600 zishafuta utu wote wa domo amuache kijana na maisha yake makasiriko yatawafokisha pabaya kwasababu hata mmakonde anaonekana haya mambo sasa sio ya kumuachia Mungu ni ya kupambana nayo kiume kwa kiume,ndo maana yamefikia hapa.
Kwani 600m harmo alilipishwa na WCB au na diamond na huo mkataba unamhusu vp mond?
 
Usichokijua ni kwamba tukio lile liliandaliwa na waandishi walimsubiri wakijua nini kitatokea
- Sio kweli kwamba nilikuwa sijui
- Mjini mipango,
- Wasanii kama content ya hizi (social) media, wanajua nini cha kufanya, hutoa taarifa mapema ili waandishi wawepo eneo la tukio.
- Waandishi/wapiga picha ni sehemu muhimu sana tena sana katika tasnia nzima ya sanaa (ya muziki na maigizo)

- Yeye harmo anatambua umuhimu wao ndio sababu aliwapa ratiba ya kurejea kwake nchini.
 
Haya mambo yalitokea miaka miwili nyumaa
Now Mmakonde yupo huru ana lebel yake na kasaini wasanii kibao

Kwa muda huu nilitegemea kumuona Mmakonde kwenye level zingine kabisa kama anadhani alikua anabanwa Usafini

Wasanii wake wamedumaa labda Ibra kidogo, Album imedorora kabisa sio kama ile ya mwanzo
Hali ya uchumi imekua mtihani Komde gang....... haya ndio mambo Mmakonde anapaswa ku deal nayo na sio kubaki ulalia lia kila siku Wasafi walinionea

Wasafi hwajamuondolea sauti wala akili lakini sasa hadi mademu zake yeye analia na wasafi
Kutwa kuimba vijembe kwa wasafi

Move on kijana
Unapoteza muda kutaka watu wakuonee huruma na kumuona Mondi mbaya
 
Wy





Mwanamuziki wa kizazi kipya, Harmonize afunguka kuhusu mkataba alioingia na WCB amesema alikuwa akipewa 40% ya mapato yoyote anayoingiza na WCB kuchukua 60% ameamua kuelezea hayo yote kutokana na watu kuwa dhana ya kwamba yeye ni msaliti. Amesema alifanyiwa fitna nyingi zilizopelekea yeye kuondoka kwenye record label hiyo.

Amesema management nzima ya WCB walikuwa wanamuogopa yeye (Harmonize) kwamba anaelekea kumshinda Diamond Platnumz kimuziki, amenongezea pia baba yake Harmonize alivyokuwa akija kumtembelea nyumbani WCB walikuwa wanasema kwamba alikuwa anakwenda kumroga Diamond.

Harmonize ameongezea pia alikwenda Nigeria kwa gharama zake kufanya collabo na Reekado Banks nchini Nigeria na akakatwa dola 5000 na WCB. Alipoona fitna zimezidi alijaribu kutafuta amani lakini ilishindikana, amesema mkataba wake na WCB alishauriwa na Joseph Kusaga kwamba akitafuta mwanasheria asingelipa chochote lakini hakutaka kupambana kwa njia hiyo na akaamua kulipa hela tu (Milioni 600) ili tu kupata amani.

Why now!!!
Au ndio kiki na kutafuta sympathy/huruma Ili muziki wake ununuliwe sana?
 
Harmo kaona urejeo wake bongo umekuwa kimya hakuna wa kumpokea akaona kupata attention ya hvyo itamsave
Yani kijeba mseleleko wake ni Diamond, akitaka kuongelewa basi anataja jina Diamond anaendelea kusavaiv kwenye muziki.
 
Diamond asidanganye lolote kuhusu serikali hawez kuiweka mfukoni. Serikali ya tanzania as idharirishe kiwango hk. kifedha pia Hana hela za kutisha, kiuchawi labda huo wa kumlala mama yake.... Ndio maana Zai akaona tusitoane roho na mama mkwe kisa........

[emoji15][emoji15]
 
Angekua peke yake kwenye kampen na kuvalishwa kofia hapo ungeleta uchawa haswa na watu wakakuelewa ila hakua msanii peke take kwenye kampeni zile. Hata konde ,kiba ni marais kwenye gang zao
Usibeze anavyotegemewa kujaza watu kwenye mikutano ya kampeni, kuhusu Urais…. tayari ni Rais wa WASAFI.
 
Haya mambo yalitokea miaka miwili nyumaa
Now Mmakonde yupo huru ana lebel yake na kasaini wasanii kibao

Jikite kwenye hoja za Konde kama una ukomavu wa kujibu, hakuna sehemu amelialia bali amechoka kusakamwa like hana fadhira na hana baraka za Wasafi…. hoja zina ukweli au porojo?
 
Harmonize ameonesha Akili Ya Waajiriwa Wengi Tanzania Ilivyo. [emoji28][emoji28][emoji28] Tungepata Hata Siku 7 kuwaona wenzetu walioendelea Namna Gani wanaheshimu Kazi, na Kuheshimu Maboss zao, Leo Harmonize asingeongea kama Anavyo ongea.

