Hasara zipi unazipitia kwa kuwa na tabia za introvert?

Umeniacha na viulizo! Hongera kwa maana ipi?
Oh hongera yangu imelenga hayo maelezo yako yote mkuu. Hata Mimi Niko hivyo pia, na kwa miaka mingi nilikuwa sijui kwa nini Niko hivi, hadi nilipoona uzi umeandikwa na Da'Vinci kuhusu " Jinsi introverts wanavyopata shida kujichanganya na jamii/watu" ndipo nilipoelewa kwa nini Niko hivi.

Naam, imenipa kujikubali na kujiamini mno, sina rafiki, na maishani mwangu naweza kusema nimewahi kuwa na marafiki wawiki tu, ila wengine tunaongea kidogo tu, ndio imeisha. Mkuu kuna mengi mno, ila kama maelezo yako yalivyo, ni ndivyo na Mimi nilivyo. Nafurahi mno kuwa hivi, kwa sababu mpaka sasa naona Mungu ameniapusha na mambo mengi ambayo naona ni uovu, naam, hivyo nikiona mtu yuko kama maelezo yako,...nafurahi mno kuona na kusoma maelezo kama yako, maana yananipa raha.

Naam!!!
 
Wale ma-introvert tukutane kwenye hiki kitabu

introvert power

Here's the link to the file:

Shared from WPS Office:
 
Oh hongera yangu imelenga hayo maelezo yako yote mkuu. Hata Mimi Niko hivyo pia, na kwa miaka mingi nilikuwa sijui kwa nini Niko hivi, hadi nilipoona uzi umeandikwa na Da'Vinci kuhusu " Jinsi introverts wanavyopata shida kujichanganya na jamii/watu" ndipo nilipoelewa kwa nini Niko hivi.

Naam, imenipa kujikubali na kujiamini mno, sina rafiki, na maishani mwangu naweza kusema nimewahi kuwa na marafiki wawiki tu, ila wengine tunaongea kidogo tu, ndio imeisha. Mkuu kuna mengi mno, ila kama maelezo yako yalivyo, ni ndivyo na Mimi nilivyo. Nafurahi mno kuwa hivi, kwa sababu mpaka sasa naona Mungu ameniapusha na mambo mengi ambayo naona ni uovu, naam, hivyo nikiona mtu yuko kama maelezo yako,...nafurahi mno kuona na kusoma maelezo kama yako, maana yananipa raha.

Naam!!!
Duniani wawili wawili, shukrani.
 
hii dunia wote wangekua intro maisha yangekua na furaha sana, intro ni watu wasio na wivu negative wa maendeleo, hawapendi majungu, wanapenda kukeep busy na mambo yao na nk.... kuna muda hutamani kungekua na makazi ya intro pekee ili wawe huru kuuishi uhalisia wa tabia zao.
 
Sahihi mkuu.

Na mimi nina machache ya kuelezea lakini naona inatosha kuyasoma ya wadau.

Muhimu naona kuwa watu sisi wenye tabia hizi tutumie muda wetu kujinufaisha zaidi kuliko mtu anakaa peke yake huku akifanya ujinga.

Tabia ya kukaa peke yangu imenifanya niwe mtu wa kuwaza tofauti sana,na hili nalishuhudia kwa watu wangu ambao wamekuwa wakinitegemea katika mawazo wakati wao ni watu wazima.

Kwa kweli hii tabia ni nzuri sana,japokuwa mimi nina rafiki angu
Kuna jamaa mmoja nilikutana nae katika ngazi za kielimu baada ya kunigundua jinsi nilivyo akaniambia "hukufaa kuishi kwenye hii karne! Karne hii si yako!! Karne za nyuma zingekufaa zaidi"

Aliniona si mtu wa kuwazungumzia watu na sipendi umbea. Nikitoka hostel asubuhi narudi jioni. Si mtu wa wanawake, sinywi pombe, sivuti sigara. Vipindi vya TV walivyokuwa wanaangalia wao mimi nilikuwa siviangalii nipo zangu chumbani. Si mtu wa starehe zinazopendwa na watu wanazoziita starehe. Si mtu wa kuvimba, ni simple man.

