Watu Naona Wanachanganya VITU HUMU [emoji28][emoji28]
Suala la Harmonize Wekeni Utimu Pembeni Halafu Tujadiribkwa Facts.
1. Watu wanalinganisha Diamond Na Clouds. Ieleweke kuwa Diamond Hajawahi Kuwa signed na Clouds Media Group as Company kama Msanii wao. Na wala Clouds Media Group Haihusiani na Kuwasimamia Wasanii. Clouds Media Group ni Compny inayojihusisha na MEDIA + ENTEGNTEIMENT INDUSTRY Basi Haimsimamii msanii. So ukiitwa na Clouds Media Group Twende Kwenye Show, Ni Suala La Makubariano malipo yenu yatakuwaje yaani kwa kifupi unakuwa Day Worker, ukimaliza kazi yako unachukua mpunga Unasepa. Kwa hiyo Diamond Alichokuwa anapishana na Clouds Media Group, ni kumdharau na kutaka kumchukulia poa na kumtumia kwenye Show watakavyo. Diamond Akaweka Standards Kwake na Kwa Wasanii wake Kuwa Mimi Ili nifanye Show Malipo yasiwe chini ya Millioni 11, Ukimtaka Harmonize Malipo Labda yasiwe chini ya Millioni 8 na wengine. So clouds Media Group kwa Wakati huo ndio Media iliyokuwa na Nguvu hivyo wasanii hizi show walikuwa wanakubali kwasababu hakuna mbadala, walivyo ona Diamond Anavimba ndio wakaingia kwenye Ugomvi. So ni Vitu viwili tofauti kabisa.
2. Watu wanaona Kwa Msanii Million 600 ni Nyingi. Lakini Kwa Level Aliyokuwa Amefikia Harmonize Kwa Tanzania Kwa Wakati ule yuko Wasafii Millioni 600 ni hela Ndogo Sana. Kwanini Ni Hela Ndogo. Tuchukue kila Video Aliyoitengeneza Harmonize imegharimu Tsh Ngapi? Kuanzia Aiyola Just Roughly Gharama Za Shooting, kwenda South Africa na Sehemu zingine na Vitu Vyote. Chukua Kila Video Imegharimu Millioni 80 kwa Nyimbo 6 ni Tsh 480M. Production ya Hizo Nyimbo? Utajikuta kwa nyimbo 6 unafikia Millioni 600, Akiwa Chini Ya WCB katoa Video Ngapi na Audio Ngapi? Na kwa Wakati ule Bila Kwenda SA huja Shoot Video. Kumbrand Harmonize Imegharimu Kiasi Gani? Wasanii wangapi Wazuri Tanzania Zaidi Ya Diamond Na Alikiba Wameshindwa Kujibrand? Utaelewa pia Kumbrand Mtu ni Gharama ni pesa Nyingi, na Kwa Wakati huo Kituo Kikubwa Cha Media Kimegoma Kucheza Nyimbo za Harmonize Unatumia Gharama kubwa kiasi Gani Kumbrand Harmonize ili Nyimbo zake Zichezwe Trace, MTV na Nchi Zingine bila Msaada Wa Kituo Cha Radio? Ukijiuliza hayo maswali Utaona Ni Gharama kubwa kiasi gani Ilitumika Kulinganisha Na Millioni 600.
3. By the Time Diamond Anamchukua Harmonize Diamond Alishakua Star, alikuwa akikupost Kuwa Wewe unajua Kuimba Au akapost wimbo Wako basi Utaenda Viral, Na Diamond Alikuwa Na Management, Chukua Diamond Alikuwa Akishirikishwa kwenye Wimbo Analipwa Sh Ngapi? Tuchukue hela ndogo 20M, Harmonize Kafanya Collabo Ngapi na Diamond For FREE ili Dogo Aendee? Na Zote Zilikuwa Moto? Chukua hiyo Gharama the Muone Kama Kulikuwa na Faida na Hiyo 600M ilikuwa kubwa?, Harmonize Alitengeneza Social Media Accounts Ambazo ziliendelea kumlipa sana Kuanzia Youtube Accounts na Instagram amefaidika Vipi na hizo Accounts? Bado WCB walimuachia.
