Harmonize: Nilipewa Mkataba wa kuonewa na WCB na nilisingiziwa kumroga Diamond Platnumz

Harmonize: Nilipewa Mkataba wa kuonewa na WCB na nilisingiziwa kumroga Diamond Platnumz

Boss akifakisha lazima achanwe kumnyenyekea nyenyekea ni kufuga ubovu, harmonize anaweza asiwe sahihi ila diamond kashfa kama hizo anazo nyingi lakini kwakua ametengeneza fanbase kubwa huwezi kuta yanazungumziwa madhaumifu yake

Wakubadilika hapo sio harmonize, ni wote endapo kuna mahali wanakosea basi zisemwe tofauti zao.

Na sio kunyamazia madhaifu ya mwingine eti kisa huyo mtu ndiye aliyesaidia kumuinua mwingine kimuzuki, hapo hamtakua tofauti na jaji anayeendesha kesi ya mbowe.
Uko sahihi
 
Mashabiki wa Diamond wanapenda kumuattack Harmonize kwasababu wana tabia ya kuwa na chuki zao tu.
Hata kabla hajasema mimi nilijua mkorofi ni domo kutokana na scenario moja niliyowai ishuhudia kati yao hapo nyuma. Harmonize ni mstaarabu sana ila mashabiki wa domo wanamfatafata sana.

Lakini dogo amesimama vema sasa hawataweza kumwangusha zaidi ya kumwongezea fans.
Kwa watoto hawa wadogo wanaokua sasa wanamfaham zaidi hamo kuliko domo.
Mashabiki wa domo wanazeeka wakati mashabiki wa amo wanakua.

Hivyo mahesabu yanaonyesha ni wapi hawa miamba wawili wanaelekea.
Huyo harmonize ambaye kila nyimbo anamuimba diamond ndo mtaarabu??!! Au ustaarabu ni nini mkuu??
 
Dogo anaelekea kuchanganyikiwa sasa hv,bora angebakia kimiya tu.

Yaani uwezekano wa kutolipa pesa upo eti kisa amani unakuja kulipa mil 600,kweli,huna ndugu wa kuwapa hizo hela hadi umpe Diamond kisa amani??,serious???

Na hizo kolabu zingine je alikatwa dola ngapi,mbona ameitaja ya reekado tu?
 
Mzee unadhani wabongo hata ukiwaambia ukweli wanabadili mawazo?

Watanzania sisi ndiyo watu pekee ambao tunapenda au kumchukia mtu bila sababu ya msingi.

Alichofanyiwa harmonize watasema sawa ila kwa ruge rip walikuwa wanasema mnyonyaji hata kama hao wanaodai alikuwa anawanyonya walikuwa wamesaini mikataba kwa hiari yao.

Tanzania jambo linaweza kuwa zuri au baya ila inategemea mtendaji ni nani.
Uko sahihi kabisa!ruge alikua mnyonyaji but diamond yuko sahihi!!ptuuu!

Uonevu tu!kunya anye kuku....!!!
Harmonize ni binadamu kila kitu kina kikomo!

Huyo Mondi mkamilifu Kagombana na Dimpoz,Shetta na Ney na wote kaimba nao ngoma!

Ina maana hao wote wakorofi Mondi ndo mkamilifu? kuna shida WCB mkubali mkatae nyie wenye timu zenu!![emoji57][emoji57][emoji57]
 
Huyu mziki ushamshinda,album inafanya vibaya.

Sasa Diamond kama angetaka kila siku kuwa yy.

Kaanzisha lebo ambayo imemtoa yy.
Kampeleka nje kufanya video kubwa.
Kamkutanisha na wasanii wakubwa Africa.
Kamtoa Rayvanny mpaka kufikia hatua ya Colabo na Maluma na kuchukua BET,Tz hii Rayvanny ndiye mwenye nyimbo yenye streams nyingi, kapiga show jukwaa la essence, mafanikio ambayo Diamond hajawahi kuya fikia.

Angeamua kuto kuanzisha label tusinge mjua na Diamond ni mfanyabiashara, always ana angalia faida na label zote duniani zina angalia faida, hata yy na JembeniJembe wanaangalia faida.

Yeye mwenyewe kuimba aliambiwa hajui, Diamond kakaa nae zaidi ya miaka mitatu, akimfundisha na kumpika kimuziki na kuna watu walimwambia hajui kuimba ila Mondi hakukata nae tamaa, kula,kuvaa na kulala kwa Diamond.

Anadai WCB walikuwa wana muogopa yy, haya leo zaidi ya miaka miwili nje ya WCB, yupo yy peke yake,free habanwi je kafika wapi,kampita Diamond?Anapata airtime ktk media zote kubwa zilizo kuwa hazipigi nyimbo zake.

Halafu haja tuambia wasanii wake wanapata kiasi gani, mikataba yao miaka mingapi,wana miaka miwili hawa heleweki wanafanya nini.
Mi huwa namshangaa sana anavyo fanya ligi na mwalimu wake..ujue mda mwingine binadamu hatuna haya na adabu..

Harmonise ni zao la WCB 100% sasa sijui kwanini hana shukrani kiasi cha kuasema anayo yasema uko na kufanya ligi za kurusha madogo WCB.

Kasahau BSS? Yule ndio yeye sasa kama Rajabu. Ukizungumzia Harmonize basi ujue ni WCB...akae akijua ivyo sikio kamwe halizidi Kichwa...

Ova#
 
Hilo nalifahamu fika...

Tangu enzi Harmonize yupo Wasafi, nilikuwa namkubali Rayvann mara 100 kumlinganisha na Harmonize

Na kilichokuwa kinanikera zaidi kuhusu Harmonize ni ile kuiga kila kitu toka kwa Diamond.... yaani alikuwa Clone ya Diamond; hakuwa unique kama Rayvann ambae hata kama umepiga mtungi na kuzima, ukisikia ngoma mpya ya Rayvann utajua tu huyo ni Rayvann!!
Ukicheki video ya inde ft dully yule ni mondi kabisa.

Wizkd alivyo kuja Mwanza alimchana live aache kumcopy mondi
 
Sina uhakika lakini nahisi Mond ana mkwanja mrefu kuliko hamo.
Hamo kwa sasa anapata mkwanja mrefu kuliko alivyokuwa kwa mond.

Naamini hizi ni facts.

I am sorry kwa leo kuongelea huu ugomvi, nimekuwa nikikwepa kutia neno kwani najua mambo machache lakini ni sababu concrete juu ya huu ugomvi.

Tuwapongeze vijana wanastruggle kuzichangisha.

Tatizo langu huwa sipendi mtu aonewe.
Sawa kaka
 
Back
Top Bottom