Sijali watu watanichukuliaje kimuonekano kwa sababu maisha ni mimi na mimi ndiye ninaejijua nipoje (kifedha). Maadamu najijua nipoje basi inanitosheleza mwenye moyoni mwangu. Kwa hiyo atakaye ni-define nipo hivi ama vile ni yeye mwenyewe ndiye ameni define na mimi simjaji.

Naamini katika nidhamu. Jamii ikiguswa na mimi naguswa, naweza nisionekane mtaani lakini yakitokea masuala ya ushirika wa kijamii nipo nitashiriki na halikadhalika nilikuwa hivyo hivyo hostel.

Ghafla tu kwa hiyo hali wengine wakawa wananiogopa. Wengine wakinifuata wananijia kwa nidhamu. Jamaa akaniambia hii karne haikufai.
 
Kuchoka kuwa introvert ni Sawa na kuuchoka uasilia wako,unaweza jaribu kujibadili ila mwisho wa siku unajikuta peke yako pasipo kupenda
Me mpaka Leo zaidi ya mika 24 cjawai kuwa na mpenzi/demu nikijaribu kutafuta mpenzi kunamaswali huwa najiuliza na kujijibu mwisho Siku zinaenda hvhv
Una cheo gani chaputa mkuu??
 
Kuna jamaa mmoja nilikutana nae katika ngazi za kielimu baada ya kunigundua jinsi nilivyo akaniambia "hukufaa kuishi kwenye hii karne! Karne hii si yako!! Karne za nyuma zingekufaa zaidi"

Aliniona si mtu wa kuwazungumzia watu na sipendi umbea. Nikitoka hostel asubuhi narudi jioni. Si mtu wa wanawake, sinywi pombe, sivuti sigara. Vipindi vya TV walivyokuwa wanaangalia wao mimi nilikuwa siviangalii nipo zangu chumbani. Si mtu wa starehe zinazopendwa na watu wanazoziita starehe. Si mtu wa kuvimba, ni simple man.

Sijali watu watanichukuliaje kimuonekano kwa sababu maisha ni mimi na mimi ndiye ninaejijua nipoje (kifedha). Maadamu najijua nipoje basi inanitosheleza mwenye moyoni mwangu. Kwa hiyo atakaye ni-define nipo hivi ama vile ni yeye mwenyewe ndiye ameni define na mimi simjaji.

Naamini katika nidhamu. Jamii ikiguswa na mimi naguswa, naweza nisionekane mtaani lakini yakitokea masuala ya ushirika wa kijamii nipo nitashiriki na halikadhalika nilikuwa hivyo hivyo hostel.

Ghafla tu kwa hiyo hali wengine wakawa wananiogopa. Wengine wakinifuata wananijia kwa nidhamu. Jamaa akaniambia hii karne haikufai.
Mkuu wiki chache nyuma nilikuwa na jamaa mmoja kanipa lifti kwenye gari yake nakaa nae mtaa mmoja.

Kwenye gari jamaa ananiambia kwamba safuher wewe pale mtaani huna rafiki sikuoni maskani kabisa uko na mambo yako kabisa.

Nikamuambia hamna kaka nakuwepo maskani sema hatuonani tu,jamaa kaniambia hamna wewe uko bize na yako sikuoni maskani,namimi nikamshikilia hapo hapo kwamba nakuwepo pale kitaa.

Nikajiuliza kwamba hivi kumbe kuna watu nao huwa wananiona.
Mimi mara nyingi huwa nahisi kwamba watu hawana habari na mimi kabisa,kumbe bhana watu huwa wanaongea kuhusu wewe.

Kuna jamaa alinambia kwamba aaaah wewe changamana na watu sijui hivi na vile,nikamuambia kwamba mimi ninachohitaji ni kuishi vizuri na watu na sio kuishi muda wote na watu.

Hata kama tunaonana mwezi mara moja na wewe basi hitajio langu ni kwamba hio mara moja tuongee vizuri na sio kila muda tupo wote tuu.