4. Watu Wanasema 600Millioni ni kubwa WCB kuchukua kwasababu walikuwa wanapata 60% kutoka Kwa Harmonize na Harmonize Anapata 40%, Twende Kwenye Jicho La Kampuni… Harmonize Akichukua 40% yeye Hakatwi kitu chochote kile yaani 40% yote Inaingia kwenye Account Yake kwasababu ni Msanii ambaye yupo chini ya Kampuni, Hivyo TRA haikuwa Inamtambua Harmonize ila Ilikuwa inaitambua WCB kupitia ile 60% ambayo Harmonize analalamika alikuwa Ananyonywa. Chukua WCB katika 60% walipe Kodi Halali ya Kitanzania ya ongezeko la Dhamani yaani VAT, katika 60% wanalipa 18% kwa TRA kama Kampuni Inabaki na 42%, Wakati huo Kampuni Ina Waajiriwa Wengie walio kuwa Wanahusika Na Kuhakikisha Show, au kila kitu nyuma Ya Harmonize Kinaenda Sawa na Wapo chini ya Kampuni, hivyo watahitaji mishahara kupitia hiyo 42% iliyobaki, zitahitajika Kumaintaine ofisi katika hiyo 42% na RUNNING COST zingine zote zitatoka kwenye Hiyo 42% unataka kusema katika 60%, PROFIT MARGINE YA WCB Ilikuwa kiasi Gani? Wenye Kampuni wanaelewa nini Nasema au Walio wahi kusimamia Kampuni… Kumbuka Muda Huo Harmonize Yeye Kachukua 40% yake Kaweka Mfukoni. Kama Ilikuwa Ni Show imeandaliwa na WCB As Compny Itagharamika Usafiri, Mavazi na Malazi Ya Msanii kwenye hiyohiyo 42% baada ya VAT Ambayo HARMONIZE ALIKUWA ANALALAMIKA ANANYONYWA. So hii ISSUE inahitaji Kuwa Knowledge ya Biashara Kuelewa COST PER UNIT + RUNNING COST Vs 40% ambayo bila makato inaenda Direct kwa Harmonize. SWALI JE 600M Ni Kubwa?
5. Tunafichwa na Mwamvuli wa Umaskini Kuamini 600M ni Kubwa Lakini Ukiangalia Walicho Spend na Faida Iliyo tengenezwa Utaona Kwa namna Gani Kumsimamia Msanii ni Gharama. Label Ngapi zimevunjika? Label Ngapi Zimeshindwa kuwasimamia Wasanii? Kuwa Na Kampuni ni Stress ndio Maana Kuna Muda Nikisikia Diamond Anatumia Madawa Ya kulevya, Naelewa Ni STRESS kiasi Gani Anapitia Kuhakikisha Kampuni Inaenda. Tunaona Matajiri Wakubwa Wakiingia kwenye matumizi ya pombe kupita kiasi na Bangi kwasababu Ya stress za Kumanage Kampuni.
