Kosa kubwa la Kambona lilikuwa ni hilo la kuropoka na kumwambafy, hata kama ndiyo iliyokuwa imani yake, alitakiwa atumie diplomacy ili ashawishi vinginevyo. Katika kipindi hicho Kambona alikuwa akiaminiwa na kusikilizwa sana na Nyerere; ndiye aliyemshawishi Nyerere kuingia Muungano na Zanzibar. Iwapo angetulia na kumwambia Nyerere hebu tukae tuongee hili jambo kwa kina kabla hatujalitoa huenda mambo yasingekuwa hivyo ilivyotokea.
Kuna watu wengi hawajui kuwa sababu moja kubwa iliyoletea azimio hilo la Arusha ni huo huo Muungano na Zanzibar, ambao Kambona aliusimamia sana. Baada ya Muungano kukatokea matukio mawili yalioyobadilisha mawazo ya Nyerere forever. La Kwanza ilikuwa ni amri ya Ujerumani Magharibi kwa Nyerere kuwa awatimue Ujerumani Mashariki na China ambao kwa kupitia Babu walikuwa na miradi huko Zanzibar; tena kwa vitisho vya kukatiwa misaada, yaani Nyere akaona kuwa sovereignty ya nchi inaingiliwa. La pili lilikuwa ni lile la marekani kuleta spy wao Mr Carucci kuwa mshauri wa Karume huku akiwa amemaliza kazi ya kumwua Patrice Lumumba huko Kongo; bwana huyu akaleta masharti yale yale ya kufukuza nchi za kikomunist tena kwa vitisho vya misaada vile vile. Kwa wale waliozaliwa wakati wa digitali, huenda hawajui kuwa kuna barabara zilizokuwa zinajengwa na Ujerumani Magharibi pale Dar es salaam zilivunjwa vunjwa na wajerumai hao kabla hawajaondoka, matanegezo ya hospitali ya Ocean road pia yalivunjwa na wajerumani waliokuwa wakiijenga upya. Kitu kimoja ambacho hawakuvunja ni Ukumbi wa Nkurmah nadhani kwa vile Nyerere aliamua kuwatiimua mara moja baada ya kuanza bomboa bomoa yao, hata hivyo hawakuumaliza ukumbi huo kama ulivyokuwa umesanifiwa.
Matukio hayo ndiyo yaliyoleta siasa ya kujitegemea: Nyerere akasema kuwa "Kujitawala ni kujitegemea; kujitawala kwa kweli hakuwezekani iwapo taifa moja linategemea misaada na mikopo ya taifa jingine kwa maendeleo yake." Miiko ya uongozi iliongezewa kwenye azimio lakini lengo kubwa ilikuwa ni kuweka mwamko wa wananchi kujituma na kujitegema. Kukawa msemo kuwa usiwe kupe jitegee.