Basi ni changamoto tu mkuu
 
Hapa nilipo najisikia kuumwa ila sitaki kumwambia mtu yoyote na ninaishi mwenyewe ni zile nyumba za kuonana kwa bahati nasibu sana majirani. Kuna demu anataka aje leo ila sijisikii kuwa na mtu mwingine ndani.

Ila ninavyowala hawa mademu! Na mpaka leo sijui kutongoza.
 
Tabia ya kupenda kukaa peke yangu bila kuwa na mazoea sana na washakaji ama majirani, kuna siku niliumwa wakuu nikakaa ndani siku nzima nakunywa maji tu hakuna anayejua kama naumwa.

Homa ilinikamata vibaya nje sionekani washakaji na majirani wakajua ndio kawaida yangu kuwa ndani kumbe mwenzao maji ya shingo, niko mbali na familia, wife hayupo.

Nikapiga simu kwa wife, wife akasema huyu jamaa atakufa kwa sababu ananijua sina kampani, wife akasafiri kesho yake akaja ndio ikawa afadhali yanguhayo maana ugonjwa ukiwa peke yako unazidi.

Nikasema nikipona mimi jamani ntatafuta washkaji wa kutembeleana ili nikipata matatizo nisaidiwe, baada ya wiki kupona ndio kwanza nikazidi kujichimbia ndani na vitabu vyangu uchwara😀😀😀

Nashauri wakuu tujitahidini kuwa na watu wa karibu washkaji ama majirani, mimi imenishinda kidogo.

Tabia ya kupenda kukaa peke yangu bila kuwa na mazoea sana na washakaji ama majirani, kuna siku niliumwa wakuu nikakaa ndani siku nzima nakunywa maji tu hakuna anayejua kama naumwa.

Homa ilinikamata vibaya nje sionekani washakaji na majirani wakajua ndio kawaida yangu kuwa ndani kumbe mwenzao maji ya shingo, niko mbali na familia, wife hayupo.

Nikapiga simu kwa wife, wife akasema huyu jamaa atakufa kwa sababu ananijua sina kampani, wife akasafiri kesho yake akaja ndio ikawa afadhali yangu maana ugonjwa ukiwa peke yako unazidi.

Nikasema nikipona mimi jamani ntatafuta washkaji wa kutembeleana ili nikipata matatizo nisaidiwe, baada ya wiki kupona ndio kwanza nikazidi kujichimbia ndani na vitabu vyangu uchwara😀😀😀

Nashauri wakuu tujitahidini kuwa na watu wa karibu washkaji ama majirani, mimi imenishinda kidogo.
Inabidi ujikubali kuwa ndivyo ulivyo na unatakiwa kuishi hivyo. Ni maumbile na mimi niko kama wewe ila nimejikubali
 
Saivi sihangaiki na vile nilivyo.

Ninachofurahi hata mke eangu naye sio mtu wa vijiwe ama vibaraza na marafiki,naweza kaa na wife home siku nzima tunapiga story tunasahau hasa kama sie ni mke na mume.
 
Aisee hongera kwa kupata mnayeivana, maana "zodiac signs" zinaogofya...ukipata mtu ambaye hamuendani.
 
mimi ndo najiona nina matatizo kabisa sipendi kuwa na watu npo radhi nkakae porini nisikie sauti za ndege na wanyama huku nasoma vitabu ila watu sitaki mazoea nao nina watu wachache sana wamuhimu hawazidi watano.
We upo km mimi, mi nataka maisha flani ya tarzani ila basi tu yani. Nikipata pesa nyingi nitaenda zangu porini huko kuanzisha familia.
 
Hasara kubwa wanayopataga ni kukosa opportunities mbali mbali kama Job promotion/opportunity, kukosa wenzi sahihi, kukosa connection mbali mbali N.K.
Hawa sijui introvert ndo watu gani aisee naombeni mnisaidie maan hili neno si geni na kila mtu anazungumza anavyojua.
 
Ni aina ya watu ambao sio wakujichanganya na watu wengine katika muda wao wa free
 
Back
Top Bottom