6. Ukishakuwa Na MKATABA na Kitu Fulani, Tafsiri Yake ni Kuwa Mmetoa Masuala ya Mahusiano na Mmeweka MAANDISHI YAONGEE. Ndio Tafsiri ya Mikataba. Kuna Sheria Tanzania Ambayo Inasimamia MIKATABA YOTE TANZANIA, Hata Mkataba Ulio pewa wakati unaajiriwa unasimamiwa na Sheria ya Mikataba Tanzania. Kitendo cha Ku sign mkataba Kinatafsirika Kama Umesoma na Kuelewa kile kilichopo kwenye Mkataba na SHERIA YA MIKATABA TANZANIA, Inalazimisha Mkataba wowote ule Kusema/ Kutaja Ukomo/Muda wa Mkataba. Sasa Kama Harmonize Either kwa Kuelewa Au Kutokuelewa akawa Alisign Mkataba Labda wa Miaka 15 kuwa Chini ya WCB then Baada Ya Miaka 5 anataka kujiondoa, Sheria Mikataba iko Wazi, Utalipia Miaka 10 iliyobaki. Tuseme Harmonize alikuwa Amepigiwa na Kampuni kila Baada ya Mwaka Anaingiza Faida Ya TSH millioni 60, kavunja mkataba ukiwa bado una miaka 10 inamaana Anapaswa na Sheria Inamtaka alipe Millioni 600 kuweza kuvunja Mkataba Au Na zaidi! Na Mikataba huwa wazi Hutaka kwanza Kufanya Mutual Agreement au pande moja Ilipie Fidia. So Harmonize Angekuwa na Mwanasheria Mzuri, Angepitia Mkataba na Kumshauri kuwa Bwana una Mambo Mawili, 1 vumilia Mpaka mkataba utakapo kuna kuisha Au 2. LIPA PESA YA MIAKA 10 Vunja Mkataba. JE, ILE SIKU ANAHOJIWA KUNA MWANDISHI YEYOTE AU MTU YEYOTE ALISHA WAHI KUMUULIZA HARMONIZE ULISIGN MKATABA WA MIAKA MINGAPI? Kwa Lugha Rahisi Angalieni Uhamisho Wa Wachezaji Mpira Wa Miguu Unavyofanywa mtanielewa kwenye Hili. Hata Nyie kama Kuna Mtu kaajiriwa na Una Mkataba Sheria Inasema Ukiacha kazi Ndani ya masaa 24 unapaswa kumlipa mwajiri wako Mshahara wa Mwezi 1 [emoji28] UKIELEWA HIVYO UTAELEWA KUWA MKATABA JAPO HATUJAUONA ILA HAUKUWA WAKINYONYAJI.
7. MWISHO
JAMANI TUKUBALIANE UKIWA CHINI YA KAMPUNI UNABEBA IMAGE YA KAMPUNI, Hivyo Kitendo Cha HARMONIZE KUFANYA SHOW Sehemu Yoyote ile Bila Ruhusa Ya Kampuni ni KUIKOSEA KAMPUNI YAKE, Na LAZIMA AELEWE DHAMANI YAKE, kwa Wakati ule WCB as Company ndio walikuwa Wanaelewa Dhamani Ya Harmonize Akisimama Kufanya Show, So ili Kujibrand na Kujipa Dhamani Huwezi shuka ovyo ovyo kwa Mashabiki kuwafanyia Show kisa Wamekushangilia [emoji28][emoji28][emoji28] so Hizo Millioni ngapi alizo lipishwa ilikuwa SAHIHI 100%, Tujiulize Mlisha Muona Wizkid Anaimba Imba Kwenye Harusi, Birthday, Viwanjani bila Show Maalumu? [emoji28][emoji28][emoji28] au Davido au Future au Msanii yeyote mkubwa Marekani? Kuna Muda hata Kwenye Interview hawaendi endi tuuu kisa Umeitwa, Hii yote ni Kujitengenezea Dhamani. Na ndicho walichokuwa wanafanya WCB kwa Wakati huo, Wewe Umeenda Taifa Kuangalia Mechi angalia Mechi maliza nenda, Kushuka Chini Kuimba kama Kampuni Ilikuwa Imepanga Next week Wakupe Show Je? [emoji28][emoji28][emoji28] WASANII WENGI WA TZ wanakosea Hapo kujishusha DHAMANI na Ndicho Anacholilia HARMONIZE ana Alicho Taka WCB wafanye.
NISEME TUU, HARMONIZE ALIBAHATIKA KUPATA KAMPUNI AMBAYO NAYO KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE WALIKUWA HAWAJUI DHAMANI ZAO. NASHANGAA HATA MANAGEMENT YA DIAMOND kwanini Inamuachia Diamond Anazurulula Ovyo ovyo na Kina Baba Levo na Juma Lokole, anaenda Ovyo ovyo kwenye Vishughuli visivyo na Maana kama Harusi [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] Ni Kujishushia Dhamani JAPO WATU HUMU MUNAWEZA MSINIELEWE.
Ni Hayo tu