Strong ladg
JF-Expert Member
- Jul 15, 2021
- 1,357
- 3,114
Nina visa viwili ambapo watoto wametafuta baba zao ukubwani. Wa kwanza baba yake alifariki wakati mimba ya huyo kijana ina miezi sita mwaka 1966 kwa ajali ya pikipiki na mama akauchuna.
Mtoto alipojitambua, kama kawaida akamuuliza mama yake biological baba. Mama akawa anazungusha zungusha ila anamueleza kuwa baba yako alifariki katika ajali ya pikipiki. Kila wakati kijana hakuacha kumuuliza ili ajue ukoo wake halisi.
Miaka 10 iliyopita, mama yake alikuwa mgonjwa hoi kitandani! akamweleza mama yake kuwa pamoja na kwamba unaumwa mama, ila la kukutokea likikutokea na hujanieleza baba alikuwa nani, sitakusamehe maisha yangu yote. Mama akafunguka kuwa baba yako alikuwa fulani, alifariki wakati yupo njiani kuja kunitembelea na mimi nilikuwa mpango wake wa kando (mchepuko). Ndiyo maana sikuona umuhimu wa kujitambulisha wakati alipofariki. Ndugu zake walikuwa fulani na fulani wanaishi 150 KM kutoka hapa.
Kesho yake akamchukua mke wake na watoto wake (bahati ashakuwa hata na usafiri wake) wakapiga hodi kwa Baba yake mdogo. Jambo la muhimu alilomweleza baba yake mdogo alisema mimi ni mtoto wenu na nilikuwa natafuta ndugu zangu na ukoo wetu. Sihitaji mali au kitu maana najitosheleza ila nilipungukiwa ukoo wetu. Huwezi amini kwa sasa ndiye mwenyekiti wa ukoo, alivyo committed na ukoo wao.
Wa pili ambapo ni kijana wa rafiki yangu, hii ni ya juzi tu. Jamaa alikuwa na mchepuko wake Songea kwa akina cocastic ! akihudumu TRA Songea Mjini enzi hizo. Mchepuko ulitaka ndoa, jamaa akamweleza ukweli kuwa hana mpango. Kwa vile mchepuko ulikuwa unaisaka ndoa, ukapata muoaji lakini ukiwa na mimba ya miezi mitatu. As usual ukauchuna mtoto kazaliwa ndani ya ndoa! Washaku unawafahamu wakapiga mahesabu na wakiangalia sura wanaona ni copy right ya jamaa aliyekuwa anafanya kazi TRA. Nao wakauchuna.
Mchepu wa jamaa alizaa na mume wake wa ndoa watoto 5 na yeye wa sita. Mama yake akafriki, baba yake akaanza kumtenga tenga wakati yupo Sekondari, maana sura zilikuwa zinatofautiana na wadogo zake. Washaku wakajitokeza na kumweleza kuwa unatengwa kwa vile wewe siyo mtoto wake wa kibailojia ila baba yako yupo TRA Dar anaitwa fulani (walikuwa ni manesi wenzake na mama yake).
Akiwa form six, akajikusanya na kupata nauli toka Songea hadi Dar. Siku moja jamaa yangu yupo ofisini, sekretari kaleta taarifa kwa boss, kuwa kuna mgeni kijana. Kijana akajitambulisha mimi ni mtoto wako. Jamaa alisituka huwezi amini. Ni story ndefu lakini sasa jamaa yangu kaisha mtambulisha kwa familia na ukoo.
Naomba msinipige mawe sisi ni wapenzi wa michepuko ndiyo maana hata mimi sijifichi na Lamomy wangu pamoja na kusema hawezi kuhifadhi takataka mwilini mwake. Sijui mtoto atapatikanaje?
Hebu angalia Mfano wa binti alivyotafuta ujombani, ili mjifunze binadamu wanavyoishi
View: https://m.youtube.com/watch?v=xA0v74BysbU
Mkuu,hiyo bado haiondoki wajibu wa baba kumtafuta mwanaye au angalau kuwaambia watu kwamba nilizaa na mwanamke fulani,nikifa mkamuangalie mwanangu.Mzazi ndo anamleta mtoto duniani,yeye ndo ana wajibu mkubwa kwa mtoto,na sio mtoto mwenye wajibu mkubwa kwa mzazi. Kama mzazi hakuwahi kujitambulisha kwa mtoto,mtoto anaweza kuamua kumtafuta au kutomtafuta,hayo ni maamuzi binafsi ya mtoto na yanapaswa kuheshimiwa.