Harusi meza kuu bibi harusi hakuna baba wala baba wadogo. Mabinti hamuoni aibu

Harusi meza kuu bibi harusi hakuna baba wala baba wadogo. Mabinti hamuoni aibu

Nipo kwenye harusi upande wa bibi harusi meza kuu hakuna baba,wala baba wadogo wala wakubwa meza kuu wapo mama mama wadogo wajomba watoto wa wajamba kaka zake na dada zake tu

mean kijana kaenda kuoa binti alielelewa na single mother na hakuwa na mahusiano mazuri na baba zake

Hili ni kosa la bibi harusi kwa namna gani?
 
Nipo kwenye harusi upande wa bibi harusi meza kuu hakuna baba,wala baba wadogo wala wakubwa meza kuu wapo mama mama wadogo wajomba watoto wa wajamba kaka zake na dada zake tu

mean kijana kaenda kuoa binti alielelewa na single mother na hakuwa na mahusiano mazuri na baba zake
Kuna kipindi naishi Dar kipindi hicho nipo na Umri chini ya miaka 20 nilikua na tabia ya kuzamia kwenye harusi mbali mbali za Dar, Sasa kuna Sendoff ilikua inafanyika maeneo ya Sinza Sasa kwenye ukumbi kuliku na sehemu mbili sehemu ya Upande wanaokaa Wazazi wa Upande wa Mwanamke na Upande wa Bwana harusi mtarajiwa, Sasa Kwenye hiyo Send-off Bibi harusi alikua kashaingia ndani kakaa mbele na upande wa kushoto wapo Wazazi wake, Sasa Upande wa Bwana harusi mtarajiwa walikua wasubiliwa ili waingie hapo Ukumbini
Sasa na sisi Wazamiaji tupo nje tunajipanga tutaingiaje na Getini kuna Wazee wanakagua Kadi na wamesimama kwenye kageti kadogo kakuingia ndani ya Ukumbi nilipokua nimesimama kuna jamaa kama watatu wamevaa suti kuwasikiliza Maongezi yao nikajua moja wao ni Bwana harusi mtarajiwa yupo na wenzake hawafiki watano na mimi nikabidi njiogeze nikajua hawa jamaa hawajaja na ndugu wala Wazazi wamekuja kimchongo mchongo na mimi nikasema hapa ndipo pakuwapa kampani ili kwenye eneo lao paonekane pamejaa, Sasa ilipofika saa Moja na Nusu MC nikasikia ana tangaza wageni waalikwa tusimame ili tuwapokee upande wa Bwana harusi mtarajiwa kwahiyo hapo Sasa geti linafunguliwa hakuna kuulizwa kadi wala nini geti lifunguliwa jamaa wakaingia na Mimi nikajiunga nao pamoja uku Dj akipiga nyimbo nzuri ya Chidumule kipindi hicho, tukaingia mpaka katikati ya Ukumbi baada ya nyimbo kuisha tukaelekea kukaa kwenye eneo tuliopangiwa kuka, chakushangaza jamaa hakua na watu wengi yani bila sisi wazamiaji kujaza viti jamaa agekua yupo yeye na wenzake wa nne tu na eneo lao lilikua na viti vingi vinakaribia viti 20, jamaa yeye akakaa mstari wa mbele na wenzake na sisi Wazamiaji tukaa nyuma yao.
Sasa nikawa najiuliza mbona hawa tuulizi lolote wala kutohoji sisi ninani, na Sisi tukawa tunaagiza bia ikiisha tuna mwambia muhudu alete tano tano tu. Kwahiyo Bana share za Dar zimekaa kitapeli tapeli sana, unaweza kwenda kweye Sendoff na Bwana harusi mtarajiwa hayupo anakua yupo Kigoma.
 
Amtafute mtu ambaye hana time nae wala hamuoni kama ana umuhimu maishani mwake? Huyo baba kama angeona umuhimu wa huyo binti angemtafuta yeye, kitendo cha kutomtafuta ni kwamba kila mtu akae na maisha yake
Nina visa viwili ambapo watoto wametafuta baba zao ukubwani. Wa kwanza baba yake alifariki wakati mimba ya huyo kijana ina miezi sita mwaka 1966 kwa ajali ya pikipiki na mama akauchuna.

