JKT lengo Lao ni zuri ila kwa wakati tuliopo inabidi wabadilike. Vijana kupata mafunzo ya ukakamavu ni jambo zuri ila kwenye utoaji life skills wapo nyuma shughuli wanazofundisha ni uzalishaji mali kwa kilimo.
JKT wao ilibidi wawe chachu ya mapinduzi ya viwanda na vijana kujiajiri wahitimu wao. Sio wale wa mujibu miezi 3 au kujitolea wakimaliza ukiwaleta mtaani wanarudi bila ujuzi wowote hata kufungua tairi ya bajaj au bodaboda azibe pancha, kwenye kilimo hata kuendesha tractor au kufunga jembe hawawezi.
JKT ilitakiwa itoe mafunzo ya ukakamavu,ulinzi na soft skills ambazo kwenye maisha halisi ya vijana mtaani wanaweza wakajiajiri au kuajiriwa baada ya kutoka makambini hata wakikosa nafasi ya kuendelea mbele kitaaluma.
JKT inabidi wawe na mafunzo ya basic agriculture machine operation, agriculture machine mechanics, solar installation,tyre change operations, ushonaji,umeme wa majumbani,kupaka rangi,uchongaji vyuma,carpentry,upambaji, ufundi bomba. JKT wana connection kubwa ya kazi kupitia Suma JKT wanaweza kuwa wanapelekwa kufanya kazi kwa vitendo na wakimaliza mafunzo ya miezi 3 wapewe certificate of service kulingana na kada aliyofanyia vitendo.