Hashimu Rungwe: Magufuli alikuwa anaimba viwanda lakini hakujenga hata kimoja

Hashimu Rungwe: Magufuli alikuwa anaimba viwanda lakini hakujenga hata kimoja

Mi nafikiri kwa "busara yako kubwa", ungemjibu Mzee Rungwe kwa kutaja viwanda alivyojenga Magufuli katika miaka yake 5. Badala yake unatoa lawama ambazo hazina msingi. Jibu hoja kwa hoja, siyo porojo.
Nawasikitikia Sana wajukuu zake maana kumuita Babu mtu kama huyu ni aibu, ninachojua mpaka mtu astahili kuitwa Babu anatakiwa kuonesha kiwango cha hekima na busara kisichotiliwa shaka.

Mzee Rungwe leo kadhalilisha wazee wenye rika Kama lake bora angekaa kimya tusingejua uzee wake
 
Alisema inajenga siyo imejenga, mnamponda marehemu wakati hata nyinyi kiswahili kinawapiga chenga.Hili swali aulizwe mama viko wapi viwanda vilivyokuwa vinajengwa na marehemu?
 
Dah...Kwa Umri Wake Yule Mzee hakika ilikuwa ndo awe Mfano wa Wapinzani Makini, Lkn Kila nikimwangalia Sioni Uwakilishi Wa Upinzani makini...!
Nadhani hata Yeye Mwenyewe Kajiweka Kundi La Upinzani Wa jokes ndo Mana Kwenye Kampeni zake Alikuwa anatembea na MAHOTIPOTI Ya Ubwabwa.
Yawezekana Hakuna Kiwanda Kilichokamilika...Lkn ni Kweli Vyote vilivyokuwepo kwenye Ilani ya chama Hakuna kilichokamilika...!
Ipo haja Kuomba Mungu wakati Unazeeka Uzeeke Vizuri.
Acha porojo,tuonyeshe kiwanda hata kimoja.
 
Alisema inajenga siyo imejenga, mnamponda marehemu wakati hata nyinyi kiswahili kinawapiga chenga.Hili swali aulizwe mama viko wapi viwanda vilivyokuwa vinajengwa na marehemu?
Kabla hatujamuuliza huyo mama utueleze hivyo viwanda vilivyokuwa vinajengwa viko wapi. Kwamba tangu 2015 mpaka 2021 alikuwa anavijenga bado, viko wapi na vilitarajiwa kukamilika lini
 
Kabla hatujamuuliza huyo mama utueleze hivyo viwanda vilivyokuwa vinajengwa viko wapi. Kwamba tangu 2015 mpaka 2021 alikuwa anavijenga bado, viko wapi na vilitarajiwa kukamilika lini
Vipo Tanzania.Vinatarajiwa kukamilika lini aulizwe muheshimiwa Samia.
 
Back
Top Bottom