Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama sio artificial basi tulipo si karibu!!
Hatuna umoja, viongozi wanawalenga ring leaders wakijua kondoo watasambaratikaMara nyingi viongozi ndo humaliza wenzao
Kama sio artificial basi tulipo si karibu!!
Wenye Degree wameambiwa waende VETA .Wakuu
Mawaziri George Simbachawene (Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu) na Prof. Adolf Mkenda (Elimu, Sayansi na Teknolojia) wamekutana na viongozi wa Chama cha Walimu Wasio na Ajira (NETO) kujadili hatua za kutatua changamoto ya ajira kwa walimu.
==
Mwenyekiti wa Umoja wa Walimu Wasio na Ajira Tanzania (NETO), Joseph Kaheza, amesema umoja huo umeendelea kuwa na mshikamano katika kudai ajira kwa walimu waliokosa nafasi za ajira.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Alhamisi Machi 13, 2025 , Kaheza ameishukuru serikali kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, kwa kulipa suala hilo uzito mkubwa na kuhakikisha linapewa kipaumbele cha kitaifa.
Amesema Waziri Simbachawene aliwakutanisha na mawaziri wa wizara tatu pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali ili kujadili namna bora ya kushughulikia changamoto ya ukosefu wa ajira kwa walimu.
Ameeleza kuwa NETO inapongeza falsafa ya 4R ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwa imechangia kufanikisha mazungumzo kati ya walimu wasio na ajira na serikali.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa NETO, Mwalimu Daniel Edward Mkinga, amesema katika kikao hicho, walimu waliwasilisha nyaraka yenye kurasa zaidi ya 22 inayoelezea changamoto wanazokutana nazo tangu hatua ya usaili hadi mwisho wa mchakato wa ajira.
Amesema katika mazungumzo hayo, walijadili mabadiliko ya mitaala, mfumo wa usaili wa walimu, umri wa kustaafu, na uzalishaji wa walimu, ambapo serikali ilikubaliana kuunda tume maalum ya wizara tano itakayoshughulikia changamoto hizo.
Ameeleza kuwa Waziri Simbachawene aliwataka walimu kuwa na subira kwa siku 30 hadi 45, wakati tume hiyo ikifanyia kazi masuala waliyowasilisha.
Ametaja wizara zinazohusika katika mchakato huo kuwa ni Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, na Wizara ya Fedha.
Amesema moja ya mafanikio yaliyopatikana mara moja ni utatuzi wa changamoto ya walimu wa somo la Uchumi, ambao awali hawakupata nafasi ya kufanya usaili, ambapo mawaziri husika waliidhinisha kibali cha kuanza kwa usaili huo mara moja.
NETO imewataka walimu na wananchi kwa ujumla kuwa na uvumilivu na kushirikiana na serikali, kwani hatua zinazochukuliwa ni za msingi
Pia, Soma
CCM wanafanya vizuri sana. Unajua ukifuga majini ni lazima uwe na damu ya kuyalisha mara kwa mara. Haya majini CCM inayofuga yatakuja kuigeuka na kuingamiza ka sababu haina damu ya kuyalisha yote yashibe.Wakati CHADEMA ikikomaa na NO REFORM, NO ELECTION, ACT WAZALENDO nao wamekuja na mpya kususia vikao vya umoja wa vyama vya siasa kwa madai kama ya CHADEMA, CCM wao wako busy kubuni mbinu za kunasa makundi mengi ya wananchi waisapoti na kuipa kura nyingi uchaguzi mkuu. Wanabuni vikundi vya ajabuajabu kama wadudu wa Arusha, wapuuzi wa NETO, wanawake wa samia, vikundi vya walemavu, mama/baba lishe, wapaa samaki, washindilia vitunguu kwenye magunia, wajasiriamali wa aina zote, motivation speakers, ma MC, ma producer, wasanii wa fani zote, ma DJ, vikundi ni vingi na orodha ni ndefu, CCM imejipanga kwa kampeni kabambe, wanakuambia UTU NA KAZI, TUNASONGA MBELE. Kiufupi CCM tayari wako mbele kwenye kampeni kabla muda rasmi haujaanza. Kwa hali hii hawa hata wakishinda ni halali yao kwa jinsi strategy ya kupata kura wanayoipata. Nafuatilia na nahudhuria abrakadabra zao nyingi wanazoziandaa kujiweka tayari kwa kampeni na kuvuna kura nyingi kwenye uchaguzi mkuu. Wapinzani bado wamezubaa sana,
Kazi yao ya kushika chaki, na kuandika ubaoni.. 🙂 🙂Kwani walikuwa wanatafuta nini?
Sidhani, mwaka juzi ilitokea Kashkashi kama hii (kada ya Afya wasio na ajira) , wale viongozi wakalambishwa asali.. 🍯🍯🍯Hapo hakuna asali,ni mbinyo na ahadi hewa.
Yule mama Kuna watu wanamdanganya kama alivyokuwa anadanganywa mwendazake...Nyuma ya NETO kuna makundi mengi zaidi kwa ufadhili wa watu ndani ya chama wasioridhishwa na mwenendo wa kwamkizi
Ni watu wachache waliopo kwenye mfumo baada ya wao kula na kushiba hawakuona umuhimu wa wengine, na hili mara nyingi husababishwa na ubinafsi, ukiritimba na roho mbaya.Inaumiza sana...aliyeanzisha huu mfumo sijui aliwaza nini