Strong ladg
JF-Expert Member
- Jul 15, 2021
- 1,357
- 3,114
Mkuu,hiyo bado haiondoki wajibu wa baba kumtafuta mwanaye au angalau kuwaambia watu kwamba nilizaa na mwanamke fulani,nikifa mkamuangalie mwanangu.Mzazi ndo anamleta mtoto duniani,yeye ndo ana wajibu mkubwa kwa mtoto,na sio mtoto mwenye wajibu mkubwa kwa mzazi. Kama mzazi hakuwahi kujitambulisha kwa mtoto,mtoto anaweza kuamua kumtafuta au kutomtafuta,hayo ni maamuzi binafsi ya mtoto na yanapaswa kuheshimiwa.Nina visa viwili ambapo watoto wametafuta baba zao ukubwani. Wa kwanza baba yake alifariki wakati mimba ya huyo kijana ina miezi sita mwaka 1966 kwa ajali ya pikipiki na mama akauchuna.
Mtoto alipojitambua, kama kawaida akamuuliza mama yake biological baba. Mama akawa anazungusha zungusha ila anamueleza kuwa baba yako alifariki katika ajali ya pikipiki. Kila wakati kijana hakuacha kumuuliza ili ajue ukoo wake halisi.
Miaka 10 iliyopita, mama yake alikuwa mgonjwa hoi kitandani! akamweleza mama yake kuwa pamoja na kwamba unaumwa mama, ila la kukutokea likikutokea na hujanieleza baba alikuwa nani, sitakusamehe maisha yangu yote. Mama akafunguka kuwa baba yako alikuwa fulani, alifariki wakati yupo njiani kuja kunitembelea na mimi nilikuwa mpango wake wa kando (mchepuko). Ndiyo maana sikuona umuhimu wa kujitambulisha wakati alipofariki. Ndugu zake walikuwa fulani na fulani wanaishi 150 KM kutoka hapa.
Kesho yake akamchukua mke wake na watoto wake (bahati ashakuwa hata na usafiri wake) wakapiga hodi kwa Baba yake mdogo. Jambo la muhimu alilomweleza baba yake mdogo alisema mimi ni mtoto wenu na nilikuwa natafuta ndugu zangu na ukoo wetu. Sihitaji mali au kitu maana najitosheleza ila nilipungukiwa ukoo wetu. Huwezi amini kwa sasa ndiye mwenyekiti wa ukoo, alivyo committed na ukoo wao.
Wa pili ambapo ni kijana wa rafiki yangu, hii ni ya juzi tu. Jamaa alikuwa na mchepuko wake Songea kwa akina cocastic ! akihudumu TRA Songea Mjini enzi hizo. Mchepuko ulitaka ndoa, jamaa akamweleza ukweli kuwa hana mpango. Kwa vile mchepuko ulikuwa unaisaka ndoa, ukapata muoaji lakini ukiwa na mimba ya miezi mitatu. As usual ukauchuna mtoto kazaliwa ndani ya ndoa! Washaku unawafahamu wakapiga mahesabu na wakiangalia sura wanaona ni copy right ya jamaa aliyekuwa anafanya kazi TRA. Nao wakauchuna.
Mchepu wa jamaa alizaa na mume wake wa ndoa watoto 5 na yeye wa sita. Mama yake akafriki, baba yake akaanza kumtenga tenga wakati yupo Sekondari, maana sura zilikuwa zinatofautiana na wadogo zake. Washaku wakajitokeza na kumweleza kuwa unatengwa kwa vile wewe siyo mtoto wake wa kibailojia ila baba yako yupo TRA Dar anaitwa fulani (walikuwa ni manesi wenzake na mama yake).
Akiwa form six, akajikusanya na kupata nauli toka Songea hadi Dar. Siku moja jamaa yangu yupo ofisini, sekretari kaleta taarifa kwa boss, kuwa kuna mgeni kijana. Kijana akajitambulisha mimi ni mtoto wako. Jamaa alisituka huwezi amini. Ni story ndefu lakini sasa jamaa yangu kaisha mtambulisha kwa familia na ukoo.
Naomba msinipige mawe sisi ni wapenzi wa michepuko ndiyo maana hata mimi sijifichi na Lamomy wangu pamoja na kusema hawezi kuhifadhi takataka mwilini mwake. Sijui mtoto atapatikanaje?
Hebu angalia Mfano wa binti alivyotafuta ujombani, ili mjifunze binadamu wanavyoishi
View: https://m.youtube.com/watch?v=xA0v74BysbU
Nakubaliana na wewe ila nimetoa scenario ambayo baba hajui! Na nina mifano ambapo baba anajitahidi kuwa karibu na mtoto wake lakini mama anaweka vipingamizi hadi baba anakata tamaa. Unaambiwa kama unanipenda mtoto, lazima kwanza unipende mimi, wakati huo Unaona hakuna future na huyo mama! Mama yeye anakuona ATM wakati hujafika pahala etc au unamfumania si mara moja. Kiboko anakuchapia mtoto.Mkuu,hiyo bado haiondoki wajibu wa baba kumtafuta mwanaye au angalau kuwaambia watu kwamba nilizaa na mwanamke fulani,nikifa mkamuangalie mwanangu.Mzazi ndo anamleta mtoto duniani,yeye ndo ana wajibu mkubwa kwa mtoto,na sio mtoto mwenye wajibu mkubwa kwa mzazi. Kama mzazi hakuwahi kujitambulisha kwa mtoto,mtoto anaweza kuamua kumtafuta au kutomtafuta,hayo ni maamuzi binafsi ya mtoto na yanapaswa kuheshimiwa.
