Pre GE2025 Hatima ya Walimu Wasio na Ajira (NETO) kujulikana baada ya siku 45, wapongeza 4R za Rais Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kodi yangu inachezewa eti kuundwe TUME YA WIZARA TANO.
Nitarudi
KAZI ni kipimo cha utu
 
Mwenyekiti wa Umoja wa Walimu Wasio na Ajira Tanzania (NETO), Joseph Kaheza, amesema umoja huo umeendelea kuwa na mshikamano katika kudai ajira kwa walimu waliokosa nafasi za ajira

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma leo Alhamisi Machi 13, 2025 , Kaheza ameishukuru serikali kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene, kwa kulipa suala hilo uzito mkubwa na kuhakikisha linapewa kipaumbele cha kitaifa.

Amesema Waziri Simbachawene aliwakutanisha na mawaziri wa wizara tatu pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali ili kujadili namna bora ya kushughulikia changamoto ya ukosefu wa ajira kwa walimu.

Ameeleza kuwa NETO inapongeza falsafa ya 4R ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuwa imechangia kufanikisha mazungumzo kati ya walimu wasio na ajira na serikali.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa NETO, Mwalimu Daniel Edward Mkinga, amesema katika kikao hicho, walimu waliwasilisha nyaraka yenye kurasa zaidi ya 22 inayoelezea changamoto wanazokutana nazo tangu hatua ya usaili hadi mwisho wa mchakato wa ajira.

Amesema katika mazungumzo hayo, walijadili mabadiliko ya mitaala, mfumo wa usaili wa walimu, umri wa kustaafu, na uzalishaji wa walimu, ambapo serikali ilikubaliana kuunda tume maalum ya wizara tano itakayoshughulikia changamoto hizo.

Ameeleza kuwa Waziri Simbachawene aliwataka walimu kuwa na subira kwa siku 30 hadi 45, wakati tume hiyo ikifanyia kazi masuala waliyowasilisha.

Ametaja wizara zinazohusika katika mchakato huo kuwa ni Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, na Wizara ya Fedha.

Amesema moja ya mafanikio yaliyopatikana mara moja ni utatuzi wa changamoto ya walimu wa somo la Uchumi, ambao awali hawakupata nafasi ya kufanya usaili, ambapo mawaziri husika waliidhinisha kibali cha kuanza kwa usaili huo mara moja.

NETO imewataka walimu na wananchi kwa ujumla kuwa na uvumilivu na kushirikiana na serikali, kwani hatua zinazochukuliwa ni za msingi na zinahitaji muda ili kuleta matokeo chanya kwa walimu na taifa kwa ujumla.
 

Attachments

  • 20250313_200221.jpg
    244.4 KB · Views: 2
Wenye Degree wameambiwa waende VETA .
 
CCM wanafanya vizuri sana. Unajua ukifuga majini ni lazima uwe na damu ya kuyalisha mara kwa mara. Haya majini CCM inayofuga yatakuja kuigeuka na kuingamiza ka sababu haina damu ya kuyalisha yote yashibe.
 
Serikali ya CCM isipoamka kutoka usingizini moto unakuja, kadiri muda unavyozidi kwenda watu wajinga ambao ndio walikuwa ni mtaji wa ccm wanazidi kupungua. Ndani ya miaka kumi na Tano ijayo nchi itakuwa imejaa maelfu kwa maelfu ya wasomi na huu uchawa unakwenda kuexpire.
 
Watoto wa wakulima wamechoka kusubili wakijaribu kudai ajira wanaambiwa wajiajiri....wazazi waliuza mashamba wakitegemea watoto watawakomboa lakini mambo yamekuwa ndivyo sivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…