tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 27,843
- 29,350
Leo nimeona mkeka wa wahitimu wa kidato cha sita wapatao 60,000 ambao wamelazimishwa kwenda JKT kwa lazima kwenye makambi mbalimbali waliyopangiwa kuripoti kuanzia tarehe 01.07.2026. Huyu mtu aliyelazimisha kutungwa sheria ya wanafunzi wa kidato cha sita kwenda JKT kwa lazima ni mwendawazimu. Hivi anafahamu kweli matatizo ambayo wanafunzi hawa wanapitia wawapo huko kwenye makambi ya mateso?
Ingependeza kama wanasiasa wanaolazimisha watoto wa makabwela kwenda kuteseka kwenye makambi ya jasho na damu nao watoto wao wangepelekwa huko wakateseke. Hawa wapuuzi watoto wao wapo Oysterbay, Msasani na Masaki wanakula bata huku watoto wa wenzao wanateseka kwenye makambi ya mateso. Inauma na inasikitisha sana.
Hivi ni lini hawa wachumiatumbo wataacha kuwatesa watoto wa walalahoi? Kuwalazimisha watoto wa maskini kwenda JKT sio tu kunasababisha mateso kwa watoto bali pia kunaongeza gharama zisizokuwa za lazima kwa wazazi maskini ambao wamejikamua hadi senti ya mwisho kuwasomesha watoto wao.
Kibaya zaidi, yapo malalamiko kwamba baadhi ya makambi haya yamekuwa yakihusishwa na vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya watoto wa kike. Wapo wazazi wanaohofia usalama wa watoto wao kutokana na madai ya mimba na maambukizi ya HIV magonjwa yanayoripotiwa kutokea kwa baadhi ya wahusika waliopita kwenye mazingira hayo
Kuna wakati tunasingizia maprofesa wa vyuo vikuu kuwajaza mimba na UKIMWI watoto wa kike na kuwapa digrii bure bilashi. Lakini kuna madai Watoto hawa huathirika pindi wanapokuwa kwenye makambi haya ya mateso. Natoa wito kwa wazazi kuwazuia watoto wao wasiende kutwezwa kwenye haya makambi ya kijanjaweed na yasiyokuwa na adabu hata kidogo. Mzazi chukua hatua; mlinde mwanao dhidi ya utwezwaji!