Hata nchi ikienda upinzani mnaweza msione tofauti!

📌📌📌📌📌🔨🔨
 
Hata huko Ulaya Jumuiya yao inavunjika-Unafikiri kwasababu gani? Na haina maana sisi Waafrika nao tuwe kama wao, ila ikumbukwe mashirikiano ya huko Ulaya yalilenga kuendeleza himaya na Ubeberu katika nchi za Afrika na Asia, hakuna lingine! Huku kwetu imekuwa kama kinyume chake;Kupinga ukoloni mamboleo na Ubeberu.


itoshe, hiyo dhana ya Kwamba haya mambo yanatokea Afrika tu ni dhana Potofu-Hebu tuambie na hiyo stability ya mchongo huko, mbona walishindwa kuafikiana kuhusu utumiaji wa nishati kutoka Urusi mwanzoni wa Vita za kibeberu huko?

Wamshukuru ndugu yao Mmarekani baada ya kuingilia vurugumechi ya Urusi na kutoa sadaka na fedha nyingi huko kUwasaidia hawa maharamia wa Ulaya.- Kwani ule ulikuwa ni nini kama sio UBINAFSI?
 
KENZY nimekuelewa vizuri point yako na ni kweli tunahitaji mjadala.

Kwa haraka haraka sisi ni Watanzania wale wale tabia zile zile.

Lakini kwa sasa tunataka mabadiliko hata ya jezi tu tumeichoka CCM.
 
KENZY nimekuelewa vizuri point yako na ni kweli tunahitaji mjadala.

Kwa haraka haraka sisi ni Watanzania wale wale tabia zile zile.

Lakini kwa sasa tunataka mabadiliko hata ya jezi tu tumeichoka CCM.
😂 Kwamba hata jezi...
 
Bila vyama vya upinzani maisha yatazidi kuwa magumu, satan, ania msichonganishwe kipuuzi na wachache sanaofaidika na chama kilichopo madarakani
Tusikubali utawal wa kifalme
Kuna vijana wanamaliza vyuo hawana kazi
Unajua kwanini? Kuna utwaka wa kiimla badala ya kustaafu wanarudishana kama hatorudishwa anawekwa mwanawe huku akiwa hana ujuzi wowote,
Untegemea watu kama hawa watakutambua raia unataka nin?
Na hii ni kawaida ya watanzania kila kitu wanajiambia tunamwachia mungu, kivipi ufanye uvivu na uzembe wako eti unamwachia mungu?!!
Eti vyama vya upinzani havina uwezo?
Tumia akili acha kuropoka je unataka chama kutoka mbinguni?
Hivi vyama hasa chadema ni muhimu kwa maisha ya watanzania
Wasipo piga kelele tutakipata cha mtema kuni
Labda mnataka chama kama cha Zito amabacho kinaenda na upepo wa watawalachama cha namna hii hakina msaada kwa wannchi
Chama ni kile kinauwezo wa kuwatoa ofsin kuja kuwashtakia wananchi
Msidanganywe vyama vya upinzani ni muhimu sana kwetu
Na kukitoa chama cha mapinduzi ni muhimu kitoke madarakani
 
Huna unachoelewa!! Unatolea mfano Kenya huku hujui Kanu yenyewe ilivunjika ndoyoote yakatokea
 
Muhimu kuliko yote ni kuwa na wananchi wenye akili nzuri na uelewa.
Msingi wa yote ni wananchi.
Viongozi, TISS, polisi, majeshi yote, watumishi wote wa uma,.... wanatokana na wananchi.
Wananchi wakiwa wa hovyo, kila kitu hovyo hovyo. Maamuzi yote yanafanywa na mmoja wote wanafuata mkumbo kama nyumbu.
Vyama vya siasa na wanaharakati hutoa elimu kwa uma na hivyo kuchochea mabadliko ya fikra.
 
Kwa nini usiseme tu ukweli kuwa wewe ni mfuasi wa upande mmoja?.
 
Inaonekana hata hujui kwanini nchi iko hivi jinsi ilivyo sasa na utatuzi wake nini ili tutoke hapa tulipo.Jipe muda wakujielimisha kabla yakuleta hisia zako hadharani.
 
Yaani una maana kwamba kinachotakiwa ni kama kile alichokisema Rais mstaafu Barack Obama akiwa Africa ya kusini “ Africa doesn’t need strong men it needs strong Institutions “ ??!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…