Hassan Rehani Bitchuka: Fundi wa muziki wa dansi, sauti ya kinanda. Yu wapi huyu mtaalam wakuu?

Huyu Mwamba Pale Sikinde alikuwa hana mfano wake..

Sikiliza Kibao cha Hiba utajua kweli huyu mwamba alikuwa ana sauti ya kipekee.

Pole nyingi kwake Mwenyezi Mungu amfanyie wepesi apate kupona.
Kweli mkuu, jitahidi pia umchangie mkuu namba yake hyo hapo juu,.
 
Aisee nimejikuta nikimkumbuka sana huyu fundi wa muziki wa dansi aliyepata kuvuma sana kwenye muziki wa dansi na nyimbo kadhaa zilizokonga vilivyo nyoyo zetu.

Yu wapi gwiji huyu?
 
Shukran sana mkuu kwa hii taarifa,
 
Bado anaumwa nilkutana na mwanae juzi amesema "Hali ya Mzee siyo nzuri bado anapambana na maradhi"
Pls mkuu, hii ya kwako ndio latest informations, unaweza elezea zaidi hali yake na the way forward kama unahitaji kuchangia kidogo, una latest number yake ya simu pls?
 
Mzee Gulumo R.I.P, wakati anahojiwa na kituo flani cha Radio wanamziki au waimbaji wake wazuri wa wakati wote yy alisema 1. Cosmass Chidumule 2. Bitchuka 3. Moshi William Tx.
 
Ambae ataweza kutupatia mawasiliano yake atakuwa amefanya jambo la maana sana.


Tujitokezeni tumsaidie wakuu,

Karibuni wote kwa suggestions zaidi.
Chacha Maginga wa TBC wanakipindi cha zilipendwa...na amekuwa akimsupport mara kwa mara kwa michango ya wadau wa music wa dansi. mnaweza kwenda TBC pale mikocheni mkamtafuta nae atawasilisha michango yenu pia mnaweza kufanya kipindi nae na kutoa michango yenu....
 
Unajua mwenzangu karibuni utatoka hospitalini,utokapo tafadhali..fika mjini ....
Huyu nafikikiri ni Maxmillian Bushoke...baba yake na Bushoke wa bonge flever
 
Pls mkuu, hii ya kwako ndio latest informations, unaweza elezea zaidi hali yake na the way forward kama unahitaji kuchangia kidogo, una latest number yake ya simu pls?
Mimi sina namba ya Mzee Bitucha ila mwanae huwa nakutana naye mara kwa mara,aliwahi kuniambia Mzee anaishi nyumbani kwake Sinza. Ngoja niulize vizuri location na itapendeza kwenda kumtembelea.

Jioni Mungu akipenda nitaleta majibu sahihi Mzee anaishi Sinza sehemu gani na kama atanipa namba ya Mzee na kuniruhusu kuweka hapa nitafanya hivyo.
 
Pls mkuu do that, thanks
 
Bitchuka anaishi Sinza mkuu yupo na mkewe hivyo ukifika pale utaweza kutoa msaada wa moja kwa moja otherwise bado sijapata nafasi yakupata contact zake...Ila yupo nyumbani kwake Sinza na anaumwa huu Ni mwaka wa pili Sasa!...
Tumsaidieni huyu legend!
Sinza mitaa ya Lion Hotel ukiuliza home kwa Bichu wanakulengesha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…