Kuna Kitu Kinaitwa Kampuni. Ikisha Kuwa Kampuni basi hata muajiriwa Fikra zako inabidi zianze kubadirika. Walio Ajiriwa kwenye Serious Companies Watakuwa naelewa nacho Sema.

Harmonize Alikuwa Msanii wa Kwanza kabisa Kuwa chini Ya WCB, huenda Wakati Diamond Anamchukua Harmonize Hakuwa na Mawazo ya kuja na Wasanii wengi na Kuwaendeleza wengi zaidi. So alimchukua kama Mtu anayetaka kumsaidia, lakini baada ya Kuingia WCB na Diamond anakuwa kiakili anakutaka na watu, Ndipo Mawazo ya kuwa na Kampuni itakayo kuwa Inamamia wasanii ikazidi kunoga, Hapo ni Lazima Diamond Akili ilianza kubadirika na kuanza kufikiria kama CEO na Sio Kama Diamond. Sasa Harmonize Alitakiwa Naye kuanza kubadirisha Fikra kuwa Sasa nipo chini ya Kampuni na Sio nipo Chini ya Mtu fulani. Angekubali hilo haya yote yasingetokea.

Kwanini Harmonize Anashindwa Kujiuliza hata Mh Rais alivyompigia simu Aliagiza Termination contract iwe signed na Sio Millioni 600 zirudi? Ina maana alielewa mikata ya Kampuni inavyo fanya kazi! Leo atalia na hizo millioni 600 lakini no one ambaye atakuja kusema kuwa hizi millioni 600 hukupaswa kulipa.

Harmonize ananikumbusha Aina ya Waajiriwa ambao wanafanyiwa Interview, anauliza Ungependa Tukulipe Sh ngapi kwa Mwezi anasema Mimi hela yoyote tuu mtakayo ona inafaa nitalipwa. Anaulizwa zaidi ya Mara 3 thamani yako ni Tsh ngapi katika kazi hii, Hataki kusema. Akisha Ajiriwa na Kupewa mkataba akaizoea Kampuni Anaanza kusema Huu mshahara ni mdogo sana na Haunitoshi, lakini kumbuka Umesha Sign mkataba. The same na Harmonize leo anakuja Kulia Na asilimia 60% kwa 40% huenda kweli ni ndogo, lakini kama ulikuwa unajiamini kuwa ipo siku utakuwa Juu, kwanini hukusema mwanzo? Kwanini hukuomba Vipengele vya mkataba Viseme kuwa kwasababu wewe ni msanii na unakua kila kitu, basi kuwe na kipengele cha ku review mkataba wako kila baada ya miezi 6 au Mwaka 1. Hakufikiria kwasababu akili yake ilimezwa kuwa BSS wamenikataa, huyu amenichukua. Hapa ndio Dhana ya Kuwa KUSOMA SHULE NI MUHIMU, Angekuwa Alisoma Suala la Mikataba angejua nini cha kufanya.

Sometime CEO anaweza kuwa Rafiki yako, na jana mmekunywa naye Bia ila kesho ukitaka kwenda Kumuona Ofisini anakwambia Nitumie Email au weka Appointment! Walio ajiriwa hili wanalijua sanaa, The same kwa Diamond Kuna Muda atasimama kama Diamond na kuna muda Atasimama kama CEO, Raisi Akiwa Kwenye Shughuli za kichama, basi wanachama ni rahisi kumuona na kumu access lakini akisimama kama Rais wa Nchi utaona kama Mambo yamebadirika.

Diamond Tunasema Alimsaidia Harmonize kwasababu alitake risk, Aliwekeza Pesa Bila Kujua kama Wananchi watampokea msanii au hawata mpokea, Sahizi Tunasema Harmonize alionewa kwasababu tunaona amesha Kuwa Star, Fikiria Hela Alizowekeza Diamond Kwa Hamornize Halafu, Mashabiki wasinge mpokea Diamond angekuwa Ametengeneza Hasara Kiasi gani? Tunarudi kule kule kwenye Kampuni, ukiwa Unaomba Msaada wa kuanzisha Kampuni na Unataka mtu aweke pesa zake, ni lazima Uandike proposal useme utafanya nini? , utapataje faida na Utarudisha Vipi Mtaji! Wakague ndio upate pesa. Lakini Diamond alimchukua jamaa, akawekeza pesa, bila kujari kama itakuwaje mbele. Sasa Tumuulize Harmonize kwa Jinsi vile alivyo imba BSS nani Angemchukua kama Msanii wake? Diamond alithubutu.

Ufike wakati wasanii wa Bongo waache kuvimba, watafute wanasheria wafundishwe sheria, mikataba na Vitu vingine, Shule ni Muhimu. Yule CEO wa Facebook, Whatsapp na Instagram. Kuna Programmer hawalali kuhakikisha Kila kitu kinaenda, kuna IT wanaipambania Kampuni, lakini CEO anaonekana Kawasaidia kuwapa Ajira na Yeye ndie anaye tajwa duaniani kuwa ni Tajiri sio wewe IT ambaye hulali [emoji28]
 
Back
Top Bottom