Hatima ya Fei Toto kujulikana Jumatatu tarehe 9 Januari 2023

Kwa hiyo ulifikiria akiweka hizo 112m Basi mkataba umevunjwa ,kweli elimu elimu elimu Ni muhimu,ingekuwa hivyo mbona wachezaji wengi wangekuwa wanavunja mikataba yao
 
Ila mkataba hauwezi vunjwa na upande mmoja lazima pande zote zilizie. Mfano Flamini wa Arsenal ,Arsenal walikuwa hawataki kumuachia na walichomoa ofa nyingi sababu bado alikuwa na mkataba na Arsenal,mwishoe Flamini akaondoka free baada ya mkataba kuisha. Pogba mda mrefu alisha onyesha nia ya kuondoka ila Man hawakutaka kumwachia mwishoe akaondoka free baada ya mkataba wake kuisha.

Hata Yanga kwa kuwa bado wanamkataba nae wanaweza kuamua hautumuzi tutamwachia free mpaka mkataba wake ukiisha so Yanga uwezo huo anao na anayo haki kisheria.
 
Ndug tofauti yetu mimi na wewe ni mitazamo tu kuniambia mimi ni mjinga sio sawa mbona mimi hakuna mahali nimekutukana??? Kuwa muungwana basi umesema hujui kama kama nimemaliza hata primary je kama ni kweli sijamaliza hata primary je ningeweza kuandika ukaelewa kama sijamaliza darasa la 7??

Hivi kwann mnachukia sana mtu akiasema ukweli?? Hivi ukiwa mshabiki wa utopolo lazima akili ziyumbee na kuduma??? Unasema hajafuata utaratibu lakini unasahau huyu fei aliingiza pesa ambazo ni haki yenu yanga ambao mlimsajilia kweny account yenu mkazirudisha sasa mnasemaje hajafuata utaratibu huo mnaoutaka nyie hawezi kuufuta kwa sababu kuna njia nyingine ambayo mtakaba unampa kufuata sio hio mnayotaka ninyi ziko njia na taratbu nyingine kweny huo mtakataba zinamruhusu sema nyie mnataka kuabudiwa kama miungu Wangu vile mnamlzamisha atumie hio njia yy hataki anatumia njia nyingine hamtaki sasa mnaanza kulia lia na kutia huruma hapa.

Mtu alisema kweli mnakiwa wakali na kuanza matusi ndug huu mchezo hautaki hasira hata kidogo kuwa mpole lakini sio George wa Geita
 
Haya, kamati imeishaamua huko.

View attachment 2471971
mdogo wetu feisal waliokudanganya wamekuponza,haya waambie waje na iyo b1 uende kwao wao si wana hela na wanakuonea huruma na unacholipwa na yanga...wangekuwa na adabu na ustaarabu mbon ungeenda tu hata kwa 400mil lkn kwa hivi walivyotuyumbisha hapa siku mbili tatu mpk wakawapa maneno MADUNDUKA FC haki ya nani bila b1 basi usubiri free agent huku ukiozea benchi.
 
Hili lilitarajiwa lakini Mwanasheria wa Yanga na viongozi kwa ujumla ni wazembe kupindukia. Una mchezaji mzuri kama Feisal huku kabatini mwako una mkataba wake wenye kifungu cha kuvunja huo mkataba kwa milioni 100?

Kwa uzoefu wangu wa haya mambo naona Yanga ni wazembe na wakiendelea hivi ipo siku watakuja kuitia Club matatizoni kwasababu kama mkataba tu wa mchezaji unakuwa na mashimo hivi mikataba mingine mikubwa hali itakuwa mbaya zaidi.
 
Labda tu nikuambie kuwa kinachofanya mchezaji kubakia kuutumikia mkataba ambao hautaki ni vipengele vya mkataba......na wanaomuhitaji wakichungulia vipengele vya kimkataba wanaondoka.........kuna kipindi Psg walitaka kumsajili kwa kuununua mkataba wake pale Barcelona lakini walikuta mkataba wake una thamani ya pauni milioni 450 kama sikosei.....ndio wakaamua kuachana naye mpaka thamani ya mkataba wake ilipopungua.......ndio maana vilabu vikubwa huuongezea thamani mikataba ya wachezaji wao tegemezi mara kwa mara ili kujilinda na kuondoka kwao hawangoji mpaka uishe..............