Mtoto alipojitambua, kama kawaida akamuuliza mama yake biological baba. Mama akawa anazungusha zungusha ila anamueleza kuwa baba yako alifariki katika ajali ya pikipiki. Kila wakati kijana hakuacha kumuuliza ili ajue ukoo wake halisi.

Miaka 10 iliyopita, mama yake alikuwa mgonjwa hoi kitandani! akamweleza mama yake kuwa pamoja na kwamba unaumwa mama, ila la kukutokea likikutokea na hujanieleza baba alikuwa nani, sitakusamehe maisha yangu yote. Mama akafunguka kuwa baba yako alikuwa fulani, alifariki wakati yupo njiani kuja kunitembelea na mimi nilikuwa mpango wake wa kando (mchepuko). Ndiyo maana sikuona umuhimu wa kujitambulisha wakati alipofariki. Ndugu zake walikuwa fulani na fulani wanaishi 150 KM kutoka hapa.

Kesho yake akamchukua mke wake na watoto wake (bahati ashakuwa hata na usafiri wake) wakapiga hodi kwa Baba yake mdogo. Jambo la muhimu alilomweleza baba yake mdogo alisema mimi ni mtoto wenu na nilikuwa natafuta ndugu zangu na ukoo wetu. Sihitaji mali au kitu maana najitosheleza ila nilipungukiwa ukoo wetu. Huwezi amini kwa sasa ndiye mwenyekiti wa ukoo, alivyo committed na ukoo wao.

Wa pili ambapo ni kijana wa rafiki yangu, hii ni ya juzi tu. Jamaa alikuwa na mchepuko wake Songea kwa akina cocastic ! akihudumu TRA Songea Mjini enzi hizo. Mchepuko ulitaka ndoa, jamaa akamweleza ukweli kuwa hana mpango. Kwa vile mchepuko ulikuwa unaisaka ndoa, ukapata muoaji lakini ukiwa na mimba ya miezi mitatu. As usual ukauchuna mtoto kazaliwa ndani ya ndoa! Washaku unawafahamu wakapiga mahesabu na wakiangalia sura wanaona ni copy right ya jamaa aliyekuwa anafanya kazi TRA. Nao wakauchuna.

Mchepu wa jamaa alizaa na mume wake wa ndoa watoto 5 na yeye wa sita. Mama yake akafriki, baba yake akaanza kumtenga tenga wakati yupo Sekondari, maana sura zilikuwa zinatofautiana na wadogo zake. Washaku wakajitokeza na kumweleza kuwa unatengwa kwa vile wewe siyo mtoto wake wa kibailojia ila baba yako yupo TRA Dar anaitwa fulani (walikuwa ni manesi wenzake na mama yake).

Akiwa form six, akajikusanya na kupata nauli toka Songea hadi Dar. Siku moja jamaa yangu yupo ofisini, sekretari kaleta taarifa kwa boss, kuwa kuna mgeni kijana. Kijana akajitambulisha mimi ni mtoto wako. Jamaa alisituka huwezi amini. Ni story ndefu lakini sasa jamaa yangu kaisha mtambulisha kwa familia na ukoo.

Naomba msinipige mawe sisi ni wapenzi wa michepuko ndiyo maana hata mimi sijifichi na Lamomy wangu pamoja na kusema hawezi kuhifadhi takataka mwilini mwake. Sijui mtoto atapatikanaje?

Hebu angalia Mfano wa binti alivyotafuta ujombani, ili mjifunze binadamu wanavyoishi


View: https://m.youtube.com/watch?v=xA0v74BysbU
 
Sasa baba na baba wadogo hawajatokea nini kimeshindikana?
Mtoto wa kike huwa ni mtoto wa Baba, ila akibikriwa tu, mapenzi kwa baba yanahamia kwa wanaomkunja. Kama binti alibikriwa akiwa mdogo less than 18 (ambayo ni kawaida kwa watoto wa singo mum), hawezi kumfikiria baba hata mara moja na vile hajawahi kukutana naye.
 
Back
Top Bottom