Mimi sipendi kelele ya aina yoyote. Connection niliyonayo ni ya watu ninaofanya nao kazi. Sikuwa mzungumzaji tangu nilivyokuwa shule. Wengine waliniita mkimya, wengine waliniita kauzu. Wengine wakasema huyu wakishua hapendi bughudha na watu.
Starehe yangu muvi, kucheza game, kula na sasa hivi nina plan ya kujifunza kutembelea mbuga na hata mikoa tofauti kwa kutumia likizo zangu ili nijifunze zaidi kuhusu mazingira na maisha kwa ujumla. Imenifanya muda wangu mwingi nimekuwa najifunza mambo tofauti na kusoma vitabu tofauti vya dini vya maarifa na kuhusu mambo mbalimbali.
Vipindi ninavyovipenda unaweza ukaniita dingi! Taarifa ya habari, channel inayoitwa Investigation Discovery, National Geographic, Beyond Belief: Fact or Fiction tangu 2008 nilikuwa naitizama, mpenzi wa You Tube channel zinazohusu watu wanaofanya kilimo na ufugaji wa kuku. Vipindi vinavyohusu ujenzi wa nyumba. Napenda science pia! Imenifanya nawaza tofauti.
Kingine nipo real tu sifeki maisha. Na imenifanya mambo ya ujana mengi siyajui. Sisikilizi radio naona wanachokizungumza si ninachokitaka. Nimeacha kusikiliza tangu 2012 au 2013! Naona wanazungumza ujinga tu na mimi nahitaji vitu vitakavyonijenga.
Kingine imenifanya nafocus kwenye kujenga maisha na kuyafanya yawe bora zaidi. Sipendi ujinga! Sifuatilii mtu labda awe kafanya kitu kinachoigusa jamii ndiyo nitachungulia. Sishoboki na mtu. Hata nikijihisi mpweke kinachonitoa upweke ni kwenda mahali kukaa peke yangu sihitaji bughdha na mtu.
Kingine naamini Mungu yupo. Inanipa amani na furaha ndani ya moyo kwa sababu napenda kumkumbuka.