Kuuvunja mkataba unatokana na kufikia matakwa ya kimkataba na sio utashi wa klabu husika.....kwa mfano klabu inapompa mchezaji mkataba maana yake humo ndani kuna matakwa na utashi wa klabu kwa mchezaji husika......na mchezaji kusaini maana yake amekubaliana navyo.......

Ikiwa klabu imeainisha kimkataba kuwa huu mkataba una thamani ya 100m maana yake ni kuwa huyo muajiriwa uhuru wake anaununua kwa 100m....na akitaka kufanya hivyo sio kuomba ruhusa bali kutoa taarifa kwa watu hao.........Suala la FEISAL inaonekana anataka kutumia mwanya wa thamani ya mkataba kujiweka huru ili aendelee na maisha mengine.........
 
Jumatatu mkataba ndo utafikia kikomo kwa sasa ni mchezaji wa yanga inajieleza vzr
 
Let's and see ila kwa sasa Yanga ndio walioshika mpini. Hata mimi sipendi Fei akomolewe japo kitendo alicho kifanya cha kihuni, huwezi kuigomea timu na kugomea mazoezi kisa unataka kuondoka.
 
Kamati imeamua kuwa Fei ni mchezaji wa Yanga.

Ila Uamuzi kamili utatolewa j3? Mie ndo sielewi au taarifa haijakaa sawaa.
Pamoja na tofauti zetu kwenye timu tunazoshabikia (Ingawa tunaweza tukawa wote tunaishabikia Majimaji ya kunyumba) kwenye hili hata mimi sijawaelewa hawa waliotoa maamuzi, na huku bado tunasubiri maamuzi kamili Jumatatu..!! Hii ya kusubiri na huku washasema ni mchezaji wa Yanga maana yake nini?
 
Let's and see ila kwa sasa Yanga ndio walioshika mpini. Hata mimi sipendi Fei akomolewe japo kitendo alicho kifanya cha kihuni, huwezi kuigomea timu na kugomea mazoezi kisa unataka kuondoka.
Hakika ndugu.....

Lakini hili Suala naona liko 50 kwa 50 kwa usiri uliopo kwenye mikataba na uendeshwaji wa vilabu vyetu inawezekana Feisal akawa sahihi kwa hichi anachokipigania.......pengine yameibuka baada ya muda mrefu wa kitokuelewana.....
 
CC Kalpana
 
Hii taarifa inathibitisha vile TFF na Kamati zake hawako huru, kuna external influence toka nje inayowaendesha, no doubt.

Kiuhalisia haiwezekani leo watoe taarifa nusu, halafu waseme Jumatatu pande zote zitatoa maamuzi kamili, hii haraka ya nini kama sio kuwaridhisha wanasiasa? huu ni wizi mtupu, mpira wetu umeingiliwa na wanasiasa.

Narudia tena kuandika hapa; kwenye hii issue haki haipo upande wa utopolo, ipo upande wa Fei toto, mtakaonuna shauri zenu, muone aibu TFF inavyolazimisha kuwabeba.
 
Kwa kuwa Yanga kashinda kipindi kile cha Morrison haki ilikiwa upande wa nani?
 
Hakika ndugu.....

Lakini hili Suala naona liko 50 kwa 50 kwa usiri uliopo kwenye mikataba na uendeshwaji wa vilabu vyetu inawezekana Feisal akawa sahihi kwa hichi anachokipigania.......pengine yameibuka baada ya muda mrefu wa kitokuelewana.....
Mpaka sasa hayupo sahihi, manake Yanga wana uwezo hata wa kumshtaki kugomea mazoezi wakati akiwa kwenye mkataba bila sababu za msingi. Kumbuka kuna sheria zina mlinda mchezaji na vile vile zipo zinazo linda mkataba.

Kwa wenzetu wangenda mbali na kuchimba hata hizo hela alizopeleka Fei ni zake au zilitoka kwa nani na wangemjua wange mfungia kujihusisha na maswala ya soka.
 
Ila fei kashasema bora awe mvuvi kuliko kurudi utopoloni [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]hv nyie was3ng* mlimfanya nini feisal,au rais alitaka kumla jicho ??
 
Ila fei kashasema bora awe mvuvi kuliko kurudi utopoloni [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]hv nyie was3ng* mlimfanya nini feisal,au rais alitaka kumla jicho ??
Mwisho wa siku atakaye umia ni nani?
 

Yanga wanaweza kuchukua hatua baada ya hukumu ya jumla sio hii ambayo bado ina mkanganyiko.......andiko hili la tff bado halihitimishi suala la FEISAL
 
Hauja jibu swali una ruka ruka tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…