Hassan Mwakinyo apoteza kwa T.K.O dhidi ya Liam Smith | M&S Bank Arena | Liverpool

Hassan Mwakinyo apoteza kwa T.K.O dhidi ya Liam Smith | M&S Bank Arena | Liverpool

Ndondi ukiwa nyumbani na ukafanikiwa kutoboa raundi zote wewe moja kwa ni mshindi ata kama uko mwanzo ulipokea ngumi nzito. Njia rahisi ya mgeni kushinda ni ashinde kwa KO
Mkuu bora soccar tu, huu mchezo wa ngumi nawaachia watemi.
Maana kwenye mchezo wa ngumi kila mtu ni mtemi, kuanzia mchezaji, makocha, refa mpaka mashabiki.

Ndio maana akili zao zinashindwa kuamua vizuri mpaka leo.

Hivi watu wanagombea kombe (mkanda) la kimataifa, alafu mpinzani mmoja anapambana kwao, hivi huoni upendeleo hapo.

Kwanini wasipeleke nchi ngeni kwa kila mmoja?
Mfano pambano lingefanyika hata India, ama nchi yeyote ya Amerka kusini, lakini hawa wapuuzi wameamua game ifanyike England nyumbani kwao Liam Smith tena ndani ya jiji alilo zaliwa (Liverpool) kama sio mchongo ni nini?

Bubu, ngumi ni mchezo wa kiduanzi kuwahi kutokea Duniani
 
Watu wamekosa burudani,awe makini wasimshuti na pipe,mbona alitoka pasipo kuchechemea kama issue ni mguu
 
kaweka video kule instagram anasema alipoteza begi airport eti ndio ikabidi apewe viatu vingine hiyu dogo lipo jambo nyuma ya pazia , how come upoteze begi airport kama sio usanii huu
 
Ngumi haziko kama unavyofikiria.Pale Kila bondia alikua na tahadhari kumsoma mpinzani wake kwa kupiga kwakushtukiza uku wakijilinda zaidi .Kwahiyo ni lazima uone sio mzuri ila nenda Youtube ukaone clip zake.pambano lingechanganya kwenye round ya nane kuendelea ndo tungeona ubora wao.
Wewe unazungumzia historia, mimi nazungumzia current forms ktk pambano la leo.

Achana na historia zungumzia, pambano hili la leo.Hata Joshua clip zake YouTube zina vutia ila bado akapigwa.
 
Ashajitetea huku kua kapewa kiatu kibovu . Na hata alipotema mouth guard refa hakusimamisha pambano.
 
Uzuri hadi pambano lilipokuwa limefikia Home noy alikua na credit za kutosha tu na kama hali ingeendelea vile mzungu asingefika raundi ya kumi

Labda kosa la mwakinyo ni kupanda na viatu hivyo ulingoni.kwani alipovivaa hakuisikia hali hiyo mwanzo?
Na hili liwe funzo we umepoteza viatu vyako unasubiria vya kuletewa pasipo kufikiria fitness yake kwanza?

Kweli huku kijichi tumekua dis appointed kwa namna pambano lilivyoisha sababu ulikua ukienda vizuri tu.mwanzo tukajua ni maji walimwaga ili uteleze!

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
 
kaweka video kule instagram anasema alipoteza begi airport eti ndio ikabidi apewe viatu vingine hiyu dogo lipo jambo nyuma ya pazia , how come upoteze begi airport kama sio usanii huu
Visingizio tu hivyo.
Sema nini,aache madharau kwa wenzake.
 
Mabibi na mabwana, usiku wa leo kwa masaa ya Afrika Mashariki, Bondia mtanzania, Hassan Mwakinyo atakuwa anapambana na bondia Liam Smith katika dimba la M&S Bank Arena huko jijini Liverpool.

Liam Smith ana umri wa miaka 33 huku Mwakinyo akiwa na miaka 27.

Pambano hilo limekuja muda muafaka mara baada ya Mwakinyo kuwa nje ya ulingo kwa muda mrefu.

Liam Smith amepoteza mapambano matatu tu katika career yake ya masumbwi.

Yote kwa yote, tunamtakia heri Mtanzania mwezetu Mwakinyo aibuke na ushindi na kuendelea kuitangaza vema nchi yetu.

Tukutane hapahapa jukwaani kwanzia saa 3:00 usiku kwa live updates

Pambano litakuwa mbashara Azam Sports 1HD
View attachment 2344162
====

BONDIA MWAKINYO APIGWA TKO

Bondia Hassan Mwakinyo amepoteza pambano dhidi ya Liam Smith baada ya kupigwa kwa TKO

Pambano hilo lililokuwa na mizunguko 12 limeishia mzunguko wa 4 baada ya Mwakinyo kupiga goti wakati pambano likiendelea
View attachment 2344962
View attachment 2344963

MWAKINYO: WALINIPA VIATU VILIVYOKUWA VINANIUMIZA KIFUNDO CHA MGUU

Baada ya kupoteza pambano lake dhidi ya Liam Smith, Bondia Hassan Mwakinyo ameelezea kilichotokea huku akisema yupo tayari kurudiana na mpinzani wake

Amesema alipoteza begi lake alipokuwa Uwanja wa Ndege, hivyo ilibidi Wenyeji wake wampatie viatu vingine ambavyo vilikuwa vinamfinya na kumuumiza Kifundo cha Mguu

Amesema wakati wa pambano alipokuwa anakabiliana na hali hiyo ilibidi ateme 'MouthGuard' maana Sheria za Boxing zinasema Refa anatakiwa amsimamishe mpinzani na kuliuza nini kinaendelea

Ameongeza "Aliniuliza kama naweza kuendelea, nilimjibu naweza kuendelea lakini viatu vilizidi kuniumiza Kifundo cha Mguu nikaa chini lakini mpinzani akaendelea kunipiga na pamabano likaisha hapo"

View attachment 2344965
Kila la kheri Champ! Nilijua lazima wangekufanyia hila yeyote Ile. All the best!
 
MTU anaposema tumuombee kuna kitu watanzania tujifunze kutoka kwa JPM na sasa Mwakinyo na majaji wa mahakama kule kenya

Mtanzania na Bondia Hassan Mwakinyo, amewaomba watanzania kumuombea kuelekea pambano lake la leo dhidi ya bondia, Liam Smith raia wa Uingereza.




" Ni dua zenu pekee zinaweza kunivusha hapa nilipo" ameandika Hassan Mwakinyo.
 
Wewe unazungumzia historia, mimi nazungumzia current forms ktk pambano la leo.

Achana na historia zungumzia, pambano hili la leo.Hata Joshua clip zake YouTube zina vutia ila bado akapigwa.
Kwahiyo wewe huyo mwakinyo unamwona ni mzuri kuliko huyo mzungu?.Hebu tuache kujifariji bana.
 
Back
Top Bottom