Kwa kweli huu uzi wadau wanepaniki, sijashuhudia panic ya hivi mda mrefu sana.Khs suala la single mothers kujaa humu h n uhakika 95%
Binafsi sijaona tatizo kwenye hii mada, na hata kama kuna tatizo bc sio kupelekea kupata hizi comments za waja humu mana naona zimejaa makasiriko mengi kupitiliza.
Ukiingia nyumba ya hivyo, possibility ya wewe kuachana na huyo mke ni 80% au zaidi.Hahahaha,Kuna Moja hiyo imefungwa juzi juzi, yaani kuanzia Mama wa bi harusi , Single mother,, mama wadogo nao single mother wako wa 4 wote single mother, Shangazi Yao mkubwa naye single mother, usikute ndio hii unayosema Mkuu
Hata Mimi naona Hivyo, maana ana mifano hai mingi tuUkiingia nyumba ya hivyo, possibility ya wewe kuachana na huyo mke ni 80% au zaidi.
Kuoa familia iliyojaa single parents kunatoa uwezekano mkubwa wa hiyo ndoa kufa kibudu.
Hawa ndio wachawi wenyewe,Acha ukuda umealikwa kwenye harusi hata msosi hujala tayari unaanza kumsema bibi harusi aone aibu
Aibu unaona wewe
Duh,Nipo kwenye harusi upande wa bibi harusi meza kuu hakuna baba,wala baba wadogo wala wakubwa meza kuu wapo mama mama wadogo wajomba watoto wa wajamba kaka zake na dada zake tu
mean kijana kaenda kuoa binti alielelewa na single mother na hakuwa na mahusiano mazuri na baba zake
Mtoa mada kusema single mother na products zake zimevamia uzi wake yupo sahihi 100%Kwa kweli huu uzi wadau wanepaniki, sijashuhudia panic ya hivi mda mrefu sana.
Hata hivyo, mleta mada yupo sahihi, sherehe kufanyika huku upande mmoja hauonekani, hata kijana anayeoa kama yupo timamu lazima ajihoji, nini hiki?
Sema, kwa dunia ya leo single parenting ndio fashion, usishangae watu wakipanic.
Ndio mkuu,Hata Mimi naona Hivyo, maana ana mifano hai mingi tu
Sio poa mkuu,Mtoa mada kusema single mother na products zake zimevamia uzi wake yupo sahihi 100%
Raia wamepanic kwa kitu cha ajabu mno
Hapo ndoa ikipata changamoto inaeza kwenda na maji,na sijui siku ya harusi walitoa wosia gani kwa Bibi harusiNdio mkuu,
Unaoa familia mama ni single, mama wadogo na wakubwa wote ni singles, unadhani ndoa ikipitia misukosuko nani atakuja kuwapa ushauri wa kujenga?
Ukitaka mke hiyo ni moja ya vigezo vya kuangalia.
Aibu ya nini sasa,
Watu wasiolewe kisa baba hakutimiza majukumu yake
Hivi kwa mfano kama kijana alipatikana kwa one night stand na mama yake hakuwahi kuwasiliana tena na baba yake wala hajulikani alipo alipaswa kufanyaje?Kwa kweli huu uzi wadau wanepaniki, sijashuhudia panic ya hivi mda mrefu sana.
Hata hivyo, mleta mada yupo sahihi, sherehe kufanyika huku upande mmoja hauonekani, hata kijana anayeoa kama yupo timamu lazima ajihoji, nini hiki?
Sema, kwa dunia ya leo single parenting ndio fashion, usishangae watu wakipanic.
Kwa hiyo unafikiria mke wako akiwa anachepuka analiwa nje baba mkwe na ndugu waliooa ndio watakusaidia kuifanya ndoa yako isivunjike?!Ndio mkuu,
Unaoa familia mama ni single, mama wadogo na wakubwa wote ni singles, unadhani ndoa ikipitia misukosuko nani atakuja kuwapa ushauri wa kujenga?
Ukitaka mke hiyo ni moja ya vigezo vya kuangalia.
Umeshasema mtoto alipatikana kwa one night stand, ni aibu hata kuismbia jamii achilia mbali kumwambia mtoto.Hivi kwa mfano kama kijana alipatikana kwa one night stand na mama yake hakuwahi kuwasiliana tena na baba yake wala hajulikani alipo alipaswa kufanyaje?
Ikiwa baba yake alimkataa na hawana mawasiliano yoyote na upande wa baba yake unataka ufanyaje?
Umefikiria pia labda baba yake alifariki ndugu zake wakawadhulumu urithi wao wakaamua kuachana nao kabisa?
Mbona scenarios ziko nyingi mkuu! Tanzania ni nchi ya watu milioni 75, nafikiri wengi wanaohoji au kushangazwa na hili jambo wanafikiria katika level ya mtaa au kijiji zaidi.
Kuna mahali ndoa inahitaji testimonies za wanaokuzunguka, unafanya makosa ila ukiangalia familia yako, ndugu zako unaona mbona nazingua, familia yangu wote wametulizana, why not me. Ila unaangalia dada zako, kaka, wajomba, nk wengi walishaachana, nani anakupa motisha kupigania ndoa yako?Kwa hiyo unafikiria mke wako akiwa anachepuka analiwa nje baba mkwe na ndugu waliooa ndio watakusaidia kuifanya ndoa yako isivunjike?!