Hata nchi ikienda upinzani mnaweza msione tofauti!

Watu wengi wanaochanganya R na L huwa na vichwa vigumu sana kuelewa mambo ya kijamii yanoyohitaji tafakari tunduizi, wewe ni mmojawapo.
 
Watu wengi wanaochanganya R na L huwa na vichwa vigumu sana kuelewa mambo ya kijamii yanoyohitaji tafakari tunduizi, wewe ni mmojawapo.
Dah! Sawa naona umeamua kuniteta kisa r na l
 
Toa maelezo ya kutosha lasivyo ni ukanjanja tu
 
Iende kwanza
 
Angalizo: bandiko hili linahitaji utafakari wako na sio hisia ama uchama na uchawa!...
Ni kweli bhana sijawahi kuona kwenye kampeni Marekani wananchi wamebeba bendera za vyama Bali hubeba bendera ya nchi, mpaka leo siijui hata rangi ya bendera ya democratics au republicans
 
Utakuwa mpumbavu kama unaamini Mkapa aliiibia nchi.
Niliposoma tu hapo nikaona ni hoja ya kisichana kinachojiuza mtaani.
Former President Benjamin Mkapa opens up on EPA scandal in ‘My Life, My Purpose’

Hiyo link nimekuwekea hapo Mkapa anakiri kuruhusu mabilioni ya EPA yaibiwe Ili kusaidia kwenye kampeni za CCM 2005!! Ni wakati wake pia ubinafsishaji ulifanyika kifisadi let alone kashfa ya Kiwira!! Huyu naye ni jizi tu kama majizi mengine na Uzuri alikiri mwenyewe Sasa unachomtetea Nini?
 
Hata sijui najadili nini na ww, hao usalama wa taifa unaowazungumzia ni kabla ya sheria ya juzi, sasa hivi wanaruhusiwa kuchunguza na kukamata. Hebu pitia kwanza hilo kisha tuendelee na mjadala.
 
Watu wenyewe wasio na sera Wala strategy hao wataleta tofauti gani? Huoni Kenya huko Kuna tofauti ya nafuu ya maisha imeletwa na kina Ruto? Ndio kwanza maisha yamekuwa magumu.

Mtu kama Lisu ataishia kuvuruga Kila kitu kama Mwendazake matokeo yake maisha yatazidi kuwa magumu.
 
Ahadi alizozitoa Mugabe wakati ule akiwa kijana anaingia ikulu ya Zimbabwe na kilichokuja kutokea katika utawala wake.

Museveni wa Uganda alitoa hotuba nzuri na ya kutumainia kuihusu Uganda. Leo hii katawala Uganda miaka likuki lakini sidhani kama Yale aliyoyaahidi wakati anaingia ikulu kama kweli kayatekeleza.

Ni kujilisha matango pori tu lakini kiuhalisia mambo ni yaleyale ,watu ni wale wale na si ajabu mpinzani akavurunda kuliko hata aliyepo madarakani kwa sasa.

Kenya waliuana kuitaka katiba mpya ,Leo hii wanazidi kulalamikia uongozi uliopo madarakani pamoja na katiba yao mpya.

Pambania familia yako na maendeleo yako, hayo mengine waachie wenye misuli ya kupambana na polisi na kulala mahubusu na kushinda mahakamani.

Kama huwezi kupambana nao jiunge nao
 
Ngoja kwanza tuwape hawa hawa wapinzani. CCM kwa zaidi ya miaka 60+ hawajafanya makubwa ya kuendelea kuaminiwa.
 
Na ndio maana hata Mimi nilishakataa kupoteza mda eti nahangaika na Wanasiasa wa Tanzania wajinga ndio watakuwa wanatumiwa.

Nitahangaika na siasa pale tuu zitakapokuwa na manufaa kwangu na.sio kufaidisha wengine hao wapiga kelele za njaa.
 
Na pia viongozi wengi ni mbumbumbu wanashindwa kuelewa kwamba bila kuvunja Mifumo ya kinyonyajo iliyoasisiwa na wakoloni hakuna kuendelea.

Utatakani maendeleo lakini huyopata ,kitendo Cha Nchi za Africa Kushindwa kuwa na Biashara kubwa baina Yao ni kaburi la umaskini.

