Pre GE2025 Hata Tundu Lissu naye huwa anadanganya!

Pre GE2025 Hata Tundu Lissu naye huwa anadanganya!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mpya kutoka kwa Tundu Lissu ni madai kwamba mtoto mmoja wa Rais Samia aitwaye ‘Abduli’ 🤣, alimpelekea Lisu rushwa nyumbani kwake.

Baada ya Lissu kuona hivyo eti akamwambia “shenzi”, kahonge huko kwa wanaohongeka.

Lissu naye ni kama wanasiasa wengine tu. Na yeye hudanganya pia.

Kwenye haya madai yake mapya, hajatoa ushahidi wowote ule.

Kasema tu kuwa Abduli alimpelekea rushwa nyumbani kwake.

Rushwa ya aina gani? Lisu hakuweka wazi.

Lisu ana historia tayari ya kusema uongo. Nawashangaa kwa nini CCM huwa hawaikamati hiyo fursa na kuitumia kwa manufaa yao kihoja!

Lisu alidanganya waziwazi kuwa mlinzi mmoja wa Rais Magufuli naye alikufa kwa korona kipindi kile kile ambacho Magufuli alikufa!

Lakini mlinzi huyo akaonekana kwenye mazishi ya Magufuli baada ya Lisu kudanganya kuwa jamaa amekufa.

Pia aliwahi kudai eti baada ya Magufuli kufa, yalikutwa mamilioni ya doła za Kimarekani nyumbani kwake 😀.

Sasa kaja na hizi stori za ‘Abduli’ bila ushahidi wowote ule.

Kama anasema uongo dhidi ya ‘Abduli’, CCM watakuwa majuha wakimwacha aendelee kupeta bila ya kum challenge [kisiasa, of course].

Pia soma Kuelekea 2025 - Lissu: Abdul aliniletea rushwa nyumbani kwangu nikamwambia "Shenzi, kahonge wanaohongeka"
Wewe huwa una chuki zako binafsi za Lissu! Huna maajab
 
I said " sacks of money" because I cannot really understand why you found it impossible for Abduli to offer a bribe to Lissu. The notion would have only been ridiculous if Lissu had claimed that he had turned away Abdulli with his sacks of money.
When it is said that Lissu said" alimtimua Abdul alipompelekea rushwa" some people assumed he was referring to hard cash and found it unbelievable that Abdul would literally do that hence Lissu must have been lying.

Amandla...
I didn’t say I found it impossible for Abduli to try to bribe Lisu.

All I said was [1] Lisu didn’t provide any evidence or proof of his claim and [2] Lisu has been caught lying before. Therefore, any reasonably minded person wouldn’t eat up hook, line, and sinker to what he says when addressing a political rally.

Lisu is not above lying and deceit.

We all know corruption is a scourge in the country and also commonplace.

To quote Carl Sagan, “what counts is not what sounds plausible, not what we would like to believe, not what one or two witnesses claim, but only what is supported by hard evidence rigorously and skeptically examined. Extraordinary claims require extraordinary evidence”.
 
Nadhani akipandwa na midadi ndo huwa anaongea chochote tu ili mradi apigiwe makofi.

Huyo ‘Abduli’ atakuwa juha kiasi gani mpaka aende nyumbani kwa Lisu kumpa rushwa?
Kama huamini kuwa Abdul anaweza kuwa juha kiasi hicho, basi hujui Watanzania waitwao "chawa" wana nguvu na ushawishi kiasi gani kwa siasa za bongo!
 
Madai ya fidia ya matibabu hakuwahi kusema kuwa alilipwa.
Usipotoshe
 
Mpya kutoka kwa Tundu Lissu ni madai kwamba mtoto mmoja wa Rais Samia aitwaye ‘Abduli’ 🤣, alimpelekea Lisu rushwa nyumbani kwake.

Baada ya Lissu kuona hivyo eti akamwambia “shenzi”, kahonge huko kwa wanaohongeka.

Lissu naye ni kama wanasiasa wengine tu. Na yeye hudanganya pia.

Kwenye haya madai yake mapya, hajatoa ushahidi wowote ule.

Kasema tu kuwa Abduli alimpelekea rushwa nyumbani kwake.

Rushwa ya aina gani? Lisu hakuweka wazi.

Lisu ana historia tayari ya kusema uongo. Nawashangaa kwa nini CCM huwa hawaikamati hiyo fursa na kuitumia kwa manufaa yao kihoja!

Lisu alidanganya waziwazi kuwa mlinzi mmoja wa Rais Magufuli naye alikufa kwa korona kipindi kile kile ambacho Magufuli alikufa!

Lakini mlinzi huyo akaonekana kwenye mazishi ya Magufuli baada ya Lisu kudanganya kuwa jamaa amekufa.

Pia aliwahi kudai eti baada ya Magufuli kufa, yalikutwa mamilioni ya doła za Kimarekani nyumbani kwake 😀.

Sasa kaja na hizi stori za ‘Abduli’ bila ushahidi wowote ule.

Kama anasema uongo dhidi ya ‘Abduli’, CCM watakuwa majuha wakimwacha aendelee kupeta bila ya kum challenge [kisiasa, of course].

Pia soma Kuelekea 2025 - Lissu: Abdul aliniletea rushwa nyumbani kwangu nikamwambia "Shenzi, kahonge wanaohongeka"
Ila huyo Abdul atakuwa ana hela sana maana kuna nyumba moja ya family friend kainunua kwa 800m cash hapo mikocheni.
 
