Pre GE2025 Hatima ya Walimu Wasio na Ajira (NETO) kujulikana baada ya siku 45, wapongeza 4R za Rais Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
CCM Haina uwezo wa ushawishi tena. Kwa taarifa yako. Ccm inajua na ina uhakika uchaguzi ukiwa huru na haki angalau kwa 50%tu,tutaongea mengine.
Mama Samia alikuwepo 2015,awamu ya tano,na anajua wao ndio awamu pekee tangu tuanze mfumo wa vyama vingi kupitia tundu la sindano mpaka kukamata dola, pamoja na kumiliki vyombo vya dola.
Hiyo inatosha sana kumuogopesha yeye na Chama chake na huo ndio ukweli.
JPM na mbwembwe zake zote aliogopa sana uchaguzi wa 2020,kwa hofu ya matokeo ya 2015,na ndio sababu ya kuharibu uchaguzi akiamini atakuwepo kwa kuwa alidhani, amesaini makubaliano na Mungu kuwa atakuwepo kusimamia uharibifu alioufanya kwenye uchaguzi wa 2020,ili kupitisha ajenda zao za kuhakikisha katiba inabadilishwa kuondoa ukomo wa madaraka.
Sasa hiki kilichoanzishwa na hawa walimu wasio na ajira,hata kama kimeisha kwa sababu zozote zile hata kama ni kutishwa, ni wazi kimeamsha wengine kwenye fani zingine ambao ni wengi zaidi, na hili la kuwaambia graduates waende veta,mmmh. Hao waliopitia veta aliyewadanganya wote wameweza kujiari ni nani?
Hivi aliyesomea veta mfano,welding anao uwezo wa kujinunulia machine za kuchomelea,grinders na vingine? Na useremala kwamba ataendelea kutumia randa ya mkono, kweli!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…