Leo hii Kenya Iko tayari Kuagiza mahindi Brazil kuliko Nigeria Kwa sababu gharama ya meli au ndege kutoka Lagos Hadi Mombasa ni kubwa kuliko Kufuata Ulaya au Uarabuni.

Sasa Kwa mazingira haya mchinhisi haziwezi endelea.
 
Afadhari iende upinzani CCM inatuzarau sana watanzania
 
Hata sijui najadili nini na ww, hao usalama wa taifa unaowazungumzia ni kabla ya sheria ya juzi, sasa hivi wanaruhusiwa kuchunguza na kukamata. Hebu pitia kwanza hilo kisha tuendelee na mjadala.
😂 Sahivi Tena hujui tunajadili nini na matokeo ya juzi hayawezi kufanana na Yale yaliyopita kwa miaka Kenda huko awali..
 
Huna hoja , tuishi kwa mazoea
 
Ndio uko sahihi, lakini Kwa asilimia mia Mimi nimeona ccm haiwezi kutupeleka hapo unapopasema. Imebaki na sera za Nyerere ambazo Kwa sasa ni outdated, sasa Si Bora tujaribu na cdm au act nk.
Bro; ni kwamba inatakiwa tufike mahali chama Chochote kisiwe na umiliki wa nchi hii.
Chama kitakachofanya Vizuri ndo tutakachoenda nacho.
Inchi zilizoendelea hakuna chama kinachomiliki nchi, ila nchi maskin hususani za African ndo zina vyama tawala tena tawala kweli kweli.
Leo ukimkuta mtawala wa sisiemu anafanya ovu, ukamkemea anakuambia utaona, sitakupa ajila, au ntakupa kesi ya uhujumu uchumi, au ntakupoteza kabisa, au vitisho VYOVYOTE.
Yaani nchi hii imemilikiwa na visisiemu adi KERO, kiasi kwamba wamekua miungu watu.
JAMANI SIIPENDI SISIEMU, IKIJA KUTOKA MADARAKANI NADHANI NDO ITAKUA HAPPY BIRTHDAY YANGU.
SIO SIRI NATAMANI SISIEMU ITOWEKE KABISA, HALMASHAURI ZA OVYO OVYO TU, VITUO police VYA OVYO, MAHAKAMA ZA OVYO, HOSPITAL HUDUMA ZA OVYO, ELIMU YA OVYO, MIUNDO MBINU YA BARABARA NA UMEME OVYO, NA MENGINE MENGI. YOTE YANASABABISHWA NA SISIEMU TU.
SIJUI NI NYANJA IPI SISIEMU ILIPOFANYA VIZURI.
Siwezi kuogopa kumpa kura yangu cdm au act maana hamna ninalopata Kutoka sisiemu ambalo pengine ntahofia kulipoteza.
Wewe unaeogopa huenda ni mkuu wa WILAYA, au mkoa, au Kuna namna mkono wako unaenda kinywani Kwa ajili ya sisiemu.
 
Ukiona mtu yupo kwenye chama chochote na chama chake kikakosea jambo nae asifanye lolote kuhusu hilo kosa,aidha kulitatua,ama kuwajibisha n.k ndugu jua huyo mtu yupo kimasirahi hana uzalendo wala upendo..

Tunapigwa na hawa wanasiasa wetu kwasababu wanajua bado tumelala!,laiti kama tutabadirika sisi hata wao hawatakuwa nabudi yakubadirika waendane nasi!.
Nasisitiza tu.
 
Wakati mwingine ni tatizo la hao viongozi baina ya nchi za kiafrika kutokuwa stable. Leo mankubaliana hivi kesho anakugeuka.

Mfano Kenya anategemea apate mahindi toka Tanzania na biashara inakwenda vizuri bila ya shida, aknakuja kiongozi mwingine anapiga marufuku kuuza mahindi nje ya nchi.....wakati huo anajua kuwa Wakenya hawana tegemeo lao ni soko letu . Unategemea mkenya atamwamini tena mtanzania!?

Jumuiya ya Afrika Mashariki ilivunjikaje? Ni nini hasa kilisababisha kuvunjika kwa ushirikiano baina ya nchi? UBINAFSI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…