Harmonize: Nilipewa Mkataba wa kuonewa na WCB na nilisingiziwa kumroga Diamond Platnumz

sema wakati wa Mungu ukifika umefika ndugu zangu.[emoji23][emoji23][emoji23]

nimecheka sana mtu kakubali kulipa 500mln lakini uhakika alio nao ni milioni 100 tu kwa mauzo ya nyumba yake.
halafu ghafla sayona wanampa hela japo kwa mbinde,crdb nao kwa mbinde[emoji38][emoji38].

all in all anastahili pongezi kwa alipofikia.
 

ndugu yetu mtaalam wa sheria umeshindwa kabisa kuiona hoja ya harmonize kwenye interview yake ya zaidi ya dakika 40???

tokea mwanzo anakwambia ni kwa namna gani alihangaika kuweka mambo sawa,aendelee kuishi pale lakini katika hali ya amani.unaweza niambia kufanya kazi chini ya visa na vitimbi ni level ipi ya sheria inayosimamia makampuni inafundisha!!!

kavunja mkataba akakabwa alipe 500mln sawa,ambayo mwisho wa siku imekuwa 600 na majungu juu,hii ni sheria gani inazungumza haya!!!

hata serikali haiamini uchawi wala majungu,ila kuwa ofisa wa serikali ndio utajua wewe ni serikali ama ni ofisa wa serikali,hakuna rangi utaacha kuiona humo serikalini.

wenye kampuni zao hata wanapopata faida kwako kupitia sheria walizoweka,bado huwa wanatamani usipeleke ujuzi kwingine baada ya kuachana nao story yako iishie pale pale.
 
Hahaha...siku huyo mwanajeshi wenu akimzidi Naseeb kwa chochote kile (hâta kimoja tu) nitawaelewa,ila kwasasa nawaona kama wafa maji tu maana hakuna hâta hoja moja ya maana mnayotoa.

huu ni ujinga umekujaa.

boss wako angekuwa na mentality kama yako hii,angekuwa kabung'aa wala hajishughulishi tena.
lakini anajua binaadam hana limit katika kutafuta,anawezapitwa.
 
Ila lazima tukubali kila kitu kina kushuka, asipojiweka vizuri atakumbuka
Siku ambayo Diamond atakuwa ameshuka, hakutakuwa na mjadala wowote kuhusu DIAMOND tutakuwa busy na mtu mwingine kabisa mwenye wakati wake.
 
Reactions: Qwy
Diamond mnyonyaji na wale mameneja wake.Unamlipishaje mwenzako 600M?

Anguko Lake lipo tu,asidhani atakuwa vzr milele.Walikuwepo wakina Juma Nature sembuse yeye!

Halafu anaanza kumfitini mwenzake na figisu kibao ili ashuke na kuanguka chini kimziki.
 
wakati wenzako wana hangaika kutoboa kimataifa zaidi na zaidi kwa kufanya collabo na wasanii wakubwa i.e Justine Bieber kuna mwamba yeye yupo bize studio na 20% ana kwambia we are going global
 
Diamond kashinda vita dhidi ya shujaa muongoza njia, kitu gani mmakonde wa Chitoholi?

mmakonde ndiye msanii mwenzie anayevaa cheni za almas,ambazo yeye anaziita mabati.

wakati mwingine njia bora ya kumzibiti jinamizi,jipake mkaa halafu mfate,uone kama atakuzoea zoea kindezi.
 

mpaka sasa konde anaongoza 8:0

mond anaposimama yeye kama yeye kumejaa baraka na ishara ya mafanikio,shida ni chawa wake wanaotaka kula kupitia yeye ndio wanaharibu.
 
Me mbona sionii mond alichofanya mpaka asemwe hivo nafikiri ni sababu ya ukubwa wake,, ukiwa mkubwa lazima usemwe tuu! Sikilizeni nyimbo nyingi za harmonize huwa zinamsema sana mond lakin mond hajawah jibu
 
Me mbona sionii mond alichofanya mpaka asemwe hivo nafikiri ni sababu ya ukubwa wake,, ukiwa mkubwa lazima usemwe tuu! Sikilizeni nyimbo nyingi za harmonize huwa zinamsema sana mond lakin mond hajawah jibu
 
huu ni ujinga umekujaa.

boss wako angekuwa na mentality kama yako hii,angekuwa kabung'aa wala hajishughulishi tena.
lakini anajua binaadam hana limit katika kutafuta,anawezapitwa.
No mimi sijajaa ujinga, ni weeeh tu na akili zako ndo umeshindwa kunielewa.

Unaposema "anaweza pitwa" hiyo ni probability tayari. It's ether going or not going to happen kwa factor yoyote ile.

Nimekuomba unitajie kitu kimoja tu ambacho Harmo anamzidi Naseeb, na kama hakipo kwa nyanja zote ,unaachaje kuonekana mjinga unapojaribu kushindanisha hawa watu wawili?

Supotini kazi za kijana wenu kama kweli mnampenda, maneno kama haya hayataweza kumpandisha wala kumshusha aliyejuu.
 
Sijasema kaiba kazi ,sasa siijui hayo maswala ya copyright yametoa wapi.

Nilichokisema ni swala la yéyé kujiita teacher wa Amapiano ilhali hiyo ngoma yote aliyoimba ni melody ya "Mang'dakiwe" kwa kila kitu.
 
Diamond ni mwanamziki mkomavu sana, toka ameanza kuhit Huwa tunasikia kwamba amefika mwisho wake lakini mwisho wake haufiki.
Diamond ni mwanamziki mkubwa na mziki unachangamoto zake pia biashara haitaki ushkaji.

Nenda hata Kwa akina Bakhresa ongea na wafanyakazi wa viwandani utajua kwamba biashara haitaki utoto hata siku moja.
Na kama utacheka na wapinzani wako wanakupoteza.

Kwamba Harmo yeye Hana matatizo mwenye matatizo ni Diamond tu basi na mchawi ni Diamond yeye sio mchawi kabisa ni mtu wa Sala sana, inachekesha sana.

Uchawi unapozungumziwa sana na mtu na kuona mafanikio ya watu yanatokana na Uchawi hiyo inakua ndio Imani yake huyu mtu anahisi Uchawi anaofanya unafanywa na kila mtu na kila mwenye mafanikio basi ni mchawi zaidi yake.

Mtu akisema huniwezi kwa Uchawi huenda ananguvu inaoushinda Uchawi.

But mafanikio ni shida sana kuyamaintain na watu wanapambana haswa ukikaa kiboya tu kwenye mziki utapoteza hufiki mbali.

Sasa Hamo kama anataka kuonewa huruma kwenye game na washindani wake atapoteza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…