Hata Mwl Nyerere ilifikia kipindi akaitwa kiongozi asiyeambilika, lakini hatujawahi kusikia viongozi waliomfuata wakimkosoa hadharani ughaibuni

Hata Mwl Nyerere ilifikia kipindi akaitwa kiongozi asiyeambilika, lakini hatujawahi kusikia viongozi waliomfuata wakimkosoa hadharani ughaibuni

Kweli kabisa hata kipindi Hayati Magufuli anamwapisha PM Majaliwa Dodoma November 2020 (Then, VP) Samia alisema"Rais Magufuli hapo mwanzoni tulipata taabu kidogo kukuelewa lakini sasa hivi tumeelewa unachotaka"

Hii nukuu inaweza isiwe perfect in details, lakini ambao mnaweza kutafuta video YouTube mtaona Rais Samia amewahi kuonesha kwamba palikuwepo na tofauti kati ya Magufuli na watendaji wengine wa Serikali, tena aliyasemea mbele ya Magufuli.
Samia alianza kumkosoa Magufuli tangu Magu akiwa hai. Kwahiyo anayoyafanya sasa hivi siyo unafiki bali ni kutoa ya moyoni hasa anapo ona ilivyo vigumu kurekebisha uharibifu alioufanya Magu ndani na nje ya nchi.
Uharibifu aliyoufanya Magu kwenye uchaguzi wa 2020 pia anaweza kuuelezea?
 
Sijui wazungu huwa wanatuchukuliaje, Yaani wako tayari kutuona tukianguka kila leo, Matumizi ya akili ni ukombozi.
 
Mbona mkuu wa nchi yetu kama anafanya ndivyo sivyo? Kuongoza nchi kumbe kazi sana. Upo nje kwenye ziara ya kikazi alafu unaeleza kwenye media kubwa kama NY times kuwa mtangulizi wako alikuwa stubborn, hii inaleta picha gani?

Hukuwa na raha wakati unafanya nae kazi pamoja kiasi cha kumchukia kwa kutofuata ushauri wako wakati wewe ulipokuwa msaidizi wake?

Ulifanya nae kazi huku ukiwa na kinyongo maana alikuwa mkaidi?

Ina maana ulikuwa unacheka nae hadharani lakini moyoni humtaki sababu ni stubborn?

Lakini mbona hata Mwl Nyerere inasemekana wazi kabisa alikuwa mkaidi juu ya kufuata ushauri wa wasaidizi wake mpaka ilifikaia hatua akaitwa baba haambiliki, hatujawahi kusikia Mzee Mwinyi au Mkapa wakimnanga huko mamtoni?

Inasemekana alishauriwa masuala mengi tu na akakaidi, mfano aliambiwa asihamishe watu kwenye miji yao kwa ajili ya vijiji vya ujamaa lakini akawahamisha. Jambo ambalo lilileta lawama kubwa. Lakini hatikusikia akipondwa huko nje. Alishauriwa asiijifanye yeye ni superpower wa Afrika lakini akakag'ag'ania kupeleka majeshi Msumbiji, Zimbabwe na Uganda ,mataokeo yake Tanzania ikakwama kiuchumi.

Tunajichafua sisi Watanzania huku wazungu wakitucheka.
Kila mtu alikuwa anajua kuwa Samia na Magufuli ni vitu viwili tofauti kabisa isipokuwa wewe, Magufuli na wapambe wake! Ndiyo mnagundua sasa? Tulipokuwa tunasema wanampaka mafuta kwa mgongo wa chupa mlidhani tuna chuki naye? Tulipokuwa tunasema wapinzani wake ni CCM na si kina Lissu alioamuru wauawe mlidhani tunakosea? Subiri dawa ikuingie. Bado utasikia na kuona mengi! Opss, si Magufuli alishaua upinzani jamani? Vipi tena?
 
Back
Top Bottom