Tuliofuatilia hotuba yake jana (Singida) mwanzo mwisho, iko very clear kuwa aliyesemwa na kuongelewa hapo ni yuleyule mnayemfahamu yaani Abdul mtoto wa Rais wa JMT Bi. Samia Suluhu Hassan. Watu waliomsikiliza live on TV na Social medias na tuliokuwepo kwenye mkutano tulimwelewa vyema sana...!!

Tundu Lissu mpaka kumwanika wazi Abdul kuwa alimpelekea rushwa nyumbani kwake, hoja yake ilianzia na aliijenga ktk misingi mikuu miwili ambayo ni👇🏻👇🏻

1. Mgawo wa pikipiki 700 kila mkoa Tanzania (sawa na pikipiki zaidi 20,000 nchi nzima) zenye nembo ya "SSH - 2025" kifupi cha "Samia Suluhu Hassan - 2025" mali ya Samia. Swali likawa; pesa ya kununua pikipiki zote hizi huyu Mama Abdul kazitoa wapi maana mshahara wake hakuna anayedhani kama unafika hata 50,000,000 kwa mwezi?

2. Ugawaji wa rasrimali za Tanganyika tu kwa waarabubila kugusa za Zanzibar: Bandari zote za Tanganyika, hekta za hufadhi ya misitu zaidi ya milioni 9 za Tanganyika, Kufukuza wamasai wa Ngorongoro, Loliondo nk ili wapewe waarabu, kuuza uwanja wa KIA na kuvunja vijiji zaidi ya 6 vinavyozunguka uwanja huo ili uwanja huo na ardhi yote ya wanavijiji hao ipewe kampuni ya waarabu wa Oman.

NDO SWALI LAKE LIKAWA: Nyie wananchi mnafikiri huyu mama (Rais Samia) hizi pesa za pikipiki na anazogawa misikitini na makanisani anatoa wapi baada ya uchafu wote huu (kugawa rasrimali za Tanganyika) aliofanya ndani ya miaka mi3 tu ya u - Rais wake?

Katika kuhitimisha hoja yake ya "rushwa ya Abdul", alisema hivi;

"....hata mwanae huyu mama aitwaye Abdul aliniletea rushwa nyumbani kwangu, nikamwambia shenzi kabisa, toka nyumbani kwangu, kawahonge haohao unaoweza kuwahonga...!!"

Kwa hiyo muhusika hapa hajafichwa ni Abdul, mtoto wa Rais Samia Suluhu Hassan. Kama ni msafi, amechafuliwa tu na anadhani amesingiziwa, yeye mwenyewe au CCM yeyote au wote wanayo fursa ya kulianzisha kwa kumshitaki Tundu Lissu mahakamani ili akathibitishe tuhuma zake na akishindwa si ndio wafurahi sasa kwa sababu walichokitafuta siku nyingi, kumpoteza huyu mwamba watakuwa wamekipata? Yanini kutafutana kwa risasi za SMG wakati mbaya wao kajiingiza mwenyewe kwenye mtego wao?

SWALI NI: CCM au Abdul mwenyewe au Mama Abdul wana ujasiri huo? Ni wasafi kwa kiasi gani kuweza kuvaa ujasiri huo wa kwenda mahakamani kwenda kulumbana na huyu mwamba hata kama mahakama ni zao?

Katika hili, Tundu Lissu na CHADEMA mpaka sasa kisiasa wanaongoza goli 11 - 0..

Na kikubwa na cha muhimu zaidi ni kuwa, hadhira yote iliyomfuatilia na kumsikiliza Tundu Lissu jana toka pande zote za nchi na dunia live toka Singida, ilimwelewa na kuamini kila neno lililotoka kinywani mwake!!
✍️📝👊👍👌👏🤝🙏
 
That’s speculative!
Mkuu mwenzio kaongea kwa kiswahili na sisi hadhira yako tunajadili kwa kiswahili, wewe ung'eng'e wa nini hapa??

Hoja ipo kwa kiswahili unaenda kujificha kwenye Kiingereza ili iweje?? Mkuu wewe mswahili hadi kisogoni, acha hizo!!!
 
Yule ,mnatakiwa mkamate na mpeleke mahakamani ,huko ndo hua anatoa ushahidi....kazi yake kashamaliza kutamka
 
Lisu aliwahi kusema "tuna rais wa ajabu, haijawahi kutokea". Machawa wa jiwe wakaja juu na kumpeleka mahakamani. Lisu akawaruka kiulaini kabisa. Akauliza nilimaanisha rais yupi? Wa bao, TFF, wasafi, wa wanaume, au rais yupi?
Ila Chadema hamna akili nyie, kwahy hapo mnamuona huyo Lissu mjanja wa sheria sana
 
Nadhani akipandwa na midadi ndo huwa anaongea chochote tu ili mradi apigiwe makofi.
Siyo kupandwa na midadi, ndugu yetu ana tatizo kubwa zaidi ya kupandwa midadi. Utengamano wa uwezo wake wa kufikiri hutegemeana na majira ya mwezi. Mwezi ukiwa kona huyo jamaa yetu anaweza kulipuka na kuropoka kitu chochote mpaka watu mkashangaa.
 
Back
Top Bottom