Hoja ya kitoto hiyo. Wote wenye akili tunajua ni ‘Abduli’ yupi anayemsema.
Tuliofuatilia hotuba yake jana (Singida) mwanzo mwisho, iko very clear kuwa aliyesemwa na kuongelewa hapo ni yuleyule mnayemfahamu yaani Abdul mtoto wa Rais wa JMT Bi. Samia Suluhu Hassan. Watu waliomsikiliza live on TV na Social medias na tuliokuwepo kwenye mkutano tulimwelewa vyema sana...!!
Tundu Lissu mpaka kumwanika wazi Abdul kuwa alimpelekea rushwa nyumbani kwake, hoja yake ilianzia na aliijenga ktk misingi mikuu miwili ambayo ni👇🏻👇🏻
1. Mgawo wa pikipiki 700 kila mkoa Tanzania (sawa na pikipiki zaidi 20,000 nchi nzima) zenye nembo ya "SSH - 2025" kifupi cha "Samia Suluhu Hassan - 2025" mali ya Samia. Swali likawa; pesa ya kununua pikipiki zote hizi huyu Mama Abdul kazitoa wapi maana mshahara wake hakuna anayedhani kama unafika hata 50,000,000 kwa mwezi?
2. Ugawaji wa rasrimali za Tanganyika tu kwa waarabubila kugusa za Zanzibar: Bandari zote za Tanganyika, hekta za hufadhi ya misitu zaidi ya milioni 9 za Tanganyika, Kufukuza wamasai wa Ngorongoro, Loliondo nk ili wapewe waarabu, kuuza uwanja wa KIA na kuvunja vijiji zaidi ya 6 vinavyozunguka uwanja huo ili uwanja huo na ardhi yote ya wanavijiji hao ipewe kampuni ya waarabu wa Oman.
NDO SWALI LAKE LIKAWA: Nyie wananchi mnafikiri huyu mama (Rais Samia) hizi pesa za pikipiki na anazogawa misikitini na makanisani anatoa wapi baada ya uchafu wote huu (kugawa rasrimali za Tanganyika) aliofanya ndani ya miaka mi3 tu ya u - Rais wake?
Katika kuhitimisha hoja yake ya "rushwa ya Abdul", alisema hivi;
"....hata mwanae huyu mama aitwaye Abdul aliniletea rushwa nyumbani kwangu, nikamwambia shenzi kabisa, toka nyumbani kwangu, kawahonge haohao unaoweza kuwahonga...!!"
Kwa hiyo muhusika hapa hajafichwa ni Abdul, mtoto wa Rais Samia Suluhu Hassan. Kama ni msafi, amechafuliwa tu na anadhani amesingiziwa, yeye mwenyewe au CCM yeyote au wote wanayo fursa ya kulianzisha kwa kumshitaki Tundu Lissu mahakamani ili akathibitishe tuhuma zake na akishindwa si ndio wafurahi sasa kwa sababu walichokitafuta siku nyingi, kumpoteza huyu mwamba watakuwa wamekipata? Yanini kutafutana kwa risasi za SMG wakati mbaya wao kajiingiza mwenyewe kwenye mtego wao?
SWALI NI: CCM au Abdul mwenyewe au Mama Abdul wana ujasiri huo? Ni wasafi kwa kiasi gani kuweza kuvaa ujasiri huo wa kwenda mahakamani kwenda kulumbana na huyu mwamba hata kama mahakama ni zao?
Katika hili, Tundu Lissu na CHADEMA mpaka sasa kisiasa wanaongoza goli 11 - 0..
Na kikubwa na cha muhimu zaidi ni kuwa, hadhira yote iliyomfuatilia na kumsikiliza Tundu Lissu jana toka pande zote za nchi na dunia live toka Singida, ilimwelewa na kuamini kila neno lililotoka kinywani mwake!!