Harmonize: Nilipewa Mkataba wa kuonewa na WCB na nilisingiziwa kumroga Diamond Platnumz

Harmonize: Nilipewa Mkataba wa kuonewa na WCB na nilisingiziwa kumroga Diamond Platnumz

Hivi harmo alivyotoka wasafi si diamond aliendelea kumsuport tena akawa anapiga ngoma zake kwenye media? Harmo alivyoanza kumtumia hbaba sijui mwijaku kumtukana diamond ndo mambo yalipoharibika sasa diamond kujibu mapiga anaonekana mbaya?
Harmo ni chenga yule
 
NB: Kweli Konde Jeshi, yaani amekaa na haya yote kwa miaka mitatu na wakati Manara alishindwa kukaa nayo hata kwa wiki moja tu.
 
Mondi Ndio kuna Baadhi ya mambo anazingua sijakataa Coz ni binadamu ila
Njomba Nchumali aache kutia Huruma kila siku anatuchosha 😅
 
Njomba Nchumali analalamika Kwa nn Diamond hawazuii Kina Juma Lokole na Baba Levo kumsema yeye kila siku 😅

Namuuliza swali Na yy Kwa nini hawazuii Kina H Baba Na Mwijaku ambao kila siku wanamtukana Diamond ambae ndio alimtoa kimziki

Au Nyani haoni kundule 😂
 
1. Pesa ya kuvunja mkataba ilitolewa na sayona CRDB bank na jembe ni jembe sio kama tulivyoaminishwa kuwa sarah alihusika.

2. Diamondi ni mtu mwenye roho mbaya sana rejea kauli za Ommy Dimpoz, belle 9, shettah rich mavoko.

3. Rayvanny anavumilia kuwa wasafi hajui pa kuanzia kutoka tena kwa yeye wanaweza sema atoe bilion 1.

4. Bila amri ya Magufuli Diamond asingesaini kuvunja mkataba kwa wakati.

5. Harmonize mwaka wa 3 anaendelea kuwepo kwa game nje ya wasafi.

6. Kuna watu huwa wanalazimishwa kumsifia na kumpost Diamond kila kukicha ama akiwa na jambo mfano jana amepostiwa na mama yake uncle shamte baba levo page ya wasafi.

7. Nyimbo zote nzuri za WCM Mondi alikuwa analazimisha aweke mistari yake ili ikitoka ionekane yeye ndio ameibeba nyimbo wakati kiukweli sio sahihi alikuwa hataki kupotea masikioni kwa watu.

8. Uchawi ni sehemu ya maisha ya Diamond.

9. Mameneja na ndugu wa Diamond walichangia ugomvi kuwa mkubwa sana.

10. Mali tunazoaminishwa za Diamond zingine hazina ukweli.
 
Aliyeanza vijembe ni Harmonize na Dimondi alikuwa kimya akarudisha majibu kwa kumuita mjomba nchumali, Harmonize akatoa wimbo wa Wapo akiwa analalamika.

Juzi huzi tena kwenye album yake karusha vijembe vya kutosha, kasema mpaka yeye ana nguvu ya kumuua simba akamuita Rayvanny paka anayejiita chui, Dimondi akarusha kijembe eti mihadharati jamaa akajaa upepo akaandika gazeti na press conference juu....mtu pekee anayemuweza Dimondi na WCB ni King Kiba....utamrushia vijembe na yeye anakutumia kijembe hajai upepo tena kuna muda anakufanyia dharau wazi wazi kabisa [emoji205]

Hapana wcb walianza bana kumsakama
Hamo mstasrabu sanaa
 
Back
Top Bottom