Hassan Mwakinyo ndio bora wa wakati wote hapa Tanzania. Wabongo wanataka kumshusha

Hassan Mwakinyo ndio bora wa wakati wote hapa Tanzania. Wabongo wanataka kumshusha

Aachane na Uswahili!! Jamaa ni mswahili sana, na alijiona kama hakuna mtu wa kumfanya kitu!!! Yaani ugomvi wako wa mtaani unauleta hadi kwenye mikataba ya kazi za watu!!
Uswahili ni hilka na asili yake, yeye Mtanga, mnataka afanane na Wanyakyusa au wasukuma?
Mnakerwa nini?

Huyu jamaa hana kosa lolote, roho kutu za wabongo ndio zinajitahidi kumshushs
 
View attachment 2778189

Wote tunajua kwenye mchezo wa boxing hajawai kutokea bondia mwenye uwezo wa kupigana ngumi hapa bongo kama Mwakinyo.

Dunia nzima inajua Hassan ndio alama ya boxing hapa Tanzania.
Ndio biashara kubwa ya ngumi East Africa ukitaka kufanya biashara ya ngumi na upate hela isiyo na longolongo basi mtumie Mwakinyo.

Mwakinyo kaitoa boxing kwenye fight za kwenye bar za Keko na Manzese mpaka ngumi zinapigwa Masaki.
Huwezi mpandisha Hassan ulingoni eti apiganie gari anaijua thamani yake.

Na tatizo ndio linaanzia hapo watu wanashindwa kumtumia kwa urahisi hivyo wanapigana vita ya kumpoteza.

Mnataka mpoteza Mwakinyo ili mbaki na nani?

Anachopitia Mwakinyo alishawai kukipitia Diamond.

Kuna wakati Diamond alipigwa vita na kila mtu kama sio mashabiki wake kusimama nae leo hii tungekuwa tunaongea mengine na sababu walizotoa ni hizi hizi. Anaringa sana, anajiona mkubwa, anavimba, muda wake umeisha ila aliwaprove wrong na wengine kwa sasa wapo kwenye team yake wanajifanya wanampenda kuliko ndugu zake amebaki kuwachora na kuwagawia riziki.
Mwakinyo awe makini sana na acheze game yake very smart, yupo kwenye nchi iliyojaa watu wenye chuki na roho mbaya zisizo na sababu.

Waswahili ni watu wa kuyakadilia mafanikio, kuna mstari wa mafanikio ukiuvuka hata wale waliokupeñda wanageuka kukupiga vita upotee. Huo ndio uhalisia. Na sasa Mwakinyo ana mtihani wa kupambana na ili kundi ambalo limekuwa kubwa likifanya jitihada apotee kabisa.

Tanzania ni nchi iliyojaa watu wajinga, ujinga ukaleta ugonjwa wa roho mbaya na husda na ikifika wakati wa kumuadabisha mtu mwenye mafanikio uwa wanaungana wanakuwa wamoja.

Kwa sasa asipokuwepo Mwakinyo hakuna mwingine wa kukaribia brand yake ila wenye chuki wanaona bora tubaki na kina Kaoneka. So sad ila ndio taifa letu lilivyo.

Naamini ili suala la Mwakinyo litaisha ila inabidi awe makini sana, na fight yake atayopambana hana option nyingine zaidi ya kushinda. Bila hivyo itakuwa ni sherehe kubwa kwa wenye chuki na roho mbaya.
Mwakinyo hana mkanda wowote anaoushikiria kwa sasa na pia ana nyota 2 kwa Sasa tofauti na zamani alipokuwa na nyota nne.

Thamani yake imeshuka automatically hivyo hata pesa anazozitaka haziendani na thamani yake , anataka pesa nyingi wakati thamani yake ndogo.

Nyie msiojua boxing anawapelekesha sana kwa kutoelewa kinachoendelea.
 
Umenena kweli
Wabongo wanamhukumu kijana eti anaringa kwani kuringa kosa kama anaringa na kipaji ni chake kuna shida gani?
Wanamtafutia sababu wamshushe waharibu kipaji cha kijana
Mwakinyo ni brand ameajiri watu
Ana connection za kimataifa
Anaweza kuwasaidia vijana wengine

Wanaleta ubabaishaji kijana ana exposure na international flights anakataa huo uhuni wanasema eti anaringa

Sio vizuri Mwakinyo muacheni kijana apigania ugali wake hicho chama kiwepo kusaidia vipaji na sio kukomoa na kuharibu Tallent za boxers


Sent using Jamii Forums mobile app
Mtu ana nyota ashushwe kwa lipi wakati hapo alipo tu yupo chini.

Baada ya kupigwa kijinga na Liam Smith kuna kuna baadhi ya nchi wamempiga stop kupigana kwenye nchi zao maana alidhalilisha sana boxing.
 
Hapo Baba aingie chimbo apige tizi Mwaka mzima mwakani atafute pambano amtie mtu kibano cha kufa ngamia alafu hao PAF Promotion na wengine watamuelewa maana ni njama ya muda mrefu kuhakikisha anapotea akiwaambia wafanye hivi wao wanapita hivi nilimsikiliza jamaa wa PAF nikaona sasa huyu jamaa anafanya Jambo na mtu alafu anafanya kwa kumtegea ili baadae ampeleke Mahakamani sio fair kabisa
Mwakinyo anajua ngumi atakuja kupiga mzungu mwingine ilo hakuna shaka. Ila kukabiliana na wajinga wenye chuki inabidi ajipange vizuri sana. Wanakuwaga wamoja kwenye jambo lao.
 
Uswahili ni hilka na asili yake, yeye Mtanga, mnataka afanane na Wanyakyusa au wasukuma?
Mnakerwa nini?

Huyu jamaa hana kosa lolote, roho kutu za wabongo ndio zinajitahidi kumshushs
Wanasema hawampendi ana nyodo ila fight yake ikitokea kesho kiingilio aweke laki na bado atajaza na biashara itafanyika mno.
 
Mwakinyo hana mkanda wowote anaoushikiria kwa sasa na pia ana nyota 2 kwa Sasa tofauti na zamani alipokuwa na nyota nne.

Thamani yake imeshuka automatically hivyo hata pesa anazozitaka haziendani na thamani yake , anataka pesa nyingi wakati thamani yake ndogo.

Nyie msiojua boxing anawapelekesha sana kwa kutoelewa kinachoendelea.
Akikubishia ntamshanga maana najuwa wewe boxing unaijua nje ndani
Tatizo mleta mada kila kitu anakichukulia kama mziki wa bongo
Fleva na mambo ya wasafi

Ova
 
Unavyosema Mwakinyo ni bondia bora wa muda wote unakosea.! Unamkumbuka Rashid Matumla (snake boy) alichofanya kwenye boxing huyo brazamen hajafika hata robo
Matumla kafanya nini wewe ushawai muona akipigana au ulitazama picha kwenye magazeti 😂😂😂
 
Back
Top Bottom