Black Sniper
JF-Expert Member
- Dec 10, 2013
- 32,406
- 55,148
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivi H baba unampaje tuzo ya mbao harmomaviSawa baba levo
Harmonize ameonesha Akili Ya Waajiriwa Wengi Tanzania Ilivyo. [emoji28][emoji28][emoji28] Tungepata Hata Siku 7 kuwaona wenzetu walioendelea Namna Gani wanaheshimu Kazi, na Kuheshimu Maboss zao, Leo Harmonize asingeongea kama Anavyo ongea.
Kuna Kitu Kinaitwa Kampuni. Ikisha Kuwa Kampuni basi hata muajiriwa Fikra zako inabidi zianze kubadirika. Walio Ajiriwa kwenye Serious Companies Watakuwa naelewa nacho Sema.
Harmonize Alikuwa Msanii wa Kwanza kabisa Kuwa chini Ya WCB, huenda Wakati Diamond Anamchukua Harmonize Hakuwa na Mawazo ya kuja na Wasanii wengi na Kuwaendeleza wengi zaidi. So alimchukua kama Mtu anayetaka kumsaidia, lakini baada ya Kuingia WCB na Diamond anakuwa kiakili anakutaka na watu, Ndipo Mawazo ya kuwa na Kampuni itakayo kuwa Inamamia wasanii ikazidi kunoga, Hapo ni Lazima Diamond Akili ilianza kubadirika na kuanza kufikiria kama CEO na Sio Kama Diamond. Sasa Harmonize Alitakiwa Naye kuanza kubadirisha Fikra kuwa Sasa nipo chini ya Kampuni na Sio nipo Chini ya Mtu fulani. Angekubali hilo haya yote yasingetokea.
Kwanini Harmonize Anashindwa Kujiuliza hata Mh Rais alivyompigia simu Aliagiza Termination contract iwe signed na Sio Millioni 600 zirudi? Ina maana alielewa mikata ya Kampuni inavyo fanya kazi! Leo atalia na hizo millioni 600 lakini no one ambaye atakuja kusema kuwa hizi millioni 600 hukupaswa kulipa.
Harmonize ananikumbusha Aina ya Waajiriwa ambao wanafanyiwa Interview, anauliza Ungependa Tukulipe Sh ngapi kwa Mwezi anasema Mimi hela yoyote tuu mtakayo ona inafaa nitalipwa. Anaulizwa zaidi ya Mara 3 thamani yako ni Tsh ngapi katika kazi hii, Hataki kusema. Akisha Ajiriwa na Kupewa mkataba akaizoea Kampuni Anaanza kusema Huu mshahara ni mdogo sana na Haunitoshi, lakini kumbuka Umesha Sign mkataba. The same na Harmonize leo anakuja Kulia Na asilimia 60% kwa 40% huenda kweli ni ndogo, lakini kama ulikuwa unajiamini kuwa ipo siku utakuwa Juu, kwanini hukusema mwanzo? Kwanini hukuomba Vipengele vya mkataba Viseme kuwa kwasababu wewe ni msanii na unakua kila kitu, basi kuwe na kipengele cha ku review mkataba wako kila baada ya miezi 6 au Mwaka 1. Hakufikiria kwasababu akili yake ilimezwa kuwa BSS wamenikataa, huyu amenichukua. Hapa ndio Dhana ya Kuwa KUSOMA SHULE NI MUHIMU, Angekuwa Alisoma Suala la Mikataba angejua nini cha kufanya.
Sometime CEO anaweza kuwa Rafiki yako, na jana mmekunywa naye Bia ila kesho ukitaka kwenda Kumuona Ofisini anakwambia Nitumie Email au weka Appointment! Walio ajiriwa hili wanalijua sanaa, The same kwa Diamond Kuna Muda atasimama kama Diamond na kuna muda Atasimama kama CEO, Raisi Akiwa Kwenye Shughuli za kichama, basi wanachama ni rahisi kumuona na kumu access lakini akisimama kama Rais wa Nchi utaona kama Mambo yamebadirika.
