Hatari, nimeongea na Ex-Wangu, nimejisikia vizuri sana

Unazidi kuwafanya wanawake wenye watoto nje ya ndoa kuwa katika hali ngumu ya kutoaminika...
Muache dada wa watu kasha move on ana maisha yake na ameolewa..huoni unataka kumvurugia?
Msaada wako mkubwa kwake ni kutowasilia na nae kabisa...
Amesha sikia raha unahisi ni rahisi kuacha
 
Dar haya mambo acha tu mm nilizaa na mnyaturu wa Singida bahati nzuri kaolewa yupo hapa Mbeya,mm nilikuwa nafanya kazi Singida nikahamia Mbeya kabla ya yeye kuolewa ,Cha ajabu alivyoolewa huku akaanza kunitafuta nipo Mbeya sehemu Gani?Nilimjulisha sehemu nilipo ,nikaomba nimuone mtoto wangu alikubali akaniletea mtoto ,Sasa imekuwa kero ,Mme wake ni fundi ujenzi akiwa hayupo ananipigia simu mara Kwa mara ,mara mtoto anaumwa,n.k nikaona huyu ni kama ananiletea mitego nifanye naye mapenzi,mm nilimwambia mtego huo ,huwezi ni rubuni kirahisi hivyo nikamblock kwenye simu ,Huwa namtafuta nikitaka kutuma Hela za matumizi ya mtoto .Ujinga wa kukumbushiana mambo yaliyopita sitaki
 
 
Unayasikiliza mahubiri ya shetani,huyo tayari ni mke wa mtu,utamuharibia ndoa yake au ya kwako itaharibika very soon...
 
Wewe ni mshenzi, mpumbavu na mbinafsi......
Huna hata haya, ulishindwa kuongea nae kipindi mtoto mdogo ndo uje urudishe mawasiliano sahizi mtoto ashakua mkubwa na hamuhitaji hata kuwa na mawasiliano????

Acha ubinafsi na roho mbaya, ishi maisha yako. Kua na haya na pia kua na huruma na mwanaume mwenzio, angekua ni mkeo huyo usikie karudisha mawasiliano na mzazi mwenzie ungejisikiaje??????? Shenzi kabisa
 
Double standard.........

Kwa hiyo ukioa singo mom, umeoa mke wa mtu; na ukiolewa na singo father; si ina maana umeolewa na mume wa mtu pia au singo father ni mume wako peke yako?
Majority mnampiga mawe huyo dada wa watu kwamba hakustahili kuolewa; je huyu mwanaume alistahili kumuoa mkewe aliyemuoa? Dada wa watu ameolewa zake huko; miaka yote hakuhangaika kumtafuta mzazi mwenzie; leo baby daddy ndiyo amemtafuta; surprisingly matusi yanaelekea kwa dada wa watu.

Wangapi humu mnamuonea huruma mke wa huyu baba; maana mumewe ndiyo ana kiranga cha kumtafuta mzazi mwenzie. Huyu baba akija akapasha kiporo na mzazi mwenzie; ni sawa kwa mke wa huyu baba ; ila sio sawa kwa mume wa baby momma? Wazazi wenza wakipasha viporo; matusi ni kwa mwanamke kwamba hafai kuolewa; je baby daddy anapasha kiporo na baby momma wake; yeye anadeserve kuoa? He huyu baby daddy si hasara kwa mkewe?. Je wanawake wakitaka kuolewa na single fathers hawatakiwi kuhakikisha wanaona makaburi ya baby mommas wao kwanza?
 
Ukijibiwa hapa nitag, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Afu nimekumic mnoo mama malezii.
 
Unataka ukapashe kiporo
 
Umepotelea wapi mama majengeka; nilikuwa nakusubiri kwa hamu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

You are missed big time.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] yaan kule selfika wameni ban nisicomment, wamejuajee kunikaushaa kizaziii? Mbona nilitakaa nika uzike ule uzi mazimaa.

Na ningewasanua waja mule, mbona afadhari ya TBC na matangazo yao Ya Tanzia. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Afu wamekuonea tu. Teh Uzi utafungwa kila siku ule; mambo elfu kumi

Em tusije kuchambwa tunaharibu uzi wa watu hapa
 
nafikiri umepata kiherehere cha kutaka kuonana nae baada ya kusikia ameolewa
kunamtu anahudumia na atakuwa amependeza akili zako zinavyokutama
angekuwa anaganga na njaa mtaani sidhani kama ungetaka kuonana nae
usitake kumuharibia dada wa watu hilo pepo la tamaa likutoke
huyo ibilisi mkemee kw
a nguvu zote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…