Harmonize: Nilipewa Mkataba wa kuonewa na WCB na nilisingiziwa kumroga Diamond Platnumz

YATASEMWA MENGI ILA ALBUM ISHABUMA NA ZA CHINI CHINI KUNA WASANII WANAMKIMBIA HAWAONI KINACHOENDELEA PALE KONDE GANG

BAADA YA MUDA SIO MREFU ATAANZA KUSHIKA UCHAWI WATU WA KIJIJINI KWAO

Hoki ndicho nachokiona
 
Jikite kwenye hoja za Konde kama una ukomavu wa kujibu, hakuna sehemu amelialia bali amechoka kusakamwa like hana fadhira na hana baraka za Wasafi…. hoja zina ukweli au porojo?
Hoja gani za kulia lia alionewa?
Nakubali alionewa so what?

Na nani ana MSAKAMA mmakonde?
Anajisakama mwenyewe kwa kukubali kuishi chini ya kivuli cha wasafi
Miaka mitatu sasa ngonjera ni hizo hizo tuu

Watu wanataka kuona ngoma zaidi ya kwangwaru na iyola
Watu wanataka kuona akina Ibrah, Cheed Angel wakifika mbali
Watu hatutaki kusikia habari za wasafi walinionea........ inatosha
Mwambieni a move on na maisha sio kukaa miaka yote yeyeni kulialia tu
Hata akipigwa chini na mademu zake lawama ni wasafi
Nyimbo zake ni kulia na wasafi
Huu upuuzi sasa
 
Sijaelewa aliamua kuongea hayo Ili kutafuta kiki mpya au? Maana sijaona logic yoyote so far na wala hakuna ubaya wowote Kwa akina Diamond walichokifanya ..
 
Hapana sio kiki, amezungumza ukweli ambao hajawahi kuzungumza kwenye media yeyote
Lengo la huo ukweli ni nini kama sio kiki kwa wajinga.Kwa mtu mwenye akili timamu sijaona kosa kwa kina diamond wala yeye alipoonewa as far as business is concerned.
 
Ukiwa huna akili ya mtizamo wa kibiashara unaweza ongea huo utoto wako.

Kama kwa kipindi kile Harmo alikuwa ndio nguzo ya label ya wcb ni wazi haingekuwa rahisi kumuachia.Pili kama kutoka kwake kulikuwa na malengo ya kuharibu label na kuwa mshindani lazima aletewe zengwe maana amekuzwa humo.

Mara ngapi wachezaji wanakataliwa kuvunja mikataba? Lazima utafutwe mda muafaka wa kumuachia asiwe threat kwa label yao ,hizo ni vita za kibiashara..

Unaona sasa katoka lakini hakuna cha maana anafanya kwa sababu za miscalculation.
 
Me mbona sionii mond alichofanya mpaka asemwe hivo nafikiri ni sababu ya ukubwa wake,, ukiwa mkubwa lazima usemwe tuu! Sikilizeni nyimbo nyingi za harmonize huwa zinamsema sana mond lakin mond hajawah jibu
Uncle shamte unauhakika
 
Me mbona sionii mond alichofanya mpaka asemwe hivo nafikiri ni sababu ya ukubwa wake,, ukiwa mkubwa lazima usemwe tuu! Sikilizeni nyimbo nyingi za harmonize huwa zinamsema sana mond lakin mond hajawah jibu

Uncle shamte mwenyewe naona upo
 
Anaelekea kusema kushindwa kwake karogwa, alifanya miscalculation..ndio maana sio kila mtu anaweza kuwa muajiri au kujiajiri ..Sasa anapanic
 
Juma juma lokole naona hela ya posho na urafiki wako na dadayake mondi unakufanya unakuwa mtumwa kwa mwanaume mwenzako
 
serikali iache kudili na masuala ya maana ianze kuhangaika na wasanii we jamaa kumbe wakat mwengine una tumia Masabuli kufikiria

ushawahi sikia serikali ya Us kuingilia ugomvi wa eastcoast na west coast?
 
Sasa unasema suala la kulipa 600M linatokea wapi wakati haujausoma mkataba wake? Sheria ya mikataba ndiyo inaratibu mkataba wake alipokuwa WCB.

Aliingia WCB akiwa hana kitu...kampuni ikawekeza milions of money...akakua na kuwa almost msanii wa pili kwa ukubwa nchi hii.

Anapovunja mkataba..lazima mrudi kwenye ule ule mkataba..unasemaje pale upande mmoja unapotaka kuvunja mkataba?

Yeye msanii pale kwenye label alikuwa anafanyiwa kila kitu..kazi yake ni kurekodi nyimbo na video chini ya gharama za label. Promotions zote inafanya label...

Videos na audio zote, jina lake la kisanii, account za YouTube zote ni mali ya label. So anapotoka na akataka kutumia hivyo vitu..ni lazima anunue rights ziwe zake.

So justification ya 600M inakuja baada ya kupiga hesabu za uwekezaji aliofanyiwa toka ameanza kurekodi wimbo wa kwanza. Pia gharama za kununua haki za kazi zake zote ambazo zilikuwa zinamilikiwa na label. Mwisho ni brand kama brand...aliingia kwenye label akiwa pangu pakavu sasa anatoka jina lake likiwa ni brand kubwa...lina value.

Utagundua kuwa 600M ni kama vile WCB wamemfanyia fair...hasa ukizingatia ameruhusiwa kutumia kazi zake, na social media platform kwa majina yake ya kisanii ambayo bado yanazidi kuingiza pesa. Fikiria kama angekatazwa kutumia jina lake na kazi zake...but those guys walimruhusu.

When a contract comes to an end..parties are restored to their original position as if they have never contracted at first place.

So Harmo alipoondoka..ilikuwa ni sawa kulipa gharama hizo maana the other side wali spend zaidi kwake kumkuza na kum brand...angeondoka bila kulipa ingekuwa ni unjust enrichment.

Sasa hivi anaiona hiyo 40% kuwa ilikuwa ni ndogo na alikuwa ananyonywa...wakati anaingia label alikuja na nini? He was broke na diamond took a leap of faith kwa kuwekeza kwake. Imeanza kuonekana ni ndogo once things turned out better.

Pia awe makini...asijepigwa defamation suit maana ametaja majina ya watu clearly na mambo mengi aliyosema hawezi kuyathibitisha endapo atapelekwa mahakamani......na pia kitendo cha kuvujisha mazungumzo yake na Vanny boy publicly kinaweza kuja kum haunt kama wenzake wakiamua kupita route ya jinai.
 
Respect Slowly
 
Anaelekea kusema kushindwa kwake karogwa, alifanya miscalculation..ndio maana sio kila mtu anaweza kuwa muajiri au kujiajiri ..Sasa anapanic
Asitafute mchawi nani ajipambanoe tuu

Yeye ni shahidi kipindi yuko wasafi jinsi walivokua wanabaniwa na media kibao bongo ila boss wake aliminya kimya mpaka alivokuja na hiyo wasafi tv & radio. Aongee kwa vitendo sio hizi bra bra ambazo zitatrend wiki 1 zitafutika vichwani mwa watu na kuanza kujudge kazi.
 
Mkuu hiki kitu kinakwepwa sana kuongelewa na kufanya WCB waonekane kweli ni wanyonyaji. Yule mwamba tumemjua akiwa wasafi mpaka anakua msanii mkubwa yuko chini yao.

Kila kitu anafanyiwa, achana na hilo si ajabu pia alikua anashirikishwa kwenye maamuzi. Sasa asset kama hii kweli ikitaka kuponyoka eti akulipe pesa ndogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…