Diamond Tunasema Alimsaidia Harmonize kwasababu alitake risk, Aliwekeza Pesa Bila Kujua kama Wananchi watampokea msanii au hawata mpokea, Sahizi Tunasema Harmonize alionewa kwasababu tunaona amesha Kuwa Star, Fikiria Hela Alizowekeza Diamond Kwa Hamornize Halafu, Mashabiki wasinge mpokea Diamond angekuwa Ametengeneza Hasara Kiasi gani? Tunarudi kule kule kwenye Kampuni, ukiwa Unaomba Msaada wa kuanzisha Kampuni na Unataka mtu aweke pesa zake, ni lazima Uandike proposal useme utafanya nini? , utapataje faida na Utarudisha Vipi Mtaji! Wakague ndio upate pesa. Lakini Diamond alimchukua jamaa, akawekeza pesa, bila kujari kama itakuwaje mbele. Sasa Tumuulize Harmonize kwa Jinsi vile alivyo imba BSS nani Angemchukua kama Msanii wake? Diamond alithubutu.
Ufike wakati wasanii wa Bongo waache kuvimba, watafute wanasheria wafundishwe sheria, mikataba na Vitu vingine, Shule ni Muhimu. Yule CEO wa Facebook, Whatsapp na Instagram. Kuna Programmer hawalali kuhakikisha Kila kitu kinaenda, kuna IT wanaipambania Kampuni, lakini CEO anaonekana Kawasaidia kuwapa Ajira na Yeye ndie anaye tajwa duaniani kuwa ni Tajiri sio wewe IT ambaye hulali [emoji28]
Hahaha...siku huyo mwanajeshi wenu akimzidi Naseeb kwa chochote kile (hâta kimoja tu) nitawaelewa,ila kwasasa nawaona kama wafa maji tu maana hakuna hâta hoja moja ya maana mnayotoa.
Siku ambayo Diamond atakuwa ameshuka, hakutakuwa na mjadala wowote kuhusu DIAMOND tutakuwa busy na mtu mwingine kabisa mwenye wakati wake.Ila lazima tukubali kila kitu kina kushuka, asipojiweka vizuri atakumbuka
Natamani sana hili litokee, naona linachelewa kutokea aiseee. Wacha waaibishweHaya mambo yakiachwa iko siku yatakuja kufedhesha mamlaka ya Rais , na sisi kama wananchi hatutakubali.
Kwa lipi yaani, lete dataRayvanny kwa harmonize haingii hata ukucha usimfananishe harmonize na upumbavu
Diamond kashinda vita dhidi ya shujaa muongoza njia, kitu gani mmakonde wa Chitoholi?
Wanaomchukia Diamond ni walewale miaka nenda Rudi,Zaid Zaid wanahamishaga kambi tu.
Huyo mange mwenyewe ndo yule yule tu,yani mpaka wanajitoa akili.
Wakati harmonize yupo full beneti na diamond walianzisha vita KWA diamond ilj amteme huyo mmakonde na wakamsifia kinafiki rayvanny Ili aonekane anajua kuimba KUSHINDA harmonize lakini hata wao hawakutegemea haya,hata leo wanamsapot kinafiki Ili kumkomoa mondi.
Ajabu ni kua anayemtukana mondi anapata umaarufu na faida,anayemsifia pia na kumtetea sana the same.
Cc mwijaku,babalevo,jumalkole na page za udaku.
Ama kweli hii kweli ALMASI,mpaka mzee mzima Ostadh Juma naye kaanza na kuanzisha ka online TV chake,anapiga vifedha vya hapa na pale
Hawezi kujibu ,Hana majibuHarmonize aache ushamba, anajiskiaje anavyongea kila siku lakini hajibiwi kitu na Mondi.
No mimi sijajaa ujinga, ni weeeh tu na akili zako ndo umeshindwa kunielewa.huu ni ujinga umekujaa.
boss wako angekuwa na mentality kama yako hii,angekuwa kabung'aa wala hajishughulishi tena.
lakini anajua binaadam hana limit katika kutafuta,anawezapitwa.
Sijasema kaiba kazi ,sasa siijui hayo maswala ya copyright yametoa wapi.Mkuu una uhakika hana copyrights mpaka kupewa nafasi ya kurudia ngoma hiyo au unadhani wanaenda enda tu chief? Hizi mambo zipo sana na ni business, nenda kamdiss Whitney Houston kurudia ngoma ya Dolly Parton au Jay Z ngoma ya Pac Me & My girlfriend, Dakika Moja AY na FA feat. Hard Mad wamerudia ya Ngwea dakika moja.. chimbua vitu chief